Noah inazingua sana (linamiss na kuwaka taa ya check engine) naombeni msaada

KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
2,149
4,752
Nina gari aina ya Noah new shape injin ya 1az.. Sasa limekua likisumbua miss muda mrefu hatimaye limebadilishwa vitu kabao hadi Sasa bado halijaaa sawa...

Shida ya sasa ni kwamba asubuhi ukiliwasha badala ya kuleta Ile kama resi hadi oil upande ndo litulie limekua likileta miss na some times had upige ress kidogo ndo litakaa sawa.

Na la pili ni kwamba wakali linatembea barabaran gafla linawaka taa ya check injin na linaendelea kwenda lakini muda mwingine linazima gafla ukitaka kuliwasha unakuta halionesh taa ya injin na betri so had zijitokeze ndio linawaka inaakua kama Kuna wire zinacheza sasa mafundi wamehangaika nalo limeshindikana

sent from HUAWEI
 
Tatizo ni kwamba ukiwasha gari yako inaanza na cold start badala ya warm start coz engine asubuhi inakua ya baridi na inahitaji warm start ili ifanye kazi sawia. Kwa cold start ndo maana unapata tatizo la miss.

Na sababu ya kusema ukipiga less ndo gari inakaa sawa ni kwa sababu hapo unakua unaipasha engine ndipo inakaa sawa.

Tunatibuje tatizo lako?
Kwa haraka kutokana na maelezo yako tatizo lipo kwenye engine control unit ndo maana inashindwa kuset engine system ifanye Warm Start pale mwanzo coz engine inakua ya baridi na inahitaji joto. Maelezo mengine yako very technical na itakua ngumu kunielewa

Kama unaweza kufika Lindi Niletee hio gari. Kuna garage ya kisasa hapo Lindi inaitwa Kahawa Motors (kahawamotors.com). Niko hapo.

Lakini kama hauwezi kuja Lindi unaweza kuwasiliana nami nikupe mwongozo zaidi.

KWA MATATIZO YA ECU KAMA HAYO UTAHANGAIKA SANA KWA MAFUNDI WABABAISHAJI KUKUINGIZA GHARAMA ZA KUBADILISHA VIFAA KWA SABABU HAWANA UELEWA NA HIZO COMPUTER ZA KWENYE MAGARI
 
Tatizo la gari kumiss;

Check coil kama zinafanya kazi, njia moja ya kucheki coil yenye tatizo, washa gari yako, anza kuchomoa moja moja na utizame gari itabadilika mlio, ukiona umechomoa coil na kuona mlio wa gari haubadiliki ujue hapo ndio kwenye tatizo, sasa kumake sure kama ni coil ibadilishe weka kwenye cylinder nyengine halafu urudie process, ukiona kwenye coil hio hio mlio haubadiliki, basi tatizo ni hio coil, na kama mlio unabadilika basi pale ulipoitoa kuna tatizo la plug.

Kama coil na plug sio tatizo, kuna culprit mwengine wa Oxygen sensor, kujua kama gari yako kama inazo oxygen sensor, check kwenye engine, zile pipe zinazokwenda kwenye exhaust pipes, zifuate utizame kama zinayo sensor, inakuwa screwed na hio pipe ya exhaust.

Hayo nlokwambia yote yanasababisha gari kuwaka taa ya check engine, la mwanzo ukifanya diagnosis kwa computer itakwambia cylinder ipi ina miss, na la Oxygen sensor itakwambia kama ni oxygen sensor.
 
hahahahaha mkuu ww ni fundi?? au maana maelezo unayoyaandika hayaendani na ukweli au uhalisia wa tatizo husika?? ni kama unayafyatua tuu google.

