Nombeni msaada wa sheria ya ardhi kuna mzee karithi mirathi alafu anasumbua majirani

Developer IOS

JF-Expert Member
Jun 20, 2017
1,457
1,409
Ndugu zangu wana jamiiforums naombeni msaada wa sheria ya ardhi.Kuna mzee mmoja karithi mirathi ya bibi mmoja lakini amekuwa akisumbua majirani mara azibe njia muhimu mara adai maeneo yote yake.

Leo kawaletea majirani zaidi ya wa 5 barua kutoka baraza la ushuluhishi wa ardhi kuwa wapo katika eneo lake akiomba mahakama iamuru nyumba zote zivunjwe wakati baadhi ya nyumba zipo tokea mwaka 1975 na mwenyewe hakuwahi kulalamika lakini yeye ndo anadai ni kwake.

JE TUKISHINDA KESI TUNAWEZA KUMFUNGULIA KESI YA MADAI

MSAADA PLEASE
 
Inawezekana mwenye ardhi hajawahi kulalamika lakini ardhi ilikuwa yake aliwaachia tu kikubwa muwe na vielelezo vinavyothibitisha hayo maeneo ni yenu kihalali.
 
Umesema hiyo kesi iko baraza la usuluhishi? Au ulikusudia Baraza la Ardhi
 
Ndugu zangu wana jamiiforums naombeni msaada wa sheria ya ardhi.Kuna mzee mmoja karithi mirathi ya bibi mmoja lakini amekuwa akisumbua majirani mara azibe njia muhimu mara adai maeneo yote yake.Leo kawaletea majirani zaidi ya wa 5 barua kutoka baraza la ushuluhishi wa ardhi kuwa wapo katika eneo lake akiomba mahakama iamuru nyumba zote zivunjwe wakati baadhi ya nyumba zipo tokea mwaka 1975 na mwenyewe hakuwahi kulalamika lakini yeye ndo anadai ni kwake.
JE TUKISHINDA KESI TUNAWEZA KUMFUNGULIA KESI YA MADAI
MSAADA PLEASE
.

Hapo naona swali lako ni je tukishinda kesi tunaweza kimfungulia kesi ya madai?
Ndugu programmer95 hiyo haitawezekana. kesi mliyofunguliwa huko barazani ni ya madai na madai yanahusu ardhi. Basi kama mna madai yenu nanyi kuhusu ardhi hiyo dhidi ya mshtaki wenu wekeni madai hayo katika kesi hiyo hiyo. Vinginevyo kesi ikiisha mtaweza kudai gharama za kesi, na hii itakubalika tu kama baraza litaluhusu/litatoa order ya gharama kwa upande wenu dhidi ya mshtaki wenu
 
Back
Top Bottom