No-box Thinking: Hivi ni kweli machafuko yanayoendelea Burundi ni Nkurunziza pekee wa kulaumiwa?

Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,604
4,259
Tarehe 25 Aprili 2015, chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD kilitangaza kuwa rais aliyekuwa madarakani wakati huo (na sasa pia) atagombea tena muhula wa tatu kukiwakilisha chama chake katika uchaguzi uliotarajiwa kufanyika miezi michache baadaye. Uamuzi huo ulipingwa vikali na makundi mbalimbali ya watu nchini humo kwa vile ulikwenda kinyume na katiba ya Burundi iliyoweka ukomo wa mihula miwili tu kwa Rais. Rais Nkurunziza pamoja na chama chake walitetea uamuzi wao kwa kudai kwamba hiyo itakuwa ndiyo awamu ya pili kwake kuchaguliwa "na wananchi" kwani muhula wake wa kwanza alichaguliwa na Bunge.

Baada ya hapo, nchi ya Burundi haijatulia tena. Mamia ya watu wamekufa katika vurugu za maandamano pamoja na mauaji ya kupangwa. Jaribio la mapinduzi lilifanyika dhidi ya Nkurunziza tarehe 13 Mei 2015 lakini lilizimwa. Maelfu wameikimbia nchi ya Burundi na hadi sasa hali si shwari nchini humo.

Wananchi, wapinzani, nchi jirani, jumuiya za kimataifa na vyombo vya habari vimekuwa vikimshutumu Rais Nkurunziza kwa kusababisha vurugu zilizopelekea mauaji ya watu wengi na wengi kuikimbia nchi yao. Binafsi nakubali kwamba kwa uamuzi wake tu huo anastahili kubeba lawama kwa kiasi kinachomtosha maana alikuwa nayo nafasi ya kunusuru hali hiyo hata kama alifikiri ana haki "kikatiba" ya kugombea tena. Ninachojiuliza (nje ya box) ni je, ni kweli yeye peke yake anastahili kulaumiwa au amekuwa njiti isiyozimika vizuri iliyotupwa kwenye majani makavu yaliyokuwa tayari kulipuka muda wowote?

Tujiulize:
i. Uamuzi wake wa kugombea tena ulitangazwa kwanza ndani ya chama chake. Tunategemea upinzani wa kwanza dhidi ya uamuzi huu ulikuwa ndani ya chama alichokuwa anakiongoza. Sina hakika kama wapo waliopinga au la, ila kinachofahamika ni kwamba mwisho wa siku chama kilimpitisha agombee. Kwa nini chama chake kilimpitisha kinyume na katiba ya nchi?

ii. Kama chama chake kimempitisha basi upinzani mkubwa ulitegemewa kutokea kwenye vyama vya upinzani. Na hivyo ndivyo ilivyotokea kwani vyama vingi vilipinga uamuzi huo na wafuasi wao wakaingia barabarani, jambo lililoanzisha rasmi vurugu zinazoendelea hadi leo hii. Je, vyama vya upinzani vilikuwa na haki ya kuingia barabarani kupinga uamuzi huo? Ingekuwaje kama badala ya kususia uchaguzi vingeamua kuingia kwenye kampeni kupambana na Nkurunziza kwenye sanduku la kura? Kwa kuwa wananchi wengi walikuwa hawajafurahishwa na uamuzi wake wa kujiongezea muda kinyume cha katiba, isingekuwa rahisi kwa vyama vya upinzani kujenga hoja na pengine kumshinda, hasa endapo vingeunganisha nguvu?

iii. Upo uwezekano Rais ambaye tayari alikuwa ameonyesha kutumia nguvu kujiongezea muda angehakikisha anashinda kwa namna yoyote hata kwa kutumia nguvu ya tume ya uchaguzi na dola, hivyo kuondoa uwezekano wa point (ii) hapo juu. Lakini tukikubaliana na hili, bado ingewezekana pia hali kuwa hivi hivi hata kama Nkurunziza angekuwa pembeni maana bado serikali ya chama cha CNDD-FDD ingekuwa madarakani hivyo kufanya nafasi ya vyama vingine kushinda kuwa finyu.

Kwa kuzingatia hizo points, pamoja na kuwa Nkurunziza amekiuka wazi wazi katiba ya nchi yake japo uamuzi huo ulihalalishwa kimizengwe na mahakama ya katiba ya nchi hiyo, naamini kuna ushawishi wa pembeni uliohusika. Yawezekana ni miongoni mwa nchi zilizo jirani na Burundi zilizokuwa zikitafuta namna ya kuiyumbisha Burundi. Pia inawezekana ndani ya Burundi kuna vikundi vilivyokuwa havina matumaini ya kushinda uchaguzi, kwa sababu za kawaida za kisiasa au kwa kuhofia nguvu ya chama tawala na vyombo vyake wakati wa uchaguzi, kwa hiyo vikundi hivyo vilikuwa vintafuta tu sababu ya kuwasha moto ndani ya nchi hiyo kuifanya isitawalike.

Kwa bahati mbaya, Nkurunziza amewapatia sababu hiyo nao wameitumia na sasa Burundi inawaka moto maeneo mbalimbali na kufuka moshi maeneo mengine.
 
kwani we unafikiri angepumzika tu awaachie wengine wenye fikra zingine za kiuongozi watawale angekosa nini kwa mfano. Unadhani kwa miaka 10 aliyoongoza Burundi,hii miaka mingine 5 atakuwa na jipya,alitakiwa ajiongeze tu akae kando,hakuna wa kuubeba mzigo huu wa lawama zaidi yake,hakuna wa kumuangushia jumba bovu,ni yeye tu ndiye anayeiweka hatma ya amani ya Burundi mashakani
 
Haya mawazo yako eti "wapinzani si wangeingia kwenye kampeni na kupambana kwenye sanduku la kura"

Mkuu wewe unaosa hii ni sawa kabisa? Kweli wewe unamawazo ya ki-CCM.

Mtu amekanyaka katiba waziwazi halafu uingie kushindana naye kwenye uchaguzi huoni hata mtoto mdogo tu anaweza kung'amua kitakachotokea?

Nkuruzinza hata kama angeshindwa asingekubali kwasababu lengo la kuongeza awamu ya tatu ni kuendelea kuwatawala wananchi wa Burundi.
 
Back
Top Bottom