Haaahaaaa

Ww ndo hauelewi nlichoongelea au ulipoona neno "charging system" umeelewa tofauti?? Namaanisha system ya kuingiza hewa kwenye gari ambayo huwa ina sensors za kuangalia temperature ya hewa inayoingia na kuzituma kwenye control box(ECU) ili ifanye adjustments

Tatizo liko wazi kabisa coz hata mhusika anasema akipiga less ndo miss inastop coz hapo anakua anaipasha engine

Anyway muache aendelee kuzunguka kwa mafundi
 
kali linux,
LEGE alivokuuliza hajakosea.

System ya kuingiza hewa kwenye gari ni MAF sensor, hii hupima kiasi cha hewa kinachoingia ndani ya engine ambayo inaipa taarifa ECU kiasi gani cha mafuta iweke kwenye engine. Hii haina uhusiano na temperature ya engine. Temperature ya engine inatizamwa na thermostat ambayo ina regulate temperature ya gari.

Charging system uzungumzie kuhusu alternator, ndio inayocharge betry na kupeleka umeme kwenye instruments.

Gari yenye kumiss ukipiga race inatulia, na kumissi kwa gari kuna possibility kubwa ni coil, plug ama O2 sensor.
 
chilubi,
Hatujaelewana tu. Mie nlikua namaanisha turbocharging ambayo kwa kifupi tumezoea kuiita "air charging system au supercharging"

Hivi hata kwa akili za kawaida tu ukute watu wanaongelea tatizo la kuingiza hewa kwenye gari na wanatumia term "charging" kweli kabisa na ufundi wako unaweza kuanza kuongelea kucharge battery???

Anyway tumetofautiana lugha.

Na unaongelea tatizo la miss, sawa hizo sababu ulizotaja hapo zinasababisha miss lkn sio sababu pekee. Sijui niseme mara ngapi hii kitu let me say it for the last time

"ENGINE INAPOANZA KAZI ASUBUHI INAKUA YA BARIDI SANA INLET MANIFOLDS ZOTE ZINAKUA ZA BARIDI, SO HEWA(AIR) IKIINGIA IKAGUSA KUTA ZA INLET MANIFOLD TEMPERATURE YAKE INASHUKA, KAMA ILIKUA NI 27°C BASI INAWEZA SHUKA HADI 20°C.

EFFECT YA HILO NI KWAMBA KAMA ENGINE INATUMIA DIESEL BASI BAADA YA COMPRESSION YA AIR KWENYE CYLINDERS, AIR HAITOFIKIA JOTO AMBALO LITALETA SELF COMBUSTION(MLIPUKO) BAADA YA DIESEL KUFUKIZWA KWENYE CYLINDERS. HII NDIO INAYOKUJA KUSABABISHA TATIZO LA MISS COZ KUNA PISTON ZITAFANYA KAZI OUT OF PHASE NA KUSABABISHA ENGINE IANZE KUSHAKE."

****REJEA MAELEZO YA MHUSIKA, KASEMA MISS INATOKEA ASUBUHI AKIWASHA GARI.

mbona kitu rahisi kuelewa hicho mkuu, sijui mnachofanya kionekane kigumu ni kipi. Mimi sio fundi mechanic lkn nadeal na ECU remapping. So jamaa yako hapo juu alikua sahihi kusema mm sio fundi
 
Fundi asiye na diagnosis tools hagusi gari yangu,period.

Labda yawe haya matatizo ya pancha,kubadili oil na mambo mengine kama hayo lkn nje ya hapo mambo ya Trial&errors sio kabisa.
 
kali linux,
Unaona sasa boss toyota noah na turbocharg wapi na wapi ???.acha kutoa ushauri mwingi wa kupoteza unachokiongelea hakipo kabisa kwanza unaleta maelezo ya gari ya disel sijui baridi hiyo kitu haipo in short tatizo lake lipo hivi.

