Nokia zinachangia kuharibu mahusiano/ndoa!!! "SCREENED MESSAGES"

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,801
6,231
"Pole sana rafiki!" Haya ni maneno ya faraja niliyompa rafiki yangu kipenzi baada ya kukutwa na dhahma!!!

Alikua na demu wake wanapendana sana, bilashaka siku chache zijazo tungevaa suti kuelekea kanisani na baadaye ukumbini....

Demu wake ana Nokia, anadai alimkuta anasoma msg aliyoidhania kwamba inatoka kwa basha mwingine wa huyo dada....

Ghafla yule dada akabonyesha kitufe cha "back" mara tatu, simu ikarudi kwenye MENU KUU, jamaa kujaribu kwenda INBOX hakuikuta tena ile msg! Akajiona faaaalaaaa!!!

Aliponisimulia nikamwambia kuna kitu kinaitwa screened msg, hapa mtumiaji wa simu anaziandika namba ambazo msg zake zikiingia basi simu yake isitoe mlio wala hiyo msg isiingie kwenye folder la INBOX, bali inaenda kwenye folder la SCREENED MSGS, so inabidi mtumiaji wa hiyo simu awe analitembela folder la SCREENED MSGS kuchek kama kuna msg mpya... Nikamuelekeza jinsi ya kuzifikia SCREENED MSGS

Jana karudi kwa dem wake, akaenda kwenye hilo folder la SCREENED MSGS akakuta msgs kama 80 hivi za mabasha tofautitofauti wa huyo manzi wake, almanusura azimie...

Jamani kwa wenye tabia hii muache, na msiofahamu, watch out! NIMEMALIZA...


:disapointed:
 
mie yangu nimeweka folder kabisa kwa namba ya hny ikiingia msg direct inaenda kwa folder yake.
Msg zake tamu zisichanganyike za kufowadiana na za kina Mentor.
 
Last edited by a moderator:
haaa kuna watu wanajifanya wapole sim anamwachia mwenzi wake
nae utakuta anajisif mi sim yake nakaa nayo mda wote
we katiza upande wa sceened massage utakutana na Majanga
 
^^
Loo! Kagua kagua hii unaweza kunywa sumu bure.
Hesabu rahisi
Let mpenzi=1
Ukikagua utakuta
mpenzi=11
hapo jibu linakuwa
mpenzi=X
^^
 
Nokia zina flash sms ambazo hufutika kwa nn hakutumia hzo

Mkuu si unajua tena watoto wa kike, ukimtext akishaisoma txt yako huwa anairudia mara kwa mara, sasa zile flash sms ikiingia tu kwny sim inajifungua yenyewe, ukibofya "back" tu inapotea...sasa ataikosa akitaka kuisoma tena usiku akiwa analala hahaha
 
mie yangu nimeweka folder kabisa kwa namba ya hny ikiingia msg direct inaenda kwa folder yake.
Msg zake tamu zisichanganyike za kufowadiana na za kina Mentor.

Am sure na mimi nina kafolder maalumu....! msg zangu zisichanganyike na za vizee kama Asprin.
 
Last edited by a moderator:
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom