NMB Bado hawajatii maelekezo ya BoT ya kupunguza Riba kwenye Mikopo

Tarehe 27 Julai 2021 BOT ilitoa maelekezo kwa Benki zote nchini kupunguza viwango vya riba kwenye mikopo kutokana na Janga la UVIKO 19.

Benki ya NMB ambayo kwa asilimia kubwa wateja wake ni watumishi wa umma ambao ndio walio pigika kiuchumi Je mpaka leo hii trh 17/9/2021 NMB wamepunguza viwango vya riba ktk mikopo ya wateja wake?

Ieleweke kuwa viwango vya riba vilipaswa vipunguzwe kwenye mikopo ambayo tayari ilikuwepo na pia kwa mikopo ambayo itakopwa baada ya maelekezo hayo ya BOT.

NMB nia yenu ni kuwakwamua wateja wenu au ni kuwadidimiza?

NMB ndio Benki yenye ukwasi nchini kutokana na watumishi wa umma lkn bado haijarudisha fadhila kwao, riba kwa watumishi wa umma ilipaswa ishushwe mara dufu tofauti na wafanyabiashara.

Kazi iendelee.
Unasema kweli ndugu ila tukumbuke na tusisahau mabenki ni kama duka ila ukitaka yaendeshwe kama charity basi yatakufa ndugu
 
Back
Top Bottom