North Korea 'executes vice premier over forestry dispute'

huyu angekua hapa tz yaani sipati picha wale wakusinzia sijui wangekua wapi leo hii
 
Hivi huyu dikteta wa Korea Kaskazini ni Kim Jong Un ni mwehu? Mwezi Mei mwaka alimuua hadharani Waziri wake wa Ulinzi kwa kosa la kusinzia wakati yeye akihutubia, mwaka juzi alimuua mjomba wake kwa kumhisi kutaka kumpindua na hivi karibuni kamuua Naibu Waziri mkuu wake kwa kutofautiana naye juu ya sera ya misitu.

Yeye anasimamia kupunguza idadi misitu kwa sababu nchi imekuwa pori na Rais hataki, hilo tu kagongwa risasi hadharani.

Huyu angekuwa huku kwetu rushwa ya uchaguzi ingejifuta yenyewe.
Umesahau kutaja na girlfriend wake 2013, aliyeuawa hadharani na firing squad?
Hakuna aliye salama nchini humo!
 
Ohpss!.kumbe ni wa 1983 bado ni kijana mdogo sanaa basi korea kaskazini wanahitaji kuwa na subira kwani akikua ataacha.hayo ni makuzi tuu.R.I.P naibu waziri uliye katishwa maisha yako ya hapa duniani.Lakini maraisi kama hawa wangekuwepo Africa ata Tembo wetu wasingetoweka hivi aiseee.
 
Eehh Mungu tujaalie na sisi Watanzania tupate kiongozi mwenye uthubutu kama huyu ili mafisadi yakimbie nchi na kurudisha heshima ya taifa hili.
 
Tatizo sio Rais, tatizo ni ukominist, ukominist ni kama imani flani ambayo kila anayekuwa na mawazo tofauti lazima auwawe. Watu wamechoka hiyo siasa, wenzao wa kusini uchumi unapaa, wao ni njaa tu! Eti usawa!!
 
Huyu dogo kama angekuwa rais wa Tz sijui kama tungesalimika manake angetumaliza kabisa!!!!

Hapa bongo uwaziri watu tunaupigania..nchini Korea kwa bwana mdogo ukipewa uwaziri jua ukizembea tu umeenda na maji..dogo hana utani.
Kuna waziri alimpiga bomu majuzi kwa kusinzia wakati wa hotuba...
 
Umesahau kutaja na girlfriend wake 2013, aliyeuawa hadharani na firing squad?
Hakuna aliye salama nchini humo!

Huyu akiendelea hivi atakuja kupinduliwa tu, haiwezekani kila mtu awe anajihisi wa kunyongwa/kuuawa kesho alafu ubaki salama.Siku zake nae zinahesabika tu.
 
dogo nouma kosa kidogo tu unajaa kwenye jeneza. , hataki mchezo

Huyu ni kichaa,toka lini kosa la kusinzia likawa hukumu ya kifo?angemfukuza kazi hapo sasa.

Huyu jamaa ata kwenye vikao vya cabinet nadhan mawaziri wanapoenda uwa wanaaga kabisa nyumbani wakijua kuwa yawezekana wanaenda kuuawa, maana bila shaka ukipinga hoja au ukaonekana unajua sana au ukionekana umekunja uso au umecheka au umemkazia macho au umeangalia pembeni unaweza kunyongwa hapohapo,yaan kila kitu ni mtego tu,maisha gani hayo?eneo kama hili ndipo kujitoa mhanga kunapokuwa na maana.
 
Huyo jamaa naamini ipo siku nae ataingia kwenye mikono ya mabandidu zaidi yake tena hapo hapo Nchini kwake,muosha huoshwa.
 
Huyo jamaa naamini ipo siku nae ataingia kwenye mikono ya mabandidu zaidi yake tena hapo hapo Nchini kwake,muosha huoshwa.

Huyo ukoo wao ndivyo walivyo mkuu. Babu alifanya hivyo, Baba hivyo hivyo, ila yeye nafikiri anataka awazidi wote ahahahaha
wamarekani wanamuogopa sana jamaa. Hana mzaa hata kidogo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom