Ndugu Mteja, tunaomba radhi kwa tatizo la mfumo wa MasterCard kwenye ATM zetu, tumia ATM nyingine yoyote yenye nembo ya MasterCard au NMB Mobile kupata huduma.

Tangazo wàlilonitumia
Watuma kote toka juzi ukitoa hela inagoma
 
Wakuu jambo iko?
Niende moja kwa moja kwenye kero maana limenifika hapa kwenye koo.

NMB ni zaidi ya wiki sasa ATM zenu hazikubali hizi card zenu mpya hivyo mnatulazimisha kuingia ndani.

Kuna muda naona huu ni mkakati wenu wa kutupiga hela maana ukitolea ndani gharama inakua kubwa tofauti na kutolea kwenye ATM.

NMB mnatuchosha sana hasa tunapokua na dharura za usiku tatizo gani halitatuliki?

Badilikeni na kama ni mkakati wa kutupiga tafuteni njia nyingine.
Hili tatizo lipo huku kibaha sijui maeneo mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbona tunabembelezana? kwani bank iko moja tuu? mimi nashauri wote tuhame kwenye bank zinazotumia umoja switch, kwa sababu hawa wamelala na wanafikiri kama hatuna options nyingine.

wawaulize NBC sasa hivi wanapumulia machine yaani chalii. kama wanashindwa declaring disaster kwenye huo mfumo na wanakaa kimya au labda hawajelewi? hiii ni (recovery time objective) what is tolerance time, kama wanachukua zaidi ya siku 5 basi wanatakiwa waadhibiwe na BOT na wapigwe penalt, halafu wa stop hii they said mastercard na waturudishie card za njano.

kama mbwai mbwai. Mimi wananidai kama m3, nikimaliza nahamia Maldiva, to-ko-li yao.
 
Nimesoma komenti nyingi na malalamiko lakini hakuna MTU WA NMB WA KUJIBU.
Kama wapo wajitokeze na kipekee nionavyo NMB haina huduma bora hasa baada ya kuleta master kadi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora nyie mnaotokea hapa jukwaani kwa ajili ya kukidhi kiu ya maswali na ushauri kwa wateja wenu

Maana wenzenu NBC wako hoi kitandani na hawana hata habari juu ya yale yanayoandikwa kwenye mitandao juu ya benki yao
Hongereni sana kitengo cha mawasiliano kwa umma NMB kwa mrejesho huu mnautupatia, Hakika nyinyi ni wadau wa kweli katika maendeleo ya taifa hili

Natamani taasisi zote zikaiga mfano huu
HEKO NMB HEKO TANZANI

Tatizo lao ni kupokea maoni kwa heshima sana na kufutika kwenye bongo zao. Nimesharipoti mara tatu kuhusu matatizo ya master card. Lakini ndo kwanza hawana habari.

Wanatuma sms tatizo limetatuliwa lakini muda huohuo ukienda benki hakuna utatuzi. Kwanini mnatulazimisha kutumia kadi hizi wakati zina usumbufu mkubwa? Kwa mfano, tangu mshahara utoke jumanne 22/ 8 hadi leo jumatatu 28/8 sijachukua mshahara wangu.

Kibaya zaidi leo wakati nikijaribu nikapewa risiti imeandikwa 'hakuna mawasiliano' lakini nikapata sms kwamba nimetoa fedha. Hali hii kwangu ni mara ya tatu kutokea.

Nilijaribu kushauri kwa kupiga simu makao makuu kuomba kadi ya kawaida, wakajibu tutalifanyia kazi.

Swali: kwanini kuendelea kulazimisha matumizi ya master card wakati inasumbua? Kuna faida gani kwa mteja kama siyo ni mchezo wa kuwaufaisha wao na kumtesa mteja?

Mimi ni mwanafunzi na ninajisomesha. Waliopitia chuo wanajua usipokuwa na mkopo inakuwaje. Inafikia wakati mtu u a hela yako halali lakini unalala njaa kisa mastercard. NMB mtajirekebisha lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mnaboa mnaboa fikiri kaunta zipo sita au Zaidi halafu kaunta Moja tuu Ndio ina mhudumu Huku foleni ina watu Kibao,yaani kuwaletea fedha Ninyi ni kujiadhibu.

Wekeni hata pipi au maji ya kunywa, mtu anasimama sukari inaisha mwilini anadondoka. Tegeta kibaoni, kibo complex

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NMB mnaboa sana huduma zenu sitakaa nifungue account kwenye benki yenu yaani huduma zenu mbovu lkn pia hata hizi MasterCard zenu ovyo yaani unakuta hela imo lkn ukienda kutoa mtandao mbovu!!!mnaboa sana kadi yenu nimeamua kuitelekeza kabisa na hata wife ataendelea kuwa kwenu kwa vile tu yuko serikalini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepewa cheque na GEPF ambapo inatakiwa nilipwe hela yangu nikaenda NMB Kenyatta road Mwanza nikaambiwa lazima niwe na account ili malipo yafanyike kwa kuwa Nina account CRDB nikawaeleza basi wakanambia nipeleke cheque CRDB itafanyiwa kazi.

nkapeleka cheque tarehe 6/9/2017 nikaambiwa nisubir had alhamis ya tarehe8/9/2017 hela itakuw tayar lakin mpaka sasa hela haijaingizwa na Nimeishiwa pesa kabisa naomba msaada wenu
 
Back
Top Bottom