akiwasha gari linakuwa na miss akikanyagia inaondoka hapo tuna sema mchanganyiko wa hewa na mafuta haupo sahihi.. na shida hiyo inasababishwa na vitu vingi tuu.. kwanza kwa aina ya gari aliyoisema noah bila shaka itakuwa noah new model yenye engine ya 1AZ FSE. hapo shida mara nyingi ni nozel zinaweza zikawa zishakuwa majanga na kwenye gari nyingi hii hutokea sababu wengi huwa wanatoa thermostata.

kingine airclener pia inaweza ikawa imechoka au plug majanga.. pia kagua na throttle inaweza ikawa chafu.

hakuna ugonjwa wakutisha hapo kama upo dar nitafute mm nitakupimia na mashine buree .shida ikijulikana ukitaka nikutengenezee nitakuchaji kijf jf au unafundi wako anakwenda anakulekebishia maisha yanasonga.

fundi ukishindwa kutengeneza GARI ZA TOYOTA ACHA UFUNDI KABISÀA
 
Fundi asiye na diagnosis tools hagusi gari yangu,period.

Labda yawe haya matatizo ya pancha,kubadili oil na mambo mengine kama hayo lkn nje ya hapo mambo ya Trial&errors sio kabisa.
kwani diagnosis ndio inatengeneza gari mkuu??. mashine zipo na unaweza ukapima na mashine na bado gari ikakuchapa vile vile?? na hizi gari za TOYOTA ndio hamna kitu kabisaa..na wengi mafundi na wenye magari wamelemaa na kulemazwa na mashine..na kuna aina ya shida lazima upige manually kwanza kama gari inakubali kupimwa na mashine ni basi mm naweza nikaipima yenyewe manually ikanipa jibu sahihi zaidi kuliko hata ukitumia mashine..
 
LEGE,
Zile habari zenu za mafundi kuchukua toilet paper iliyoloa maji na kuingiza kwny exhaust na mnaangalia masizi sijui yamefanya nini ndo mjue kitu gani kinaendelea huko ndo nije niwaamini?Fundi anayetengeneza gari yangu ni mwenye diagnosia machines na mwenye kujua anachokifanya,period.Na tangu nimeanza kutumia mfumo huu sijawahi kufeli.

Mfano mzuri tu, kwny hii thread ya Noah tu tayari mafundi mmeshapishana mbaya kabisa kusema nini solution ya tatizo la hio Noah ni mwendo wa kufanya trial&error tu mwanzo mwisho.

Mafundi gonga nyundo walishaniharibia gari yangu na wakishaharibu hua hawana aibu kabisa wanakwambia kirahisi rahisi tu,hio ishakufa tayari boss.Nilishanunulishwa na mafundi spares kwa sana tu wkt hazihusiki na tatizo husika.

No wonder Mercedes/Bimmer/Audi/Vw zina mafundi wachache sana mtaani maana wengi bado wako analogy.
 
chilubi,
Hatujaelewana tu. Mie nlikua namaanisha turbocharging ambayo kwa kifupi tumezoea kuiita "air charging system au supercharging"..

Mkuu, ukisema charging system na hata ukiingia google utaletewa mfumo wa umeme. unachozungumza wewe hakiitwi charging system, ni Forced Induction, ndio tunazungumzia kuhusu turbo na superchargers. Isitoshe, mada ilikuwa kuhusu Noah, sifikiri kama Noah iko turbo charged (labda ukaipeleke kwa turner).

Also, ni Petrol system, tumfahamishe mleta mada kwa mujibu wa gari, mfumo wa diesel na petrol sio sawa katika baadhi ya mambo.

Halafu jambo jengine muhimu, kwanza ijulikane tofauti ya miss na calibration ikifanyika (kuweka vipimo sawa). Wakati wa asubuhui engine ikiwa baridi, inafanya calibration sio miss. Inafanya hio process ili gari ipate moto haraka na kuanza ku operate normal as required. Kumiss manake kuna cylinder 1 au zaidi hazina mripuko

Miss ni kuwepo kwa cylinder moja au zaidi kukosa mripuko na kusababisha mzigo wa cylinder husika kwenda kwa nyegine na hio nyengine kuzidiwa ndio mana unaona inatikisika na kuwa perform very poor au kuzima kabisa.

