No comment - Kingunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

No comment - Kingunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JoJiPoJi, Aug 27, 2009.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Na Leon Bahati na Mkinga Mkinga
  Mwananchi


  KINGUNGE Ngombale Mwiru amekuwa mwepesi kuzungumzia waraka wa Kanisa Katoliki kuhusu jinsi ya kuchagua viongozi katika uchaguzi ujao kila mara alipotakiwa kufanya hivyo, na wakati mwingine aliita waandishi wa habari ili atoe msimamo wake, lakini jana alimudu kusema maneno mawili tu; "no comment".

  Mbali na Kingunge, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ambaye Halmashauri Kuu ya chama chake ilipendekeza kuwa viongozi wa dini wakutane na viongozi wa kisiasa kabla ya kutoa nyaraka zake, alitoa kauli kama ya Kingunge, hali kadhalika Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo.

  Mwananchi ilikuwa imetaka maoni yao kuhusu tamko la Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kuwa kanisa halitapokea maagizo wala maelekezo wakati wa kuandika nyaraka zake.

  Waraka huo ambao umesambazwa na kuuzwa nchi nzima, unaelekeza waumini wa kanisa hilo kuchagua viongozi waadilifu, wapenda amani na wenye kujali zaidi maslahi ya wananchi.

  Lakini baadhi ya watu, wakiongozwa na Kingunge wamekuwa
  wakiupinga kwa madai kuwa unaweza kuwa hatari kwa amani.

  Akiongoza ibada ya mazishi ya Askofu Anthony Mayalla juzi, Kardinali Pengo alieleza bayana kuwa si jukumu la viongozi wa kidini kupokea maagizo na maelekezo ya na wanasiasa wakati wa kutekeleza majukumu yake kwa sababu kufanya hivyo ni kukiuka misingi na maelekezo ya kanisa.

  Kardinali Pengo alikwenda mbali zaidi alipotoa maneno yaliyoonekana kumlenga moja kwa moja Kingunge aliposema "wakomunisti siku zote wako mbali na Mungu, afadhali hata ya mapebari wanaamini kuwa Mungu yupo".

  Kingunge anajulikana kama mmoja wa waumini wakubwa wa siasa za Kikomunisti na hula kiapo kwa kunyoosha mkono juu tofauti na wanasiasa wengine ambao hushika vitabu vitakatifu vya dini zao wakati wanapoapa.

  Mwananchi ilipowasiliana na Kingunge jana kupata maoni yake kuhusu msimamo wa Pengo, alikiri kuwa hana hoja tena katika suala hilo.

  "No comment (sina la kusema)," alijibu Kingunge na kukata simu. Kingune amekuwa akisisitiza kuwa waraka huo wa Kanisa Katoliki haufai na kulitaka kanisa liufute.

  Na hata kanisa lilipomtaka aeleze ubaya wa waraka huo, aliendelea kusema haufai na kusababisha alaumiwe na viongozi wengi wa dini pamoja na wadau wengine wa masuala ya dini na demokrasia.

  Kauli kama ya Kingunge ilitolewa na katibu mkuu wa CCM, Makamba."Sina lolote la kusema katika hilo. Wewe niulize ya CCM.

  Kuna kura za maoni za kuwachagua wagombea wa serikali za mitaa," alisema Makamba, ambaye chama chake kiliratibu mkutano na waandishi wa habari ambao Kingunge aliutumia kusisitiza msimamo wake dhidi ya waraka wa Katoliki.

  Baadaye Makamba alipozungumza tena na gazeti dada la Mwananchi The Citezen alisema: ÒNdugu yangu kila mtu amemsikia baba askofu, sasa unataka mimi niseme nini? Mimi sibishani naye hata kidogo na siwezi kusema abadilishe msimamo.

  ''Kimsingi, Mwadhama Pengo ni kiongozi mkubwa sana katika Kanisa Katoliki, siwezi kubishana naye hata kidogo.''

  Hoja za kupinga na hata kuunga mkono waraka wa Kanisa Katoliki, zilianzia Bungeni Julai Mwaka huu.

  Mjadala huo pia ulijadiliwa kwa hisia tofauti na wanasiasa, wasomi, viongozi wa dini na hata wananchi wa kawaida.

