Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,919
- 15,604
Baada ya North Korea kuwa na changamoto ya ukame kwa muda mrefu, hatimae wamefanikiwa kutengeneza mvua (artificial rain).
Utafiti huo ambao kwa mara ya mwanzo uliripotiwa mwaka 2017 ambapo Chuo Kikuu Cha Kim-Il Sung nchini humo, kiliamua kutengeneza roketi na mizinga maalumu ya kuibusha (induce) mvua. Silaha hizo (maroketi na mizinga) walizibebesha kemikali ya Silver Iodide na dry Ice kisha kuzivurumisha kwenda tabakahewa (artmosphere). Kemikali hizo hubadili kiwango cha unyevunyevu ktk tabakahewa, kufanya mawingu mvua, kisha mvua kumwagika ardhini.
Teknolojia hiyo itabadili mabadiliko hatarishi ya hali ya hewa na hivyo kuepusha ukame, kuhakikisha upatikanaji wa maji ya kutosha (mvua) na ya uhakika kwa ajili ya matumizi ya kilimo na ufuaji umeme.
Halafu utasikia Wamarekani wa Nanyamba wakiibeza North Korea ktk maendeleo ya sayansi na teknolojia!
Source: Fox News
======