NMB na hazina wanashiriki kuchelewesha mishahara

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
kumekuwa na katabia kanachofanywa na NMB wakishirikiana na hazina kuchelewesha mishahara ya watumushi wa umma kwa kuwa wanapitishia mishahara yao bank tofauti na NMB.
Huu ni mwezi wa tatu au nne tumeshuhudia wafanyakazi wakipewa mishahara katikati ya mwezi unaofuata bila maelezo ya kuridhisha.
 
mkuu kwani kuna tatizo gani, maana mi sielewe, nipo crdb mpaka leo hakijaeleweka, wakati walio nmb walisha pata tangu tar 29 mwezi uliopita, kuna una taarifa zaidi hebu nijuze mkuu
 
mkuu kwani kuna tatizo gani, maana mi sielewe, nipo crdb mpaka leo hakijaeleweka, wakati walio nmb walisha pata tangu tar 29 mwezi uliopita, kuna una taarifa zaidi hebu nijuze mkuu

Ina maana mpaka sasa hujapata mshahara?? Pole sana.
 
sio hazina tu,mi nahisi ni hao NMB wenyewe,maana mishahara ya ofisi niliyopo kwa watu wa NMB haijasoma hadi leo
 
Ina maana mpaka sasa hujapata mshahara?? Pole sana.


Mkuu bado, kama sio ujasiriamali ningekua icu, ila nashindwa kuelewa hizi benki zetu za kibongo, crdb wanadai nmb ndio wanachelewesha, nmb wanadai hazina, basi kazi kweli kweliii
 
wote wenye account za mishahara tofauti na NMB wamechelewa kupata mishahara ya mwezi wa 11
 
hata sie ulichelewa tukapata tar1,dec ..sasa sijuhi ni hazina,nmb ama serikali iko bankrupt ..watu wanahaha aisee!
 
serikali hii ni nzuri tu kwani pesa ipo na inatoka kwa wakati ila kuna watu wanaoshughulikia mishahara katika sekta au idaara husika wanafanya makosa makusudi halafu hata ukifuatilia majibu ni ya ovyo na watu hawa wanajulikana na hata ukifuatilia zaidi hakuna wa kuwawajibisha mpaka mfanyakazi anawajibika kuonga ili asaidiwe kupata mshahara wake ambao ndiyo haki ya msingi kwa mfanyakazi kuuliko kitu chochote kile sasa kwa swala hili hata ikifikia hatua waziri anaambiwa lakini hakuna anaye ogopa na kujirekebisha hii ni hatari sana jamani hakuna usalama wa taifa au wapelelezi wa kufuatilia haya malalamiko? Kwasababu kuna watu kwa makusudi wanafanya mambo ili watu kwa maana ya wafanyakazi waichukie serikali ya kikwete sasa mmekwisha pewa taarifa fuatilieni muone ni wafanyakazi wangapi katika idara zote au maeneo yote hawajalipwa mishahara yao ya miezi iliyopita mpaka sasa na sababu ni nini? Halafu wanaohusika kufanya upuuzi huu muuwambie umma mmewachukulia hatua zipi? Vinginevyo watu wataendelea kuichukia serikali bila sababu za msingi
 
Back
Top Bottom