nokia yazindua asha 205 na asha 206 return of candybar

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,689
39,755
ni juzi tu samsung alizindua simu ya kufunua yenye candybar na leo nae nokia katoa simu ya candybar je hii inamaanisha nini? Kama hujui candybar ni simu zenye button 3 kiupana ambazo ukitype message button moja ina herufi 3. Mfano unataka herufi f itabidi ubonyeze namba 3 mara 3.

Nokia leo wamezindua nokia asha 205 na 206 je kipi kipya kutofautisha na simu za mwanzo?

13c9nokia-asha-205-206-600x476.jpg


nokia asha 205 ndo ina qwerty na 206 ina candybar

slam sharing
hii simu ni ya kiafrica na kiasia zaidi ndo maana ikaekwa slam sharing. Hii ni feature mpya ya kuhamisha vitu kwa bluetooth bila kupair device.

fabula design kwa nokia 206
hii ni design ya nokia lumia zote na naona sasa imehamia kwenye nokia asha. The way camera ilipo na edge corner
proxy2.jpg


dedicated facebook button

Nokia 205 itakua na dedicated facebook button ambayo ukibonyeza hapo hapo unakua facebook.
proxy.jpg


pre loaded apps
moja ya vitu vilivonivutia ni apps ambazo zitakuja na simu hizi kwa ujumla utakuta apps 40 zimeshakua installed na nyingi kati ya hizo ni zile top games na app kama mig33 (zimezinduliwa indonesia hizi simu)

bei
bei imeuzwa indonesia rupia laki 6 ambazo ni kama shilingi laki 1 ya bongo su tuzi expect labda kwa laki na 20
 
Mambo ni SMART PHONE. Hizi za kuvaa miwani ndiyo utumie naona nipumzike nazo. Kiboko ni Tablet yenye simu na Camera maana unafanya kila kitu ndani yake.

BPhone-5-inch-Tablet-Phone.jpg
 
Hiyo ya candybar ndo naisubiri aisee nimesha choka kubofya kioo nataka kurudi kene buttons aisee but kene SMS hakuna threaded view
 
cool... Ila mm nokia wanaanza kuniboa ... Bado mpaka leo cjaskia smartphone ya windows ambayo itakua cheap atleast hata laki 3
 
cool... Ila mm nokia wanaanza kuniboa ... Bado mpaka leo cjaskia smartphone ya windows ambayo itakua cheap atleast hata laki 3

nokia 510 ni laki 3 na nokia 610 ni laki 3 na elf 40 nokia 710 ni laki 3 na elf 70.

Hio 510 nimeongea for experience na 610 na 710 nimeziona dukani. Sema 610 na 510 zina ram 256 so uwe makini zina limit sana japo wp7.8 update yake ni ya ukweli

ila huawei w1 itakua na double core 1.2ghz na itatumia wp8 na bei chini ya 200usd itakua ndo simu rahisi zaidi ya wp8 hii ikitoka ikiuzwa na mitandao ya simu kama tigo tutaipata kwa chini ya laki 2
 
Wee na wewe vipi tena? Ukiona Mchina anayo basi ujuwe kaiga kwa akina Samsung, Nokia, Asus nk.

Mara nyingi hiyo tablet inakuwa peke yake na wajanja wanazitengenezea Keyboard na unaweza kuunganisha.

Samsung Galaxy Tab 10.1 Keyboard Dock Revisited - This Time With TouchWiz UX

ASUS_EeePadTransformer_4.jpg

440x330-xperia-tablet-s-keyboard.jpg


Pichani ni SONY S 3G. na juu ni ASUS ambazo kama umegundua, ni Taiwan na Japan na siyo Mchina kama unavyofikiria.

Ukitaka kujua haya mambo, uwe unatembelea GSMARENA. Wale jamaa nawaaminia sana ingawa pia huwa nikitaka habari zaidi basi huenda Website nyingine nyingi na haswa youtube kuangalia Video za product.

Kuhusu simu yangu, natumia Nokia na sijawahi kutumia Mchina hata siku moja. Kuhusu ku-install programs, mhhh... Desktop yangu nimeunda mwenyewe na ku-edit mwenyewe BIOS na mwisho nika-install mwenyewe program zote kwenye computer. Nikipata shida, huwa namuuliza GOOGLE. Kwa asilimia 99 huwa ananipa jibu na nikishindwa, kuna mshikaji anafanya kazi IBM huwa ananipa jibu kamili la nini la kufanya. Hivyo usiwe na wasiwasi kuwa ntakusumbua jinsi ya ku-install OPERA

mkuu ndo simu gan hii? We chezea mchina tu utakuja kuona madhara yake.

Usije tuuliza tu unainstall vp opera
 
ila si wachina wote wanaiga samsung kuna huawei na zte wanatengeneza product nzuri tu mfano mzuri ona modem unayotumia toka internaet imeanzishwa tz hadi leo ni wao.

