Nmb mobile kwenda airtel money makato yake makubwa

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
4,911
3,082
Tafadhari naomba kujua kwa wahusika ivi kwa nini huduma za nmb mobile ziko juu sana? Kwenye acaunt yangu ya nmb bank kulikuwa na kiasi cha sh.45,050
Nikatoa pesa kwenye acaunt kiasi cha sh.2000 kwenda airtel money nikaitumia baadae nikatoa tena sh.2000 kwenda airtel money kwa jumla ikawa nimetoa sh.4000 nilipo kuja kucheki balance yangu kwenye acaunt ya bank du ni hatari kwenye 45'050 nikakuta imebaki sh.34'650/=ukiangalia hesabu hapo utakuta wamechukua sh.6400
Kwa makato hayo aisee ni hatari.
 
Unapoingia tu kwenye menu unakatwa sh 350, na kila operation unayoifanya unakatwa hiyo 350. Utaendelea kwa kukatwa 350 mpaka ukamilishe muamala. Baadae kuna change za transfer. Bila kusau airtel nao wana chao. Kama hauna salio huweziingia
 
Du aisee kweli ni shida sema nmb walichowai ni kwasababu hii benk IPO mpaka vijijini
 
Nilikuwa nafanya savings kwenye akaunti ya nmb nimeona ni ujinga haya makato. Nahamia crdb nijaribu
 
Nilikuwa nafanya savings kwenye akaunti ya nmb nimeona ni ujinga haya makato. Nahamia crdb nijaribu
Ayaaaa huko CRDB ndio utajuta makato yao... Cha msingi ujue tu hii biashara ya kuhamisha pesa kutoka bank kupitia simu yako ni ya ghali kupita maelezo ifanye tu under emergency la sivyo tumia ATM ni cheaper 10 times.
 
Back
Top Bottom