Nkrumah Hall Yesterday: One of my greatest moments in my life, I wish my father was alive....!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
.. to witness his son doing his very first live ( televised)public presentation. During my childhood at Ilala, I remember my late father, John Ramadhan Mjengwa telling me to follow him to a number of public rallies, at Jangwani grounds and even at the National Stadium.
I grew up at Ilala, Iringa Street, House Nr. 27. I remember, in the evenings, seeing my father, outside our Baraza, debating lively with his friends, on issues relating to social- political and even sports. And my father possesed some few political litteratures; books like, ' The Life of Patrice Lumumba' and the one, and banned one, written by John Okelo, ' The Zanzibar Revolution'. Surely, not only my mother, but, my late father, played a role in forming me to become the person I am today.

Na presentation ya jana?

Ilikuwa ni moja ya mitihani migumu kuipitia. Nilielewa dhamana na heshima kubwa niliyopewa; kwamba kwenye mwaka wa 51 wa Uhuru. Mwaka wa kwanza kuelekea miaka 50 ijayo, hivyo basi, miaka 100 ya Uhuru ifikapo Desemba 9, 2061, napewa jukumu la kutoa mchango wangu wa fikra juu ya Amani na Utulivu wa Taifa letu kwa miaka 50 ijayo.
Nilielewa, kuwa sitakuwa hai itapofika siku ya Desemba 9, 2061, lakini, historia itakuja kunihukumu kwa nitakachokisema kwa taifa katika dakika kumi nilizopewa.

Hivyo, kama ilivyo kawaida yangu, kwenye fikra zangu hakukuwa na Chadema, CCM wala majina ya wagombea Urais, bali, kwa siku mbili nzima za matayarisho, kichwa changu kilijaa fikra ya nchi yetu kwa miaka 50 ijayo. Ilihusu kuchangia ndoto ya taifa letu.

Kwa kawaida kwenye jambo zito lililo mbele yangu huwa kwa kiasi nafunga kula chakula pia. Jana asubuhi nilikunywa chai ya rangi isiyo sukari na vipande viwili vya vya tikiti . Mchana sikula chochote, nilikunywa maji tu.
Nilipofika Nkrumah Hall niliendelea kunywa maji. Chupa mbili nilizowekewa mezani nilizimaliza ndani ya dakika 20.

Nilitamani kuchukua chupa ya maji ya Profesa Gaudence Mpangala aliyekaa jirani yangu. Na alikuwa hajazifungua. Sikufanya hivyo, ingelikuwa utovu wa adabu.

Mara nilimwona ndugu yangu January Makamba akimalizia presentation yake. Nilifahamu kuwa inayofuata ni yangu. Mwenyekiti wa mjadala alishaninong'oneza, kuwa ningekuwa na dakika 8, lakini angeweza kuongeza 2. Nilimshukuru, maana, presentation yangu niliipangia dakika 8, na mbili za dharura, kama ingehitajika. Niliamua kuwa ningewasilisha bila kusoma kwenye karatasi. Kwamba ningeongea kutoka kichwani tu.

Nilichukua kipande cha karatasi kilichokuwa na mihili minne ya presentation, kunisaidia kama ingetokea nikapata ' break-down' kwenye kuwasilisha.

Na ndugu yangu January Makamba aliniumiza kichwa pale kwenye presentation yake alipogusia central theme ya presentation yangu. January aliongelea kidogo juu ya Haki pale unapojadili amani na utulivu. Na mimi nilipanga kujikita kwenye mambo mawili; Uzalendo na Haki. Bahati nzuri January alihama mapema kwenye reli yangu ya fikra. akaenda kwenye Elimu na Rasilimali. Nilipumua. Hivyo, alichogusia January kuhusu haki hakikuathiri flow yangu ya hoja.

Nikaanza presentation yangu. Niliyafanyia kazi mashaka ya sekunde za mwanzo kwa kumlink Dr. Semboja kwenye hoja ya kuwa na ndoto ya taifa na kuhusisha suala la rasilimali aliloliongelea Dr. Semboja. Nikawa comfotable katika hilo, hivyo, nikapata entry muafaka ya presententation yangu. Nikaendelea kujitahidi kuwa composed and focused.

Na presentation kufanikiwa ama kutofanikiwa huchangiwa pia na namna unavyoanza na kuhitimisha. Kichwani nilikuwa na mahitimisho mawili; moja la dakika moja na nusu, lingine la dakika 3. Mwenyekiti wa mjadala aliponiashiria kuwa zimebaki dakika 2, basi, sikuwa na wasi wasi. Nikaswitch kwenye hitimisho la dakika moja na nusu.

Nikahitimisha presentation yangu. Nikasikia ukumbi ukishangilia sana. Nikasema moyoni; Wow, I Made It! I realised that I did a more than a ‘Ok' job.

For a while, my thoughts went to my late father, John Ramadhan Mjengwa. I realy wish he was alive to see and hear his son doing that presentation. And I dedicate to him , that piece of presentation I made for our country's future.

I thank you too, for following what I am doing.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam
 
Mjengwa hapa umeelezea furaha yako lkn sio kile ulichoelezea its pity kuelezea your private ktk Natioanal Dialogue of Next 50 years Is not about you! Maggid is about Tanzanian Sorry kuteleza~!
 
Mjengwa hapa umeelezea furaha yako lkn sio kile ulichoelezea its pity kuelezea your private ktk Natioanal Dialogue of Next 50 years Is not about you! Maggid is about Tanzanian Sorry kuteleza~!

Sinshoo,
Asante sana, lakini sidhani kama kuna ubaya katika kuyaelezea mazingira kama hayo ya mtu alikotokea. Tatizo letu Watanzania huwa tunaona aibu hata kutaja majina ya vijiji tulivyozaliwa au kule wazazi wetu walikozaliwa. Ni hali ya kushindwa kujitambua, kujiamini na kuthubutu.

Ni fikra zangu tu.
Maggid
 
ke kwa chama chake baada ya kukatwa jina kugombea u-NEC na wengine kadhaa. Hebu kumbusha uliongea nini inawezekana hata marehemu dingi wako (who you think he would have been proud) hakumbuki uliongea nini huko aliko. Nimejaribu kuangalia hata kwenye news papers za leo haumo pamoja na kwamba ni mwandishi wa siku nyingi katika media tofauti. Tililikaaaaaaaaa
 
Magid@ leta nondo ulizoshusha...ulipozaliwa.. ulipokulia..utakapofia..hayo tuyaache kwa sasa...tujadili mustakabali na nafasi ya kuendelea kwa dola hili linalonyonywa na kunguni wachache..
 
Sinshoo,
Asante sana, lakini sidhani kama kuna ubaya katika kuyaelezea mazingira kama hayo ya mtu alikotokea. Tatizo letu Watanzania huwa tunaona aibu hata kutaja majina ya vijiji tulivyozaliwa au kule wazazi wetu walikozaliwa. Ni hali ya kushindwa kujitambua, kujiamini na kuthubutu.

Ni fikra zangu tu.
Maggid


Hi Maggid,

May you please attach your presentation for those of us who were not there? If you dont mind please do the needful.


Congrats for that achievement & Cheerz,
 
Kuzungumza ulivyozungumza sio jambo dogo, unastahili pongezi.

Kwa wale ambao hawakukusikia ama kukuona jana unaweza kuweza kuweka muhitasari hapa.
 
Kwa wale tuliokuwepo tuliona ulikuwa wa kawaida 2 na mimi sikushangaa kumwona maggid mjengwa kuwa ni mmoja wa waalikwa kwenye kongamano kama hilo.Cha kushangaza ni jinsi ulivyojiexpress hapa kuwa umelichukulia hilo tukio kama vile hukustahili! Nakushangaa majjid kwa sababu wewe una media attention.Je tungekuwa akina sisi ambao jf na mitandao mingine ya kijamii ndo inayotutambia ingekuwaje kwa mtazamamo wako? Mi nadhani kongamano hilo yeyote anayejua kuongea angeweza kuwa msemaji kwa sababu watanzania wote tuko sawa tu na wala usichukulie kwamba kilikuwa ki2 pecurior saaana
 
Katika wachangiaji wote waliozungumza katika lile kongamano la jana nilifurahishwa na alichokiongea Mzee Butiku, kwamba Watanzania sasa tuache kulalamika, tuchape kazi jamani, kila mmoja katika nafasi yake achape kazi nchi hii isonge mbele. Mzungumzaji alienitibua ni Deo Filikunjombe, yeye pamoja na kwamba ni Kiongozi akarudia yale yale aliokataza Mzee Butiku, KULALAMIKA.
 
HONGERA SANA KAKA MAGGID MJENGWA: <br>Umetoa hotuba nzuri kulingana na maandalizi yako. You have the right to be proud of yourself! WHY NOT? watanzania tupo wazuri kukosoa zaidi ya ku-Appreciate. kama ulivyoeleza malengo yako hayakuwa kwenye chama ama itikadi yoyote zaidi ya MSTAKABALI WA TANZANIA KWA MIAKA 5O IJAYO. Umelenga penyewe Mjengwa 'congrats'. Heshima uliyopewa ni kubwa na umeitendea haki. Binafsi nikuombe uiweke ile hotuba yako nzuri hapa kwenye JF ili wale ambao hawakuweza kukusikiliza pale NKURUMAH HALL-UDSM wapate fursa ya kuona mchango wako. Ukiiweka kwenye BLOG yako pia sio mbaya.<br>Thanks.
 
Sikuona kipya alichoongea chenye kusukuma utendaji utakaoleta tija
 
Iweke tafadhali,kuelezea furahayako sio mbaya tatizo umekua mmbaguzi kudhani kua watu wote walikua kwenye tv. Wengine ratiba ya kipindi tulikua nayo alakini mazingira ya majukumu hayakuturuhusu. Mbona ESTER WASIRA tumempata vilivyo...!
Tiririka mkuu,mwana blogu.
 
Hongera sana Magid, wanaokubeza achana nao. Kusimama mbele ya watu na media si jambo wanaloweza wengi.

Hongera saana, wapuuze hao. Lakini karibu kwenye chama cha wakombozi CHADEMA. Kama wewe ni mpenda haki njoo huku kwenye chama cha kujitolea, hatuna pesa kama Magamba
 
Sikuona kipya alichoongea chenye kusukuma utendaji utakaoleta tija

Ukiwa na roho mbaya kama hii ya kubeza watu kama hivi huna tofauti na mtu anaemloga jirani yake kwa kumuonea wivu wa maendeleo yake
 
Maggid hujawahi fanya presentation katika maisha yako?. Sasa hapa kilichokuwa 'so special' ni kipi. Au ukumbi wa Nkurumah?. Degree holder yeyote lazima atakuwa ameishafanya presentation labda km huna hii kitu. Nilivyokuwa O'level tulikuwa na Morning Talk, tulikua tukiongea hata dk 15.
 
Ingekua vyema kama ungetuwekea hapa hiyo presentation yako. Pamoja na kwamba si kitu kibaya kuona fahari baada ya presentation "nzuri" uliyofanya; mimi nilitegemea zaidi kutoka kwako...
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom