No problem Sir, Yes Yes. No problem. Siasa itaharibu watoto wa maskini

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Nipo Dodoma kwa muda kidogo, Vichekesho ninavyokutana navyo huku vinasikitisha sana Katika mfumo wetu wa elimu

Kazi za sasa ni kujieleza vizuri kwenye Usahili na kujiamini lakini kwa kizazi hiki inasikitisha sana

Watoto wa maskini waliosoma shule za Kawaida utawaonea huruma huko Makazini na kwenye Usahili au Interview

Na sasa ukishaona mjadala utakuwa mrefu sana waajiri wengi wanaamua kutumia Kiingereza, Hapa ndio kimepelekea niandike uzi huu

Watoto wa maskini ambao wanasisitizwa kusoma kiswahili utawaonea huruma, akiulizwa kitu kuhusu haki zake au malalamiko yake kwa Kiingereza hata kama anayo lakini kwa kushindwa kumudu lugha utasikia Yes sir, Yes Sir No problem, No problem

No problem sio kwamba hana matatizo yanayomsibu bali kufupisha mambo na kushindwa kujieleza anaamua kusema No problem, No problem sir

Mimi ni mwana siasa lakini kwenye lugha ya watoto wetu tuchague lugha moja
 
Vipi wewe unaimudu hiyo lugha?. Kujua lugha ya kingereza na kujieleza ni vitu viwili tofauti. Kujieleza ni kujiamini(confidence) kwa mtu.
 
Lugha sio kwa watoto wa maskini tu hata hao maprofessor na wengineo lugha kwao ni shida
 
Kwahiyo hua manafurahi na mioyo yenu jinsi mnavyowafanya mazuzu wadanganyika..eti elimu bure..absurd.

Wakati huo watoto wenu wapo wanasoma mitaala ya cambridge.

#MaendeleoHayanaChama
 
Watafutwe walimu wa kizungu waje wafundishe hiyo lugha maana kila mtu nowadays ni kuzungu kizungu.
 
lipo tangazo la Haki Elimu #KINAPANDA aiseee ile ni reflection ya unaloliongelea hapa.
 
Back
Top Bottom