Nkrumah Hall Yesterday: One of my greatest moments in my life, I wish my father was alive....!

Sasa ulitaka kila mtu pale aeleze hayo mawazo yako hapo juu ndiyo uone amesema cha maana? Hata mimi nina mawazo yangu ambayo ninaona ni ya maana kwa mustakabali wa taifa letu lakini hayakusemwa pale. Hiyo haifanyi kilichosemwa pale kisiwe na maana.

Hivi nawe ili uonekane umechangia lazima uchukue maneno yako uyaweke kwa mwingine. Hakuna sehemu niliposema presentation yake haikuwa na maana kwa sababu it never captured areas highlighted myself. Nimeonyesha jinsi presentation yake haikuwa na conceptual framework that captures grave circumstances that to me have created a bad shape of our country. Haki aliyotaka kutuonyesha kwa sasa na miaka 50 ijayo si kitu kama mamabo niliyoyaonesha ambayo kwa wazalendo wengi ni maovu (vices) na kwa wachache ni neema maana kwayo wamekuwa matajiri yataendelea kutokea. Unaweza ukaimba haki lakini kama hujaondeoa variable zinazoibaka haki basi haki ya kweli haitakuwepo bali itabaki kwenye makabrasha na imani ya kweli haitakuwepo bali woga na hofu kama ilivyokuwa Tanzania ya leo. Mfano elimu ni ufunguo wa maarifa na maendeleo lakini kama tunaendelea kuwa na elimu ambayo wachache wanapat elimu bora na wachache wanabaki shule za kayumba na wanafika kidato cha nne hawajui kusoma na kuandika na wewe unapewa nafasi kuchangia unashindwa kukapture kitu kama hicho kama kizingiti cha haki basi. Nakubali kila mtu ana mawazo yake lakini on contectual basis kunakuwa na similarities na consistency ambavyo sikuviona katika presenatation ya Mjengwa
 
Naona uzi wako unalenga kutaka tukujadili wewe binafsi badala ya kile ulichokiwasilisha.
 
Binafsi nilifurahishwa na utulivu, kujiamini na hoja ulizowasilisha. Lazima ujipongeze na sisi tunakupongeza sio kazi ndogo ile. Kuongea mbele ya kadamnasi ya wasomi ni tofauti na kuandika kwa ajili ya watu kujisomea wenyewe.
 
.. to witness his son doing his very first live ( televised)public presentation. During my childhood at Ilala, I remember my late father, John Ramadhan Mjengwa telling me to follow him to a number of public rallies, at Jangwani grounds and even at the National Stadium.
I grew up at Ilala, Iringa Street, House Nr. 27. I remember, in the evenings, seeing my father, outside our Baraza, debating lively with his friends, on issues relating to social- political and even sports. And my father possesed some few political litteratures; books like, ‘ The Life of Patrice Lumumba’ and the one, and banned one, written by John Okelo, ‘ The Zanzibar Revolution’. Surely, not only my mother, but, my late father, played a role in forming me to become the person I am today.

Na presentation ya jana?

Ilikuwa ni moja ya mitihani migumu kuipitia. Nilielewa dhamana na heshima kubwa niliyopewa; kwamba kwenye mwaka wa 51 wa Uhuru. Mwaka wa kwanza kuelekea miaka 50 ijayo, hivyo basi, miaka 100 ya Uhuru ifikapo Desemba 9, 2061, napewa jukumu la kutoa mchango wangu wa fikra juu ya Amani na Utulivu wa Taifa letu kwa miaka 50 ijayo.
Nilielewa, kuwa sitakuwa hai itapofika siku ya Desemba 9, 2061, lakini, historia itakuja kunihukumu kwa nitakachokisema kwa taifa katika dakika kumi nilizopewa.

Hivyo, kama ilivyo kawaida yangu, kwenye fikra zangu hakukuwa na Chadema, CCM wala majina ya wagombea Urais, bali, kwa siku mbili nzima za matayarisho, kichwa changu kilijaa fikra ya nchi yetu kwa miaka 50 ijayo. Ilihusu kuchangia ndoto ya taifa letu.

