Nokia Yatoa Simu Zinazochajiwa na Baiskeli

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Kampuni kongwe ya simu duniani, Nokia imezitambulisha simu zake mpya za bei chee zenye laini (SIM card) mbili ambazo betri zake huchajiwa na dainamo ya baiskeli.
Simu hizo zilitambulishwa kwa watu jana nchini Kenya ambapo Nokia imesema kuwa imelenga kuziuza kwa bei chee ingawa simu hizo ndio zitakuwa simu za kwanza za Nokia kutumia laini mbili.

Simu hizo pia zina radio na tochi na vionjo vingine vya kawaida.

Simu hizo zinazoitwa Nokia C1-00 zitauzwa kati ya Tsh. 50,000 na Tsh. 90,000 wakati chaja yake itakayotumika kwenye baiskeli itauzwa kuanzia Tsh. 15,000.

Chaja ya simu hiyo inatumia dainamo ya baiskeli hivyo spidi ya mtu kuendesha baiskeli ndivyo betri litakavyojaa chaja nyingi.

Safari ya dakika 10 kwa spidi ya kilomita 10 kwa saa italichaji betri na kukuwezesha kuongea mfululizo dakika 28 au masaa ya 37 ya simu kuwa ON.

Nokia imesema kuwa simu hizo zimelenga zaidi maeneo ya Afrika ambako umeme unapatikana kwa tabu.
 
kwa kweli safi sana tutawasiliana na ndugu zetu huko vijijini kwa urahisi sana
 
Kampuni kongwe ya simu duniani, Nokia imezitambulisha simu zake mpya za bei chee zenye laini (SIM card) mbili ambazo betri zake huchajiwa na dainamo ya baiskeli.............

Nadhni hapa Nokia wanapromote zaidi hizi simu zenye laini mbili na ya bei chee kwa soko la africa . Kuchaji simu kwa basikeli ni teknolojia nokia walikuwanayo toka zamani

ukitembelea Nokia Europe - Nokia Bicycle Charger Kit - Overview utaona kwenye compatibility karibu simu nyingi zinaweza kuchajiwa kwa dynamo
 
Back
Top Bottom