NMB wananitumia SMS za kuweka pesa hali ya kuwa sijaweka

DOTHRAK

Member
May 22, 2021
15
154
Habari wakuu?

Nina kama miezi miwili sasa tangu nisajili laini yangu ya Tigo. Kuna jumbe zinaingia katika simu zangu kutoka NMB ya kwamba nimefanikisha kuweka pesa hali ya kuwa sijafanya kitu kama hicho na wala laini hiyo sijaiunga na huduma yoyote ya kibenki zaidi na zaidi ina Tigo pesa tu.

Shida itakuwa wapi hapa?
 
Hizi laini za simu ni shida sana. Mi nimenunua line ya Airtel basi najuta maana napigiwa sana na jamaa zetu wa kanda ya ziwa WASUKUMA, WAJITA, WAKEREWE wakiniambia kuwa wananifahamu
Worse enough wanapiga muda mbaya usiku sana na kuniambia maneno ya karaha mara nakupenda mara wee ni mzuri wakati bibi wa watu mimi umri umeenda wanadai eti wameona picha kwenye profile....n.k...n.k.
Kwa ujumla ni kero sana sasa sijui wenye mitandao wanatusaidiaje.
Ni vile nimesajili NMB mobile kutumia namba hiyo otherwise ningeitupilia mbali!!!!!
 
Mimi mwezi sasa nimetengeneza line ya Hallotel,Napigiwa sana na Wasukuma wanaongea kilugha tu hata sijui wanataka nini..
Hahaha shida sana nilinunua line ya Airtel , ilikuwa ya mdada mmoja kutoka kigoma nikawa naongea na watu huko daily mpaka nikatamani niache ile laini baada ya muda waliacha kupiga .
 
Nimeshangaa sana NMB kusema kuna kadi yangu branch nikaichukue wakati sijawai kuomba Kadi nyingine ya pili ,hii nimeigundua baada ya kuwataarifu kwamba Kadi yangu ya NMB MasterCard haifanyi kazi Kila nikijaribu naambiwa invalid account selected!! Nikawapigia Kwa Whatsap kuwaelewesha wanaangalia kwamba kuna Kadi iko branch na Suala hili limesnishangaza sana sijawai omba kadi nyingine hili Suala sijui tatizo ni nini
 
kuna watu wanasajili line then ndani ya muda mfupi hawaitumii ile line,sasa ii mitandao naisi ina utaratibu wa kutoa tena zile line ambazo wanaona hazijatumika muda mrefu
 
Hizi laini za simu ni shida sana. Mi nimenunua line ya Airtel basi najuta maana napigiwa sana na jamaa zetu wa kanda ya ziwa WASUKUMA, WAJITA, WAKEREWE wakiniambia kuwa wananifahamu
Worse enough wanapiga muda mbaya usiku sana na kuniambia maneno ya karaha mara nakupenda mara wee ni mzuri wakati bibi wa watu mimi umri umeenda wanadai eti wameona picha kwenye profile....n.k...n.k.
Kwa ujumla ni kero sana sasa sijui wenye mitandao wanatusaidiaje.
Ni vile nimesajili NMB mobile kutumia namba hiyo otherwise ningeitupilia mbali!!!!!
Waombe hela wataacha kukupigia
 
Line yangu nadhani walipeana watu walipokutana harusini au msibani wakakosea tarakimu au labda nilipewa zilizofufuliwa. .. maana nilibatizwa mama Rwegasira mwaka mzima nina kazi ya kujieleza.
 
Back
Top Bottom