Kwa kawaida kwenye jambo zito lililo mbele yangu huwa kwa kiasi nafunga kula chakula pia. Jana asubuhi nilikunywa chai ya rangi isiyo sukari na vipande viwili vya vya tikiti . Mchana sikula chochote, nilikunywa maji tu.
Nilipofika Nkrumah Hall niliendelea kunywa maji. Chupa mbili nilizowekewa mezani nilizimaliza ndani ya dakika 20.

Nilitamani kuchukua chupa ya maji ya Profesa Gaudence Mpangala aliyekaa jirani yangu. Na alikuwa hajazifungua. Sikufanya hivyo, ingelikuwa utovu wa adabu.

Mara nilimwona ndugu yangu January Makamba akimalizia presentation yake. Nilifahamu kuwa inayofuata ni yangu. Mwenyekiti wa mjadala alishaninong’oneza, kuwa ningekuwa na dakika 8, lakini angeweza kuongeza 2. Nilimshukuru, maana, presentation yangu niliipangia dakika 8, na mbili za dharura, kama ingehitajika. Niliamua kuwa ningewasilisha bila kusoma kwenye karatasi. Kwamba ningeongea kutoka kichwani tu.

Nilichukua kipande cha karatasi kilichokuwa na mihili minne ya presentation, kunisaidia kama ingetokea nikapata ‘ break-down’ kwenye kuwasilisha.

Na ndugu yangu January Makamba aliniumiza kichwa pale kwenye presentation yake alipogusia central theme ya presentation yangu. January aliongelea kidogo juu ya Haki pale unapojadili amani na utulivu. Na mimi nilipanga kujikita kwenye mambo mawili; Uzalendo na Haki. Bahati nzuri January alihama mapema kwenye reli yangu ya fikra. akaenda kwenye Elimu na Rasilimali. Nilipumua. Hivyo, alichogusia January kuhusu haki hakikuathiri flow yangu ya hoja.

Nikaanza presentation yangu. Niliyafanyia kazi mashaka ya sekunde za mwanzo kwa kumlink Dr. Semboja kwenye hoja ya kuwa na ndoto ya taifa na kuhusisha suala la rasilimali aliloliongelea Dr. Semboja. Nikawa comfotable katika hilo, hivyo, nikapata entry muafaka ya presententation yangu. Nikaendelea kujitahidi kuwa composed and focused.

Na presentation kufanikiwa ama kutofanikiwa huchangiwa pia na namna unavyoanza na kuhitimisha. Kichwani nilikuwa na mahitimisho mawili; moja la dakika moja na nusu, lingine la dakika 3. Mwenyekiti wa mjadala aliponiashiria kuwa zimebaki dakika 2, basi, sikuwa na wasi wasi. Nikaswitch kwenye hitimisho la dakika moja na nusu.

Nikahitimisha presentation yangu. Nikasikia ukumbi ukishangilia sana. Nikasema moyoni; Wow, I Made It! I realised that I did a more than a ‘Ok’ job.

For a while, my thoughts went to my late father, John Ramadhan Mjengwa. I realy wish he was alive to see and hear his son doing that presentation. And I dedicate to him , that piece of presentation I made for our country’s future.

I thank you too, for following what I am doing.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam

Hivi kama January Makamba, Joseph Butiku, na wachangiaji wote waje wajisifu hapa kwa presentatiins zao, inamaanisha nini? Halafu wewe ndo mwandishi mwenye taaluma ya uandiahi Tanzania. Ungetumia muda huu na jukwaa hili kuendeleza mchango wako zaidi ya ule wa kwenye presentation ningekuona wa maana sana. Lakini nakuona kama umebweteka kana kwamba umefika mwisho wa kufikiri kwa kuja na thread ya kujipongeza. Hakuna kitu. Ikiwa kila mwanaJF atakuja na sifa zake hape, historia yake na mambo mengi yanayofanan na hayo wewe utaonekana dagaa kwenye Sangara. Sijaona cha maana kwenye thread yako zaidi ya kuchukua muda wangu kukuelimisha kidogo ingawaa naona elimu ya uandishi haikusaidii kabisa.
 
