Kesho nmb kushughulika bima za watu wakiibiwa huo ndoo mtiani wasumbufu sana sijui wana ajenda gani na bima
 
Samahani naomba kuuliza maswali haya NMB

1) baada ya kukopa ni mda gani MTU anaweza kufanya top up
2) branch moja na branch nyingine zinaweza kuwa na sera tofauti?
3) naweza kukopa tawi A alafu nikaenda kutop up tawi B? Lakini ndani benki moja ya NMB
4)riba ni kiasi gani? Na kwa muda gani?
5) ni vigezo gani nafuata ili kuwa NMB Wakala?
6) akaunti ninayo fungua kupitia kwenye simu naweza kupata ATM?
 
Mfumo wa kukokotoa hesabu za mkopo wa nmb kwa watumishi WA serikali ulipoteza kumbukumbu, vp wadau kuna aliewahi kuenda Leo akafanikiwa kuprocess mkopo, maana Hali Tete,msaada tafadhal
 
Karibu kufungua NMB Chap Chap Account, piga *150*66# na fungua akaunti sasa. Karibu Sana
NINA SWALI LA MUHIMU KWA NMB.

Kuna watumishi katika baadhi ya Wilaya waliondolewa kwenye PAYROL tangu 2016 na mishahara yao iilikuwa inapitia benki ya NMB.

Mimi pia nilipata tatizo hilo...nilikuwa nikienda kwenye A/C yangu nakuta kumeandikwa "Blocked by DED ....." hapo kwenye desh desh ni jina la Wilaya, kwamaana ya kwamba aliyeblock salary flow ni Mkurugenzi mtendaji ambaye ndiye Mwajiri.

Baada ya hapo ilikuja kufahamika kuwa tuliondolewa kimakosa tu na tunapaswa kurudishwa katika PAYROLL

■ SWALI JE kama nilichukua mkopo na miaka mitano ilipaswa kuisha katikati ya mwaka huu, ITAKUAJE?

mwenzangu niliyechukua naye mkopo siku 1 tayari ameshamaliza...mimi mishahara ilizuiwa ila nilishalipa nusu ya mkopo, ikaja kugundulika sikuwa na kosa la kuzuiwa mishahara.


JE BADO NINADAIWA? NASAIDIKAJE?


Msaada please.
 
Mkuu naomba unisaidie kujibu hilo la mkopo.

Je kama tayari nilishalipa mkopo kwa kutumia mishahara kwa miaka miwili na nusu na ikabaki miwili na nusu nikazuiwa mishahara halafu baadae kabisa wakagundua kuwa sikuwa na kosa la kuzuiwa mishahara...

JE DENI LANGU LITALIPWA LOTE AU?
Karibu kufungua NMB Chap Chap Account, piga *150*66# na fungua akaunti sasa. Karibu Sana
 
Mkuu naomba unisaidie kujibu hilo la mkopo.

Je kama tayari nilishalipa mkopo kwa kutumia mishahara kwa miaka miwili na nusu na ikabaki miwili na nusu nikazuiwa mishahara halafu baadae kabisa wakagundua kuwa sikuwa na kosa la kuzuiwa mishahara...

JE DENI LANGU LITALIPWA LOTE AU?
Hello Azare,

Karibu katika ktawi letu la karibu kuweza kuonana na Afisa mikopo na kukupa taarifa na taratibu sahihi za kutatua tatizo hilo

Karibu sana.
 
Wakati mtu anapokopa huwa mnakata sehemu ya fedha mnazoita ninyi bima ya mkopo. Je akimaliza kulipa deni lake hiyo bima anarudishiwa? Maana ni mali yake?
 
Wakuu NMB Tanzania
Hivi majuzi nilitoa pesa kwa ATM, na nilipotoa risiti ikanionyesha figure za 'salio" na 'kiasi kilichopo' zinatofautiana kwa kiasi cha 110k ('kiasi kilichopo' kikiwa pungufu kwa 110k dhidi ya 'salio' ambapo figure za kwenye salio ndizo figure sahihi kuwepo kwa acc. Nikachukulia poa, nilivyokwenda kutoa hela tena salio lilipungua kutoka kwenye kile kiwango ambacho siyo sahihi (kiwango pungufu).

Nikaenda kwa tawi jirani nikaeleza situation wakaniambia nijaze form ya ATM refund na nikaambiwa pesa itarejeshwa baada ya masaa 24, lakini yakapita masaa zaidi ya masaa 48 bila pesa kurudi.

Leo nimeenda bank kuulizia inakuwaje wakasema ishu hiyo inabidi ishughulikiwe na mtu aliyepeleka hiyo form ambaye leo hakiwepo na atarudi jumatatu.

Sasa napenda kujua yafuatayo:

Ni sababu zipi zinasababisha amount za kwenye 'salio' na 'kiasi kilichopo' kutofautiana kwenye risiti zinazotolewa na ATM.

Pili, japo shida yangu imeanza kushughulikiwa lakini naomba kujua itanichukua muda gani hadi kupata pesa yangu?

Nawasilisha.
 
Naomba kujuzwa kuhusu mikopo kwa watumishi wa umma. Nina mKopo NMB na CRDB . Kwa sasa mshahara unapita CRDB na na ninataka kutop up mkopo wa NMB.

Je ninalazimika tena kupitishia mshahara NMB iwapo ninayo Akaunti hai?
 
Nawapenda sana japo niliwahi kuitumia miaka mingi sana. Hivi naweza kuanza tena?
images
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.


Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:


Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.


4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Hivi huwa mnatoa huduma au msaada gani kwa wajasilia Mali haswa sisi vijana.
1. Kwawanao taka kuanza biashara
2. Kwawalio anza biashara
3. Na kwawalio bobea katika biashara(wazoefu)
 
77 Reactions
Reply
Back
Top Bottom