Kwaio mfano wako a diesel, hio sio miss, hapo ni ECU inafanya kazi yake.

Mtoa mada pamoja na kusema kuwa asubuhi linamfanyia ivo, kilichonipa concern ni pale aliposema kuwa baadhi ya time anapata taa ya check engine.
 
LEGE,
Zile habari zenu za mafundi kuchukua toilet paper iliyoloa maji na kuingiza kwny exhaust na mnaangalia masizi sijui yamefanya nini ndo mjue kitu gani kinaendelea huko ndo nije niwaamini?Fundi anayetengeneza gari yangu ni mwenye diagnosia machines na mwenye kujua anachokifanya,period.Na tangu nimeanza kutumia mfumo huu sijawahi kufeli...
Point yako ya mwisho sikubaliani nayo. Nunua mashine ya kufanya diagnosis, halafu ikiwaka check engine, ichomeke na usome uone tatizo nini (haihitaji uwe fundi kufanya diagnosis). ukishajua, mpelekee fundi wa kitaa tu wa kawaida, halafu mwambie akutengezee jambo flani (kwa mujibu wa kodi uliopata). Atakutengenezea tu na itakuwa fresh.

Shida iliokuwepo ni kwamba, mafundi hawana diagnosis tool ndio maana unakuta wana bahatisha bahatisha. Ila kama unayo, huihitaji kuwa fundi kujua tatizo lipo wap kwenye gari.

Hakuna gari ilioko Analogy siku izi, even before 1997 magari yalikuwa na OBD1 port kwa ajili ya diagnosis. Mafundi wanatumia uzoefu kwa vile hawa diagnosis tool. Wakiwa nazo, huyo ulomuona sio fundi wa Bimmer basi utamwita wa fundi wa bimmer.
 
Mleta mada pole sana..
Huku Jf utapata ushauri mseto mpaka kichwa kitauma. Kuna jamaa huko juu kasema sijui itakuwa oil. Mwingine kasema charging system...

Matatizo ya gari kuleta miss husababishwa na mambo kadhaa. Tukianza na yale marahisi kwenda magumu..

1.Spark plugs...huenda moja wapo imekufa.

2. Vacuum hoses...Kuna vipipe vidogo vidogo vinavyohusiana na hewa, kakiwa kametoboka au kamechomoka unaweza kupata miss na check engine light. Mfano kuna vacuum hose moja huwa inatoka pale kwenye cylinder head cover inaingia kwenye hose kubwa kati ya throttle body na MAF sensor...hii ikiwa na tobo au ikilegea kwa magari mengi utaona miss na check engine..

3. Ignition coil....Hapa huenda zile rubber boots za coil zinazoshuka kwenye spark plugs zimemetoboka...hizi hukakamaa kutokana na joto kubwa la engine na kutoboka au kupasuka....sehemu iliyotoboka itakuwa inavujisha umeme unaotakiwa uende kuchoma spark plug na umeme huo hupotelea kwenye block engine.....hapo utapata miss isiyoisha ila ukipiga resi rmp iwe kweny 4 mpaka 5 miss inapotea..

4. Fuel filter, air filter au throttle body huenda vimechafuka sana.

5..MAF au O2 sensors...huenda moja wapo ina loose connection au imechafua sana au ndiyo inaenda kufa kabisaaa.

6.Fuel injectors huenda zimekuwa clogged zinahitaji kusafishwa...

Kama maeneo yote hayo yamekaguliwa na hayana shida., fanya vipimo vya mashine....huenda control box imepata COVID 19.

Ukifuatilia haya, utapata suluhisho. Kwa fundi mjuvi, hako katatizo wala hatahitaji diagnosis machine..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom