TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,667
- 1,566
Katika pita pita zangu za kutafuta ridhiki huwa napita sana chalinze na kufanya biashara kidogo pale na wadau wangu wa eneo lile. hivyo katika muktadha huo Bank ninayoitumia ni NMB tawi la chalinze kwani ndiyo tawi la Bank pekee lililopo eneo lile ingawa pamechangamka kibiashara na uwekezaji. uendeshaji wa tawi hili la Benk ni tofauti sana na ukiukwaji mwingi wa taratibu na sheria za kibenk unaoendelea kufanyika, hizi ni baadhi ya kasoro na kero nilizojionea hapa
1. wafanya biashara wanaokuja kuweka (deposit) fedha nyingi kuchanganyika na wale wanaokuja kuweka au kutaka huduma za kawaida dirishani badala ya kwenda au kutengewa chumba maalumu yaani bulk kwa ajili ya kufanya miamala yao. hii hufanya huduma katika madirisha ya kutolea huduma kuchukua muda mrefu kwani huchukua muda mrefu kuhesabu mfano milioni kumi na tano au ishirini ambazo mtu amekuja kuweka hasa siku za jumatatu na Alhamisi, Pia kuhatarisha usalama wa huyu anyefanya miamala mara kwa mara kwani watu humkariri na hivyo kuwa hatari kwa siku za baadae.
2. usirogwe uombe bank statement, inaweza kukuchukua wastani wa saa moja au saa moja na nusu kupata bank statement hiyo. hapa nashindwa kuelewa wanakwama wapi
3. Wafanyakazi wanafanya kazi kwa kujuana sana na baadhi ya wateja. kuna wateja inafikia hatua hawapangi foleni. Akifika kwenye mlango wa bank, anapiga simu kwa mhudumu wa bank, mhudumu anajifanya kama anakwenda toilet then kama ni muamala zinachukuliwa fedha pamoja na bank paying slips zinagongwa muhuli mtamuona mwenzenu huyoo anaondoka nyie mnakodoa tu macho kwenye foleni. hii inatokea sana kati ya wahudumu na wafanya biashara wakubwa ambao wanakuja kufanya miamala mikubwa hapa kwenye tawi
4. Rushwa kwenye kitengo cha mikopo, ingawa hii inaweza kuwa ni tatizo ndani ya NMB yote lakini kwa chalinze imekithiri. kuna tatizo kubwa sana katika kitengo cha mikopo NMB chalinze, unaweza kuomba mkopo lakini mpaka kuja kuingiziwa mkopo laima umtafute "kikubwa" afisa mikopo
5. cheque transaction ndiyo "kimeo" ukideposit cheque unaweza kaa mpaka siku tatu mpaka nne cheque haijaingizwa katika account ya mteja husika. hii huwafanya wafanya biashara kugombana sana na wateja wao.
jambo la nyie NMB kumshukuru Mungu, ni kwamba katika eneo hili la Chalinze, hakuna tawi lingine la Bank nyingine, lakini kama kungekuwa hata na katawi ka bank yoyote ile, naamini hapa mngebaki na walimu na manesi tu.
niwatakie kazi njema katika ujenzi wa serikali ya viwanda
NMB Bank
close to you