NLD yaifagilia chadema kuondolewa bungeni kwa muswada wa katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NLD yaifagilia chadema kuondolewa bungeni kwa muswada wa katiba mpya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M TZ 1, Apr 20, 2011.

 1. M

  M TZ 1 Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk. Emmanuel Makaidi, amesema kuondolewa kwa muswada wa kuundwa kwa tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya bungeni kumetokana na juhudi kubwa zilizofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
  Dk. Makaidi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kufika kwenye ofisi za NIPASHE zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
  Alikuwa akitoka katika ziara ya mikoa ya Mtwara na Lindi ambapo alisema ameamua kuipongeza Chadema kutokana na kuguswa na kazi nzuri inayofanywa hivi sasa na chama hicho ndani na nje ya Bunge.
  "Nimekuja hapa kulizungumzia hili sijatumwa na mtu, chama wala kikundi, Chadema wamenikuna endeleeni na kazi nzuri mnayoifanya kwa faida ya Watanzania, sio kawaida yangu kusifia lakini kwa hili nimeguswa, naongea hivi kama mwenyekiti wa chama changu lakini pia kama mwenyekiti wa vyama vyote nchini, " alisema na kuongeza:
  "Chadema msivunjike moyo kwa vitisho vya CCM kwa sababu kupitia utafiti wangu nilioufanya hivi karibuni kwenye mikoa hapa nchini nimebaini kuwa, mnaungwa mkono kwa asilimia 80 na Watanzania kuhusiana na jitihada zenu za kupigania maslahi ya wananchi, atakayebisha hili nitashindana naye kwa takwimu tu, mimi ni msomi hivyo siropoki," alisema.
  Dk. Makaidi alisema muswada uliotaka kupitishwa ili kuunda tume ya Katiba mpya ulilenga kuwasaliti Watanzania lakini jitihada zilizofanywa na Chadema ndizo zimesaidia kuuondoa bungeni na kuurudisha kwa wananchi.
  "Chadema kama Kambi Rasmi Bungeni kikiongozwa na kiongozi wake, Freeman Mbowe, kimefanya muswada huo kufa kifo cha mende, sitegemei kama muswada huu utarudishwa tena bungeni labda uje ukiwa na maudhui mapya," alisema.
  Akitoa maoni yake kuhusiana na mchakato huo unaoendelea hapa nchini kwa sasa, alisema wakati raia duniani wanataka kuhodhi mamlaka za nchi zao muswada ulikuwa unataka kuweka mamlaka hizo mikononi mwa Rais wa Tanzania.
  "Haya ni makosa na usaliti wa umma wa Watanzania, ombi langu kwa viongozi wa CCM na serikali yao, wajifunze kupitia matukio yanayotokea ulimwenguni kwa sasa, pamoja na nchi za Kifalme na Kiarabu kutaka kuhodhi mamlaka za nchi lakini wananchi wake wanataka kuziendesha kwa maslahi ya watu wote sio kikundi," alisema.
  Kutokana na upinzani mkali uliotokana na kelele, ukosoaji na vilio vya umma dhidi ya muswada huo, Ijumaa iliyopita serikali ililazimika kuuondoa kwenye orodha ya kuwasilishwa katika mkutano wa Tatu wa Bunge.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Safi sana Makaidi, wapashe wale wate wanaokibeza CHADEMA.
   
Loading...