binafsi nakupongeza bro, mjengwa. umeeleza ukweli juu ya furaha yako kwani ulihitimisha vyema kazi uliyopewa ndani ya muda uliopewa na wasikilizaji kukupigia makofi ni ishara ya kukubaliana nawe. pamoja nawe nampongeza pia Prof Shivji kwa lile alilosema viongozi wawe wawazi kabisa wanaongoza taifa lipi? kati ya walionacho na wasionacho ndani ya taifa lililogawanyika la TANZANIA. hakika kuna siri nzito hapo kwa wanajf
 
Yafaa mleta uzi wetu ajiulize mbona mwana JF mahiri ndugu Kitila Mkumbo, alizungumza masuala ya msingi lakini hakuanzisha uzi wa kujielezea kama alivyofanya yeye?
Mathalani ,hoja ya Ndugu Aldin Mutembei iliyosisitiza umuhimu na haja ya kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika ngazi ya sekondari na vyuoni kama mkakati wa kuongeza ufaulu ilipingwa na Kitila Mkumo aliyehoji pamoja Elimu ya Msingi kutolewa kwa lugha ya Kiswahili mbona tafiti na takwimu zinaonyesha bado ufaulu katika ngazi hiyo upo chini kulinganisha na Sekondari kunapotumiwa Kiingereza?
Kuzungumza ktk ukumbi wa Nkurumah kamwehakuwezi kuwa suala kubwa kiasi cha kuhadithia watu maana hata wasanii wengi wa Bongo Fleva nao wamepata kupata fursa ya kutumbuiza wanazuoni!
Badala ya kuleta hapa jamvini mawazo usiyokubaliana ama unayokubaliana na wawasilishaji wenzako,wewe unaleta porojo za kutaka kuchukua maji ya Prof.Gaudence Mpangala!!Hii ni nini sasa?
Kiu yako ya maji jana inahusiana na chochote kuhusu miaka 50 ijayo kweli?
Hapana.

sikutaka ku log in ila imenibidi baada ya kuona hii post ya huyu gamba mjengwa, zamani mjengwa alikuwa anaandika vizuri ila aliporuhusu njaa imuongoze kwenye uandishi wake hapo ndipo alipopoteza mwelekeo. nilikuwa simuelewi kwenye uandishi wake kwa nini anakwepa kuonyesha uhusiano wa moja kwa moja uliopo wa matatizo yaliyopo kwenye jamii na chama kilichopo madarakani kumbe alikuwa anakusudia kugombea NEC, juzi ndio kajidhihirisha. NI MCHUMIA TUMBO TU KAMA WENZAKE AKINA NEVIL MEENA.
 
Hivi nawe ili uonekane umechangia lazima uchukue maneno yako uyaweke kwa mwingine. Hakuna sehemu niliposema presentation yake haikuwa na maana kwa sababu it never captured areas highlighted myself. Nimeonyesha jinsi presentation yake haikuwa na conceptual framework that captures grave circumstances that to me have created a bad shape of our country. Haki aliyotaka kutuonyesha kwa sasa na miaka 50 ijayo si kitu kama mamabo niliyoyaonesha ambayo kwa wazalendo wengi ni maovu (vices) na kwa wachache ni neema maana kwayo wamekuwa matajiri yataendelea kutokea. Unaweza ukaimba haki lakini kama hujaondeoa variable zinazoibaka haki basi haki ya kweli haitakuwepo bali itabaki kwenye makabrasha na imani ya kweli haitakuwepo bali woga na hofu kama ilivyokuwa Tanzania ya leo. Mfano elimu ni ufunguo wa maarifa na maendeleo lakini kama tunaendelea kuwa na elimu ambayo wachache wanapat elimu bora na wachache wanabaki shule za kayumba na wanafika kidato cha nne hawajui kusoma na kuandika na wewe unapewa nafasi kuchangia unashindwa kukapture kitu kama hicho kama kizingiti cha haki basi. Nakubali kila mtu ana mawazo yake lakini on contectual basis kunakuwa na similarities na consistency ambavyo sikuviona katika presenatation ya Mjengwa

Bigaraone, hiyo conceptual fremwork unayoisema mjengwa angeweza kuiongea ila angeiongeaje bila kuiponda CCM chama ambacho yeye ni cadre wake, halafu anajifanya hakutaka kuchanganya na siasa. Yeye anajiona ni cadre kuliko makamba na filikunjombe!! NJAA BWANA!!, Filikunjombe kataja tatizo kuu la uongozi tulilonalo, yeye mjengwa na njaa yake anamung'unya maneno. mimi nilishaga mzarau huyu mjengwa tokea zamani ambaye anabisha atafute article zake kipindi cha uchaguzi ndio utamuona mjengwa mwenyewe akiwa anatumia tumbo kufikiri.
 
Kwa upande wangu hakuna presenter kutoka meza kuu aliyeongea vitu vya maana zaidi ya Kitila Mkumbo wengine wote Ushuzi wa bata tu, huyo semboja mwenyewe si ndio alikuwa kwenye inner circle ya kikwete kama mchumi tokea 2005, hizo sababu alizozitoa kuhusu kwa nini uchumi unapanda na umasikini unaongezeka na hiyo point yake ya ku nationalize uchumi wa madini kwa nini hakuwafeed magamba wenzake, NJAA BWANA!!! . kwa upande wa presenters kutoka kwenye floor aliyeongea point ni Mzee butiku tu. Uzuri wa nkurumah watu hawaangalii wewe unasoma au umekariri kama mjengwa, watu wanasikiliza kile unachosema kina hoja inayoeleweka? Mzee butiku aliongea maneno machache sana lakini alieleweka kuliko wale maprofesa wa kiswahili akina mutembei.

hata easther alishindwa kucompress hoja zake pale nkurumah, tumekuja kumwelewa huku JF, sisi wengine hatuangalii makofi unayopigiwa tunaangalia content ya ulichoongea, hivyo hata mjengwa unayo nafasi ya kumalizia kile ulichoshindwa kukariri kutokana na ukosefu wa bytes unaweza kusuplement hapa JF
 
Hongera mzazi, changamoto zinazo tolewa hapa naamini utazifanyia kazi.
 
Ndugu zangu,

Nimesoma maoni yote humu kuhusiana na thread niliyoianzisha.

Nawashukuru wote walionipongeza na kunitia nguvu katika niyafanyayo. Nawashukuru pia walionikosoa kwa hoja. Siwezi pia kuacha kuwashukuru walionibeza kwa minajiri ya kunikatisha tamaa. Hii ndio maana halisi ya demokrasia. Watu wawe huru kutoa mawazo yao. Ni wajibu pia kwa mwuungwana kuyasikiliza hata yale ya wenye kukubeza, kukudharau na kukuita majina. Na ndio maana ya elimu; sikiliza, zingatia unayoyasikiliza, yatafakari, yachuje, hoji, tafiti na baadae yafanyie kazi yale yenye tija kwako na jamii. Ni kwa kwenda kwenye jamii na kusambaza maarifa uloyapata. Binadamu tunajifunza kila siku, kutoka kwa wadogo na wakubwa.

Ndugu zangu,

Kuna wenye kuniomba niweke maandishi ya presentation yangu ya pale Nkurumah. Niwe mkweli kwenu; Presentation ile sikuiandika mahala popote kabla na hata baada ya kuitoa. Niliipanga kichwani na kuitoa kutoka kichwani.

Najua niliongea nini, lakini , hata nikiandika sasa, haiwezi ikawa kama vile nilivyoongea kwa dakika zile kumi. Ingekuwa vema kama nitapata sauti iliyorekodiwa nikaiweka hapa. Natumaini nitaipata, maana hata mimi sijasikia marudio ya nilichokiongea kwenye sauti. Natamani nisikie mwenyewe pia.

Hivyo basi, mtaniwia radhi, kikaratasi kile nilichokuwa nacho niliandika point nne kama mihimili ya hoja niliyokwenda kuwasilisha; 1. Intro, 2. Vijana 3. Uzalendo na Haki 4. Hitimisho.

Naelewa kuwa wengi huandika presentation zao na hata kuzisoma wakati wakiziwakilisha. Hilo huwasaidia hata kwenye kugawa copy za presentation hizo. Lakini mimi hupenda zaidi kuandaa points tu za nitakachoongea, kisha kuweka kichwani nitakachokiongea. Naamini husaidia kuifanya hadhira yako kuwa more engaged katika unachokiongea. Tunaweza kuwa na mitazamo tofauti, huo ni wangu.

Asanteni sana.

Maggid,
Iringa.
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
Back
Top Bottom