Nmb yawakomboa vijana kiuchumi

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
"NMB YAWAKOMBOA VIJANA KIUCHUMI KWA KUWAPA MIKOPO NAFUU YA PIKIPIKI Ni mikopo kwa ajili ya pikipiki za miguu miwili na mitatu"


Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina ya Bajaji, kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors inayosambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu.
Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa mbali mbali za kibenki zinazogusa kwa karibu mahitaji ya wateja na watanzania kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza,Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu,Mhe.Dkt.Mary Naguamesema “Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku.
"Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu kiuchumi”, alisema.
Vilevile kutoka NMB, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki, Bw.Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya ina lenga kupunguza changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.
“NMB itaendelea kubuni bidhaa ili kupambana na changamoto za ajira zinazowakumba wateja. tutaendelea kushirikiana na makampuni kamaFair Deal Auto Private Ltd, Car & General Limited Ltd pamoja na Quality Motors ili kupata bidhaa zenye ubora zaidi.” alisema Mponzi.
Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani yamuda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa kuzingatia taratibu za makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB.
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima hii ni kwa ajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha.
Mikopo hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia asilimia thelathini ( 30%) ya bei ya pikipiki ya miguu miwili au mitatu kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi za Fair Deal Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality Motors.


*Kwa maelezo zaidi temembelea matawi ya NMB.


Source: MIM
 
Back
Top Bottom