  Mzee Kingunge, ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na kada anayeheshimika sana ndani ya CCM baada ya kufanya kazi kwa karibu na marais wa awamu zote nne, alionekana kutoa hoja nzito zaidi na hasa alipobeba msimamo wa chama hicho kutaka waraka huo uondolewe.

  Kama hiyo haitoshi, CCM kupitia Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec), hivi karibuni, ilitoa azimio la kuwataka viongozi wa dini kukaa na viongozi wa dini ili kushauriana katika suala zima la utoaji wa waraka, ikiwa ni njia ya kuepuka kuvunja mshikamano wa kitaifa.

  Lakini juzi, Kardinali Pengo alisema Kanisa Katoliki litaendelea kutoa nyaraka zake bila kuomba baraka kwa serikali na hata chama kwa sababu huo ni wajibu waokatika kufanya kazi ya Mungu.

  "Waacheni maaskofu wafanye kazi zao na wasifundishwe kazi kwa maana kuandika waraka ni mamlaka kutoka kwa Mungu na si kwa uwezo wao.

  Vyama visilazimishe kwamba ni lazima vitoe ushauri," alisema Pengo katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete, mawaziri, wabunge na marais wastaafu.

  Kardinalo Pengo pia alikemea wale ambao wanaonekana kuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi wakati hata ingekuwa wao ndio walio katika nafasi hizo, wangefanya vitendo hivyo vya wizi wa lami za umma.

  Kuhusu kauli hiyo ya Kardinali Pengo dhidi ya vinara wa vita dhidi ya ufisadi, mmoja wa wabunge walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ufisadi, Aloyce Kimaro (Vunjo-CCM) alisema binafsi hana uhakika juu ya suala hilo lakini anajifahamu kuwa moyo wake ni safi.

  Lakini alimwelezea Kardinali Pengo kama mmoja wa watu mahiri na wanaohitajika sana katika kuendeleza vita itakayowezesha kuwaangamiza mafisadi ili mali za Watanzania zibaki salama.
   
 2. O

  Omumura JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa kawaida maumivu ya kuambiwa ukweli huanza kuuma taratibu, mwishoni huwa makali kama nyigu, haya ngoja kimaro na wenzake wajiseme taratiiiibu!habari ndo hiyo, bravo Cardinal pengo.
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Pengo kawatolea uvivu .
  Hapa anaposema watu wanaopiga kelele kuhusu rushwa kama wangekuwa na nia ya kweli ufisadi ungeisha,hapa hamaanishi wapiganaji kama Zitto,Slaa, Seleli nk.

  Hapa ana maanisha ma RAIS hadi eti kufika kuunda chombo cha kupinga ufisadi TAKUKURU.
  Its very clear RAIS akitaka ufisadi ukome una koma ndani ya week moja.Lakini Zitto hata akipiga kelele la kufa mtu na ana nia na dhati ya kweli Ufisadi hauwezi kuisha.
   
 4. w

  wasp JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bravo his Eminence Policarp Cardinal Pengo for your eloquent homily during the burial of the late Archbishop Anthony Mayalla. People like Hon. Aloyse Kimaro who have acquired large pieces of land amidst peasants without land and yet identifying themselves as corruption crusaders are not honest and sincere.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Better late than never. In the end he has learnt to say no comment.
   
 6. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Walijifanya wanajua sana kuongea .......yes, waongee tena kutetea misimamo yao, why ''No comment''?
   
 7. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Bora iwe "no comment" or else, impact ya waraka huo itakuwa kubwa unimaginable. Kardinali Pengo kiboko, anamtwanga JK hapo hapo live! Nakubaliana na MkamaP, hakuwa amawasema wapiganaji wa ufisadi bali alikuwa anampa JK live.
   
 8. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yaani, siku zote ukweli utasimama daima!. Pengo kwa vile kasimamia upande wa ukweli wenyewe wababaishaji wataumbuka na kwishilia mbali!. CCM wanajua for sure kwamba siku zote wanatumia ignorance ya wapiga kura kuwa hadaa na kuendeleza undava na wizi wao na tabia yao ya kulindana na kufichiana maovu huku wakiendelea kupokezana uongozi kama mchezo wa kupeana vijiti!

  Kwa waraka huu, ambao nina hakika unapenya hadi vigangoni pembezoni mwa nchi ukombozi wa mdanganyika u karibu!

  Ijumaa ilo pita nilikuwa karibu na msikiti ulioko Sinza makaburini, ni kabahatika kusikiliza mawaidha ya swala ya ijumaa, ndugu zangu kumekucha! Huyo mtoa mawaidha hakusita kugongomelea ukweli kwa kuwasifu wana kigoma waliomchagua Zitto, na maendeleo aliyo waletea. Na akawashangaa wana dar, watu wenye upeo mkubwa yet, wanakimbilia kofia na khanga na kuuza utashi wao!

  Kama kweli mambo yataendelea hivi, kazi ipo by 2010!
   
 9. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mzee Pengo nimemvulia kofia. Niliiangalia ile hotuba yake. Alikuwa anatoa hoja baada ya nyingine, tartiibu kama anampa mgonjwa dripu vile!
   
 10. M

  MathewMssw Member

  #10
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado! wakuu wote wa dini mnapaswa kuelimisha wapigakura wenu ili waking'oe chama cha mafisadi(ccm)
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Na bado watatia superglue hiyo midomo
   
 12. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Is acquiring land a problem? and this is noticed at times when that land is acquired by a tanzania. In that the same area where Kimaro has land, there are so many other foreigners in possession of bigger land than that of kimaro. If he followed procedures why not!

  Refer to mjombas words " tusiwatukure wazungu na kuwakataa waafrika wenzetu"

  Acha chuki binafsi au nawe ndio wale waleeee!
   
 13. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #13
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  KWELI PENGO WEWE NI MTUMISHI WA MUNGU...nakuaminia hasa..sio mnafki..umewapasha wazi wazi.
   
  Last edited by a moderator: Aug 28, 2009
 14. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Your last statement abuot JK is irrelevant in this forum considering that he is the head of state and he deserve respect. This does tarnish the image of this post. Behave yourself
   
 15. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Kakwangu ni kajiswali tu,hivi ukomnist ni dini? nauliza hivi nikimaanisha kwamba hivi mtu ukifuata na kukubaliana na falsafa za kina Hegel,Trotsky,Karl Max,Mao Tse Tung, Fidel Castro na wengineo,inakufanya au kukulazimisha uachane na dini yako? Wadau tusaidiane hapa,nini msingi mkuu wa ukomunisti?
   
 16. S

  Sendeu Member

  #16
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera Baba Pengo ujumbe ulifika safi kabisa wenye mamlaka waliokuwepo pale ni wanafiki wakubwa km JK nk bora Pengo ulivunja ukimya
   
 17. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Wadau mimi nina kajiswali kengine,hivi baba Askofu Cardinal Pengo anaposema wanaopinga ufisadi na wao wajiangalie kwanza kama ni wasafi,sasa je ina maana Padre mzinzi (na wapo kibao) si ruksa kukemea uzinzi pamoja na kwamba ni wajibu wake kama 'mchungaji wa kondoo' kufanya hivyo? au Padre mkwapuaji wa sadaka (wapo pia kibao,hasa hela za mavuno) asikemee wizi kwa kuwa na yeye mdokoaji? na kwa maana hiyo Mapadre wa namna hiyo pia si ruksa kumfanyia mtu kitubio muumini mwenye dhambi ya uasherati/wizi?
   
 18. l

  lucymtoi Member

  #18
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wembe huohuo baba, tupo nyuma yako
   
 19. C

  Calipso JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  PENGO VS SIMBA? au PENGO VS JK? au PENGO VS CCM?. ingekuwa shekhe kasema maneno yale tena sehemu kama ile hivi sasa tusingemuona tena. letu jicho...
   
 20. S

  Superstar Member

  #20
  Aug 28, 2009
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rwabugiri - kwa kweli umenigusa - 2010 moto utawaka naomba wanajamii tuendeleze moto huu - tuchochee mpaka basi. Hongera sana Cardinal Pengo - Endea kusimamia haki ya wanyonge. Tuko nyuma yako Baba, kwa kila hali - kwa maombi, mawazo nkm. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni !!!!!
   
Loading...