Nnauye:Mafisadi wasahau kusimamisha maamuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nnauye:Mafisadi wasahau kusimamisha maamuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wednesday, 13 April 2011 20:53

  Midraji Ibrahim na Joyce Mmasi, Dodoma

  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, amesema watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho, wanapaswa kusahau uwezekano wa wao kujipanga na kusimamisha hatua zilizoanza kuchukuliwa.Nnauye alisema chama kitashinda vita ya ufisadi na kwamba, kama kuna watu wanajifanganya kuwa wanaweza kufifisha moto uliowashwa, wajaribu.

  Akizungumza mjini Dodoma jana, Nnauye alisema kilichofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM, ni mwanzo wa mapambano ya kufagia mafisadi ndani ya chama hicho kinachotawala."Chama kitashinda vita hivyo, kama kuna watu wanafikiri wanaweza kujaribu, Tumeanza tutamaliza,"alisema.

  Kuhusu madai kwamba tamko kuhusu watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi kupewa siku 90 kujiuzulu Nec alilotoa na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, John Chiligati, lilikuwa lao na kwamba si la Nec, alisema maamuzi yote ya kikao yapo kwenye maandishi."Maamuzi yako kimaandishi si yangu, yanasema wajiuzulu wenyewe wasipofanya hivyo chama kitawawajibisha chenyewe," alisisitiza Nnauye.

  Akitoa tamko hilo juzi usiku baada ya kumalizika kwa kikao cha Nec, Chiligati alisema "wenyewe wapime na kuchukua hatua za kuwajibika ndani ya chama kama tulivyokubalina hapa ndani, wasipofanya hivyo katika kipindi cha miezi mitatu, chama hakitasita kufanya hivyo kwa niaba yao."

  "Hata kama hatuna ushahidi, hisia tu kutoka kwa wananchi zitoshe kuwafanya wajipime wao wenyewe, na kama kuna hoja ya kuonewa kwa nini usemwe wewe tu." alisema.

  Nnauye aliwataka wanachama waliokimbia kwa hasira, kurejea CCM kwa sababu walichotaka kimefanyika na kwamba, tayari ana maombi mengi ya wanafunzi na wanachama kutaka kurejea.Kuhusu muda wa kufanya marekebisho kwenye chama ngazi zote, Nnauye alisema mpango wa kazi upo na utatekelezwa kwa hatua."Hata unapoanza kuoga huanzi mwili mzima, unakwenda hatua kwa hatua. Mpango kazi upo utatekelezwa," alisema.

  Alisema kufuatia uamuzi wa Nec, baadhi ya wanachama wameomba kukutana na sekretarieti na kwamba, itaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara, Pius Msekwa.Nnauye alisema ziara ya kukutana na wanachama hao ilianza jana mjini Dodoma na leo, itaendelea mkaoni Morogoro.

  Kwa mujibu wa Katibu huyo, Aprili 16, mwaka huu, sekretarieti itakutana na wanachama wa Chalinze, Kibaha na Dar es Salaam na kabla ya kwenda Zanzibar, Aprili 17 mwaka huu.
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,700
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  hatutaki maneno tunataka vtendo,namuomba Mola niweze kufika ktk hìzo cku 90 na kujionea yatakayojiri
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Nnauye & Co. kama wana ubavu wawataje hao mafisadi kwa majina yao. Au hao mafisadi hawana majina?
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Wao wanafikiri 90 ni nyingi sana tutasahua leo tu zimebaki 85 countdown.
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Enzi zile walikuwa wanasema CCM haina msamiati wa neno Fisadi tena wakasema kama kuna mtu anamjua fisadi ampeleke mahakamani mbona leo wanaanza kuwahukumu watu kwa hisia tu bila kuwapeleka mahakamani?
   
 6. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,700
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  We waache 2nao hao mpaka kieleweke,wameiba sana bana!
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mnajua hawa CCM wanachekesha sana.. Hivi Ufisadi tunaozungumzia upo ndani ya chama au upo serikalini?..
  Wananchi wanalalamika na matendo maovu ya viongozi wa chama hiki waliopewa wadhifa ndani ya serikali na chama hakikuchukua hatua zozote isipokuwa leo tunasikia kuna Mafisadi ndani ya chama, hivyo kunifanya nikubali kwamba Uongozi wa CCM unajali zaidi maslahi ya chama kuliko ya Taifa..

  Ikiwa hofu ya chama ni kupoteza ushindi mwaka 2015 ndio maana wamefanya mabadiliko haya, nashindwa kabisa kuelewa kama hawafahamu kwamba chama kitashindwa kwa sababu ya Ufisadi na utekelezaji mbaya wa serikali iliyopo madarakani..

  Binafsi sioni kilichopungua zaidi ya chama kujisafisha tayari kwa uchaguzi ujao ili kulinda maslahi ya hao hao mafisadi..It's all good and beneficila to Mafisadi kuondolewa ktk wadhifa wa chama..Rostam hahitaji kuwa NEC wala CC maadam kesha wekeza fedha zake sehemu muhimu za Kuifisadi serikali, kisha basi hajawahi kukifisadi chama isipokuwa kukiwezesha zaidi..
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hey hey hey......Nape..........THIS IS VERY GOOD from you.....keep it up!
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mazee "Ngosha" naona umerudi na full muziki............
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Apr 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kama kawa mwanawane....nambie? Kwema huko kwako?
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  maan, dis boy gonna give dem Lowassa and ting....hell...trust me!.......remember UVCCM project
   
 12. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hamna mengi sana yakusema...Cha msingi wapeni muda wawasafishe.. Ukweli ni kwamba this can only be positive for Tanzania... EL will never be President na mtu yeyote aliyekatika nafasi yakufanya grand corruption atajicheki mara mbili.. Ndio wizi hautoisha lakini zile za kivijisenti type tena itakuwa ngumu.. Mambo ya mabilioni London etc...itabana kidogo, watabakia na 10% za hapa na pale.. walioba washaiba na watakaoiba saivi watakuwa wanadonoa tuu.. Wamefanya kazi nzuri tuu cha msingi upinzani uendelee kuwabania white-ball. This is about filling in the loopholes and here some holes have been filled...Not the great majority, no but a significant amount. Kama jahazi linaelekea kusini na linatumia injini zakisasa...basi upepo nao ukisaidia si mbaya.. Upinzani uendelee na kazi ya kuwabana hawa watu...adi kieleweke.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,552
  Trophy Points: 280
  Ngoja miye niwasaidie...Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Mramba, Mkono, Chenge, Rostam, Makamba, Karamagi, Kigoda na wengineo wengi ndani ya chama chao. Hawana ubavu wa kukisafisha chama chao. Watafanya usanii wa kuwaondoa madarakani wachache na kisha kuwaambia Watanzania look at us! we're a new party! lakini wanachokisahau ni kwamba Watanzania wa 2011 sio wale wa mwaka 47 waukubali upuuzi wao kirahisi namna hiyo.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi ingekuwaje Mwalimu angempa Jumbe muda wa siku 90 kuamua mwenyewe kama amesababisha kuchafuka kwa hali ya hewa?
  Majibu ya Nape kutoka kwa Rostum yako kwenye gazeti la Mtanzania la jumatano hii. April 13. Litafuteni mkalisome.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,552
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi yule mtu mwache aende zake. Alikuwa kiongozi shujaa asiyeogopa mtu kwa sababu alikuwa anajijua kwamba ni msafi hivyo hakukuwa na ugumu wowote kwake kumfukuza mtu toka TANU/CCM au kumstaafisha kazi kwa manufaa ya umma. Kikwete hana ubavu huo ndiyo maana anajibaraguzabaraguza kuwapa miezi mitatu na jamaa wakitaka kulala naye mbele wanaweza kumtisha kwamba watayaanika hadharani madudu yake hapo ndipo tutaona jinsi asivyo na ubavu kama kiongozi wa kufanya maamuzi mazito.
   
 16. S

  Selemani JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  The political weather during Mwalimu's time was just perfect. Uhuru, Mzalendo, RTD, na jumapili's Burudani. Jumbe had no chance. You wouldn't expect the same decisions to be emulated today. Lets get over Mwalimu's era folks.

  Nape is doing his work, serikali should also do her work equivalently, na sisi wabongo wa kawaida should also do our part. Collectively our small ufisadi (rushwa ya kila siku mtaani) add a bigger dent to our economy than Mzee Vijisenti.
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Selemani,
  Mwalimu's era may be over. But leadership qualities continue. That is what one expects from the chairman of a ruling party. Decisiveness and what we say in Swahili, kuchukua maamuzi magumu, hata kama yatagusa rafiki zako. Sio hii ya kuwapa siku 90 eti wajitazame nafsi zao na wachukue maamuzi wao wenyewe. Sasa Waswahili wakisema huu ni usanii mtajitetea vipi?
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Apr 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Kikwete yeye sasa si fisadi? Ni kwamba zile tuhuma ambazo naye alikuwa akituhumiwa nazo hadi kufikia watu kumwanzishia mada kuwa na yeye ni fisadi zilikuwa za uongo?

  Au tuhuma zimefutika baada ya yeye kujivua magamba or whoever aliyejivua magamba (whatever the hell that means)? Watanzania tunashangaza. Na Mkapa je? Au na yeye si fisadi?

  Tegemeeni haya ma CCM kutawala kwa muda mrefu sana.
   
 19. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Cry my beloved country, yaani as if kama hatuifahamu Tanzania, je toka 2005 ni mara ngapi baraza la mawaziri limevunjwa? What has been improved so far kutokanma na mabadiliko hayo? Hamkuambiwa juzi juzi tu hapa kwamba tatizo la ufisadi limeshughulikiwa eti kesi zipo mahakamani (Au tumesahau zile tungo kama JK afanya kweli, haijapata kutokea, Sasa serikalini hakushikiki etc.........sasa hao mafisadi wapya wametoka wapi?

  Tutazunguka mbuyu weeeeeeee lakini kama hatutatatua tatizo kuu ambalo ni JK hakuna kitakachobadilika. Yetu macho.
   
 20. S

  Selemani JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  You are not being pragmatic. It is also leadership to oust them from CC. And it is also an act of leadership to give them 90 days. You just do not make decisions for the sake of bending towards a populist wind. Mrema was also popular. Ndio maana kikao cha Bagamoyo hakikumfukuza Zitto. Nape will go to work regardless if you Chadema folks are pleased or not. Ya'all would never be pleased, regardless of you inadequate to lead.ie Freeman Mbowe.
   
Loading...