Kama kuna benki yenye kiwango cha chini kwenye ubunifu basi NMB ni moja wapo! Wakati benki zingine zikiwa zimeshaachana na lile sharti la kung'ang'ania mfanyakazi anayetaka mkopo lazima mshahara wake upitie benki yao, NMB wao ndo kwanza wanazidi kusisitiza hilo sharti kama kigezo namba moja!
Benki nyingi zilishaachana na hilo sharti baada ya kuona wanapoteza wateja wengi ambao mishahara inapitia benki nyingine. Kwa mfano CRDB, Barclays, NBC benki ya posta na benki zingine ndogo ndogo kama Bank ABC zote hizi zimeshaondoa hicho kipengele.
Ni sharti ambalo halina maana kwa sababu mshahara unalipwa kutoka hazina hivyo benki ina uhakika wa kupata makato ya mkopo wa mfanyakazi hata kama hapokelei mshahara kwao! Chondechonde NMB badilikeni mmebakia nyinyi peke yenu wenye masharti ya hovyo kama hayo!