Noma sana

Kabisaaaa.

Sesten Zakazaka njoo uone chapati huku. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Mi nimependa hizo za Arusha. 😎😎
Shadeeya hizo za Arusha zimepikwa kwa ngano isiyokobolewa? Lakini kama nausoma moyo wako vile umedondokea kwenye kitu cha Tanga :D

Mimi hapo kwenye hizo za Tanga hunitoi aisee, halafu angalia zilivyokunjwa yaani Kimakororamakorora hivi:p:p:p
 
Shadeeya hizo za Arusha zimepikwa kwa ngano isiyokobolewa?
Itakuwa unga wa kawaida tu Ses ila si wajua tena kupika ni kipaji.
Lakini kama nausoma moyo wako vile umedondokea kwenye kitu cha Tanga :D
πŸ™ˆπŸ™ˆπŸ™ˆπŸ™ˆ

Mimi hapo kwenye hizo za Tanga hunitoi aisee, halafu angalia zilivyokunjwa yaani Kimakororamakorora hivi:p:p:p
Hapo wenyewe nasikia huwa chapati ka hizo wanakula na yale Maharage yale ya kukata na chai ya maziwa pembeni. πŸ˜€πŸ˜€
 
Itakuwa unga wa kawaida tu Ses ila si wajua tena kupika ni kipaji.
Nimefurahi na hilo neno "kipaji". Wanikumbusha chapati zikiwa nzuri unasifiwa unga wa ngani ndio mzuri, zikiwa zimekataa mapishi basi lawama anatupiwa mpishi, sasa Shadeeya umeamua kumwagia sifa mpishi hivyohivyo japo ukawka anagalizo kua akipata uzoefu atatoa nzuri zaid :p :p :p
Hapo wenyewe nasikia huwa chapati ka hizo wanakula na yale Maharage yale ya kukata na chai ya maziwa pembeni. πŸ˜€πŸ˜€
Yanaitwa maharage ya kuparaza na chai ya maziwa wanaita chai kiwete maana yake hata ikimwagika haitawanyiki jinsi maziwa yalivyokua mazito, hahahaaa watu wa Tanga!
 
Nimefurahi na hilo neno "kipaji". Wanikumbusha chapati zikiwa nzuri unasifiwa unga wa ngani ndio mzuri, zikiwa zimekataa mapishi basi lawama anatupiwa mpishi, sasa Shadeeya umeamua kumwagia sifa mpishi hivyohivyo japo ukawka anagalizo kua akipata uzoefu atatoa nzuri zaid :p :p :p
Ndio Ses huyo mpishi pole pole naye atakuwa mjuzi tu huko mbeleni.

Yanaitwa maharage ya kuparaza na chai ya maziwa wanaita chai kiwete maana yake hata ikimwagika haitawanyiki jinsi maziwa yalivyokua mazito, hahahaaa watu wa Tanga!
Bora umenisaidia kunipa Kiswahili kinachotumika huko. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Hebu fanya hamu siku moja nawe upitepite mitaa ya Mikanjuni, Sahare, Makorora, Mabanda ya Papa, Ngamiani n.k usikie harufu ya hiliki na viungo kuanzia vya chai hadi vya pilau. Wenyewe wanasema watu wa Bara wanachemsha chai wakati Tanga chai yapikwa :D :p ;)
 
Hapo umekua kama muibua vipaji maana umegundua kipaji cha baadae atakakachokuja kua nacho mpishi wetu eeh? Ila hebu mpe nasaha zako kwa sasa
Hahahaaa. Nasaha zangu ni kwamba apike mara kwa mara tu basi mwisho wa siku atafikia hapo alipofikia huyo wa Tanga.

Sababu si ajabu huyo wa Tanga naye alitoka huko huko. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Hebu fanya hamu siku moja nawe upitepite mitaa ya Mikanjuni, Sahare, Makorora, Mabanda ya Papa, Ngamiani n.k usikie harufu ya hiliki na viungo kuanzia vya chai hadi vya pilau. Wenyewe wanasema watu wa Bara wanachemsha chai wakati Tanga chai yapikwa :D :p ;)
Ewaaaaa. Usijali Ses natumai utakuwa mwenyeji wangu. 😎
 
Hahahaaa. Nasaha zangu ni kwamba apike mara kwa mara tu basi mwisho wa siku atafikia hapo alipofikia huyo wa Tanga.

Sababu si ajabu huyo wa Tanga naye alitoka huko huko. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Hapo umemaliza Shadeeya, nasaha zinajieleza zenyewe. Na mimi basi anomba shule ya mapishiπŸ₯΅πŸ˜…
 
Arusha na Kilimanjaro ni ziro kabisa, sijapata ona watu wasiojuwa kupika kama wa hiyo mikoa. Mchagga akikupikia wali basi tegemea kula mawe, akikupikia ugali tegemea kupigana na makunja/magolori yasiyowiva. Akikuchomea nyama ndiyo kabisa, utakula mkaa/jiwe yaani nyama inakauka mpaka inakosa radha.
Bora kidogo hao mkuu, usiombe ipikiwe wali na muhaya daaaaah, utokula kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom