NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania

Verified Member
Joined
Sep 13, 2014
Messages
93
Points
150

NMB Tanzania

Verified Member
Joined Sep 13, 2014
93 150
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
12,312
Points
2,000

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
12,312 2,000
1. Nenda ATM yeyote ya NMB, chomeka kadi yako
2. Bofya chini, kulia
3. Chagua badili namba ya SIMU
4. Ingiza namba mpya ya SIMU unayotaka
5. Ingiza pasword uliyokuwa ukitumia awali ku-access huduma za bank kwenye simu, maliza.
Baada ya hapo utapokea ujumbe kwenye simu yako kuwa umefanikiwa kubadili namba ya NMB Mobile kutoka Mf. 0752XXXXXX kuwa 0683XXXXXX.

Gharama zipoje kwa kila mtandao hapo, maana haya ndiyo mambo hayasemwi mwisho wa siku tunajikuta tumeliwa halafu tunawaelekezea lawama Nmb
 

obas7x7

Senior Member
Joined
Sep 3, 2017
Messages
149
Points
225

obas7x7

Senior Member
Joined Sep 3, 2017
149 225
Habari..... Mimi ni mtumishi wa serikali pia ni mfanyabiashara. Naomba kujuzwa Endapo nitachukua mkopo(Tsh.5000,000) kwa kutumia nafasi ya utumishi wangu kwa muda wa marejesho miezi 60 ambayo interest yake itakuwa Tsh.2,455,772.73

Swali: Je? kupitia mihangaiko yangu ndani ya miezi 12 nikahitaji ku clear mkopo wangu nitalipa interest kiasi gani?
Je nitalipa ile ya miezi 12 yaani interest ya Tsh.472285.12
 

ISLETS

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Messages
8,096
Points
2,000

ISLETS

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2012
8,096 2,000
Wajuzi namba msaada hapa kwenye Klik App wa NMB inasumbua kidogo. Nikitaka kulog in nikiandika namba ya simu na PIN inaishia kuniletea hii notification badala ya kufunguka.
Mwanzo nilijua kwa vile nimebadili namba na kuweka Voda kwenye NMB mobile wakati Internet natumia ya Tigo, Lakini hata nilipojaribu kutumia internet ya Voda bado mambo ni yaleyale.
IMG_20191001_134941_730.jpeg
 

kamwamu

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
2,152
Points
2,000

kamwamu

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
2,152 2,000
IT walio program mashine za mawakala ni wanafunzi. Hazina mifumo kutoa taarifa mwamala unaposhindikana. Zinatunza kumbukumbu moja tu. Mtandao ukiwa chini waweza hudumia wateja na usipate jibu kumbe transaction imefanyika. Ukiangalia salio haikubali. Mtandao ukirudi salio limepungua. Kama ni umeme ndio humpati, labda awe jirani mstaarabu. Watafuteni IT waliokuwa MAXCOM, ni weledi.
 

Mkweli77

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Messages
1,272
Points
2,000

Mkweli77

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2013
1,272 2,000
Mkuu hiyo voda umeweka laini number ngap katika simu? Number 1 au mbili...
Wajuzi namba msaada hapa kwenye Klik App wa NMB inasumbua kidogo. Nikitaka kulog in nikiandika namba ya simu na PIN inaishia kuniletea hii notification badala ya kufunguka.
Mwanzo nilijua kwa vile nimebadili namba na kuweka Voda kwenye NMB mobile wakati Internet natumia ya Tigo, Lakini hata nilipojaribu kutumia internet ya Voda bado mambo ni yaleyale.View attachment 1220512
 
Joined
Sep 16, 2017
Messages
19
Points
45
Joined Sep 16, 2017
19 45
Nmb kwenye swala La Mikopo
Mafisa Mikopo wanatamaa sana
Nahitaji Mikopo WA MIL 8 kukuza biashara yangu ili niweze pata mkopo haraka lazima nimwachie MIL 1.5 kwenye kulipa deni nalipa mwenyewe Pamoja na alizo chukua wakati kuandaa mkopo Nmb Mafisa Mikopo wenu wanatumiza Sana sisi wafanyabiashara wekeni utaratibu mzuri
 

Forum statistics

Threads 1,343,415
Members 515,044
Posts 32,783,970
Top