Nokia Yatoa Simu Zinazochajiwa na Baiskeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nokia Yatoa Simu Zinazochajiwa na Baiskeli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 14, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kampuni kongwe ya simu duniani, Nokia imezitambulisha simu zake mpya za bei chee zenye laini (SIM card) mbili ambazo betri zake huchajiwa na dainamo ya baiskeli.
  Simu hizo zilitambulishwa kwa watu jana nchini Kenya ambapo Nokia imesema kuwa imelenga kuziuza kwa bei chee ingawa simu hizo ndio zitakuwa simu za kwanza za Nokia kutumia laini mbili.

  Simu hizo pia zina radio na tochi na vionjo vingine vya kawaida.

  Simu hizo zinazoitwa Nokia C1-00 zitauzwa kati ya Tsh. 50,000 na Tsh. 90,000 wakati chaja yake itakayotumika kwenye baiskeli itauzwa kuanzia Tsh. 15,000.

  Chaja ya simu hiyo inatumia dainamo ya baiskeli hivyo spidi ya mtu kuendesha baiskeli ndivyo betri litakavyojaa chaja nyingi.

  Safari ya dakika 10 kwa spidi ya kilomita 10 kwa saa italichaji betri na kukuwezesha kuongea mfululizo dakika 28 au masaa ya 37 ya simu kuwa ON.

  Nokia imesema kuwa simu hizo zimelenga zaidi maeneo ya Afrika ambako umeme unapatikana kwa tabu.
   
 2. k

  kirongaya Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  kwa kweli safi sana tutawasiliana na ndugu zetu huko vijijini kwa urahisi sana
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nadhni hapa Nokia wanapromote zaidi hizi simu zenye laini mbili na ya bei chee kwa soko la africa . Kuchaji simu kwa basikeli ni teknolojia nokia walikuwanayo toka zamani

  ukitembelea Nokia Europe - Nokia Bicycle Charger Kit - Overview utaona kwenye compatibility karibu simu nyingi zinaweza kuchajiwa kwa dynamo
   
Loading...