Na mwakani zte anatoa simu yenye 8 core imekua codenamed apache (mpaka sasa simu yenye core nyingi ni 3) so imagine mwenyewe from 3 to 8.

Then angalia xiaomi na meizu hawa ni wachina xiaomi ndo simu yenye rich specs ya android
 
Kwa sasa hilo KOPO silitumii kwa kweli. Lipo tu na nafikiria kuligawa maana kuliuza ni hasara sana ukilinganisha na bei niliyonunulia parts zake. Nilichonacho hapa ni Box tu la Motherboar MSI KT4AV for AMD Athlon XP CPU.
Nilikuja kugundua kuwa Laptop itanisaidia sana na nikanunua Asus baada ya kusoma kuwa zinadumu sana na hazirudi Service kwa wingi. Ila cha ajabu nikawa nimenunua F3 ambazo kumbe zina matatizo sana ya Sound Card kufa. Baada ya miezi mitatu, nikaipeleka Service na ikapona. Nimeitumia kama miaka 4 na ghafla ikazimika. Kumbe graphic cards imekufa. Service wakatengeneza kwa kulipia (huwa sigusi kabisa Laptop ndani, ila nafikiri ntaanza baada ya kuwa Service mara kadhaa nimegundua si kazi sana). Ila baada ya kutumia kwa kama miaka 2, ikazimika tena na nikampa Mshikaji mmoja ila nikanyofoa Hard Disc. Yeye akasema atatengeneza na ampe dada yake ila akakuta kumbe ni Motherboard imekufa.....

Kwa sasa natumia Laptops..... sijui ipi maana zipo tu nyumbani na iliyowazi ni haki yangu. Ila kwa sasa hata Laptops ununuzi wake na matumizi umepungua sana huku Tablet na Smartphone zikichukua namba moja.

tupe specs za computer yako uliounda mwenyewe
 
Mkuu,

Huawej nawafahamu sana na habari zao huwa ninazipata kwa ukaribu sana. Nafahamu sana ubabe wao ingawa kwenye smartphones na Tablets kwa kweli wameachwa kidogo na hasa kwenye kutangaza biashara na ubora wa bidhaa.

Kuna JF member anaitwa Mtanzania ambaye ni mfanyakazi wa hiyo kampuni huko UK, huwa nikimpata kwenye SKYPE basi hunipa story zao kwa sana na hasa kama ndiyo kwanza amerudi kutoka HQ ya Huawei huko China.

Kuhusu bidhaa zao, nakiri kuwa hadi leo sijatumia yoyote iliyoandikwa hilo jina. Ila inawezekana nimetumia tuseme imeandikwa Vodacom ila kumbe ndani ni Huawei. Pia mitambo ya simu na Internet ya hao Voda inaweza kuwa ya hao Huawei, hilo silifahamu.

Ila hizo Core 8, si itakuwa upuuzi tu kama huna Internet speed kubwa, RAM za kutosha na graphic card nzuri. Vinginevyo itakuwa ni sawa na kununua Kamera ya Pixels kibao ila ZOOM ni mbovu na Engine ya Camera mbovu. Anyway, ngoja tusubiri tuzione zitafanya maajabu gani......
ila si wachina wote wanaiga samsung kuna huawei na zte wanatengeneza product nzuri tu mfano mzuri ona modem unayotumia toka internaet imeanzishwa tz hadi leo ni wao.

Na mwakani zte anatoa simu yenye 8 core imekua codenamed apache (mpaka sasa simu yenye core nyingi ni 3) so imagine mwenyewe from 3 to 8.

Then angalia xiaomi na meizu hawa ni wachina xiaomi ndo simu yenye rich specs ya android
 
Hiyo ya candybar ndo naisubiri aisee nimesha choka kubofya kioo nataka kurudi kene buttons aisee but kene SMS hakuna threaded view

Mimi kwa candybar hunitoi.
Natumia Symbian s60 Nokia E52 mpaka leo... Sitaki kusikia hayo matouchskrin yaenu!
 
ndo hio hio inaiwa c5-00 5mp sema haina wifi ila vitu vyengine ipo safi sana

Nimeitazama GSMarena, iko poa sana na ndiyo niliyokuwa naitafuta hiyo.
Wi-Fi si muhimu sana kwa kuwa inamaliza chaji... Ngoja nii-shortlist kwa matumizi ya baadae!
 
ila si wachina wote wanaiga samsung kuna huawei na zte wanatengeneza product nzuri tu mfano mzuri ona modem unayotumia toka internaet imeanzishwa tz hadi leo ni wao.

Na mwakani zte anatoa simu yenye 8 core imekua codenamed apache (mpaka sasa simu yenye core nyingi ni 3) so imagine mwenyewe from 3 to 8.

Then angalia xiaomi na meizu hawa ni wachina xiaomi ndo simu yenye rich specs ya android

Hv mkuu kwani quad core it means znakua core ngapii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom