Dr Kantangaze
Senior Member
- Jul 3, 2014
- 124
- 79
Wakuu naomba kujua gharama kujua salio kwa NMB mobile na je ukitumia ATM kuna gharama? Na kiasi gani?
Habari Munkari, tumia namba hii 0800 11 22 33 kuwasiliana na kituo cha huduma kwa wateja. Unaweza pia kutupata kupitia mitandao ya kijamii NMB PLC Tanzania (@NMBTanzania) | Twitter na NMB PLC TanzaniaHivi call centre no ya nmb ni ngapi?mana hii inayoishia na 500 chenga tu!
Mi nataka kufungua akanti na nmb niko ubungo mtanisaidiaje
Mmepandisha riba ya mkopo (personal loan) kutoka asilimia 18 mpaka asilimia 20?Ndugu wana JamiiForums,
Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.
Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.
Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.
4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom