North Korea yavutia watalii kwenda kutembelea nchini kwao

Bullava

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
550
1,000
Habari JF members!!

Balozi wa North Korea nchini Hispania KIM HYOK - CHOL amewakaribisha watu /watalii toka sehemu mbalimbali za dunia kwenda kuitembelea North Korea ili kujionea mambo mbalimbali na kueleza kuwa waombaji wa Visa watapatiwa chini ya mwezi mmoja tangu tarehe ya kuomba, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la EL Pais jijini Madrid siku ya Alhamisi wiki hii. Balozi KIM HYOK - CHOL alivilaumu vyombo vya habari vya magharibi kwa kupotosha ukweli kuhusu nchi yao kwa kuandika mambo mabaya yenye kuichafua nchi yao.
b28ae542bfc7f5e7fb0cbd3b14eb4a71.jpg

Source : RT news
Hapa JF kumekuwa na mada nyingi kuiponda North Korea kuwa kuna shida, njaa na maisha magumu kwa ujumla wake. Nadhani hii ni fursa sasa kwa wale waliokuwa wanatamani kwenda kumuona Mapanki Mzee wa Kiduku uwanja ni wenu wakuu. Mkirudi mtuletee mrejesho wa hali ya huko
4b916f622b3e1f458940ca266cff915b.jpg

d8fd551bdce28b4d3626f012ca5de293.jpg

7984e68675799819bebe61ba381cca4b.jpg

253bafb5179923373c92ea3955c50b72.jpg
 
thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,421
2,000
North Korea iko poa sana! Hawana shida kivile! We fikiria pamoja na kutengwa na dunia karibu yote na vikwazo kibao bado anaweza kuwekeza kwenye silaha kwa gharama kubwa tu!
Na ndio maana uchumi wao ni wa chini mambo mengi wanayofanya hayapo kwenye mlengo wa kiuchumi
 
Bullava

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
550
1,000
Na ndio maana uchumi wao ni wa chini mambo mengi wanayofanya hayapo kwenye mlengo wa kiuchumi
Hata kama mambo yao mengi hayapo kwenye mlengo wa kiuchumi bado uchumi wao hauwez kuwa kwa namna Western media wanavyowachafua. Propaganda western media ni kubwa kuliko maisha halisi yalivyo. Kipindi cha nyuma nilikuwa naamini North Korea haina ubalozi nchi nyingine zaidi ya China na Russia. Lakini ukisoma kupitia vyombo mbalimbali vya west na east utagundua North Korea wana mengi mazuri
 
thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,421
2,000
Hata kama mambo yao mengi hayapo kwenye mlengo wa kiuchumi bado uchumi wao hauwez kuwa kwa namna Western media wanavyowachafua. Propaganda western media ni kubwa kuliko maisha halisi yalivyo. Kipindi cha nyuma nilikuwa naamini North Korea haina ubalozi nchi nyingine zaidi ya China na Russia. Lakini ukisoma kupitia vyombo mbalimbali vya west na east utagundua North Korea wana mengi mazuri
Ni kweli kuna propaganda hasa za west lakini kwa uwezo walio nao ni hawakupaswa kuwa na uchumi mdogo
 
Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,585
2,000
Binafsi, naikubali NK na Kim Un.

Mengine, ni uchoko tu wa USA na wapuuzi wengine.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom