Nkrumah Hall Yesterday: One of my greatest moments in my life, I wish my father was alive....!

Hongera sana na naamini waliokuwepo watatuhabarisha zaidi ila kwa uandishi wako na maadui uliokuwa nao hapa JF nitashanga kama itapita bila kutukanwa kidgo.Tusubiri tuone.
 
Hongera Maggid, that was a very good beggining, as nobody could discover it, to be your first presentation at nkurumah
 
Kutoka moyoni nikupongeze ndg M. Mjengwa kwa hotuba nzuri ya kusisimua sana ya jana pale Nkrumah Hall. Kwa kweli nilisisimka sana na hasa ulipo-base kwenye National Interest instead of the political party you support! BIG UP...!
 
Sinshoo,
Asante sana, lakini sidhani kama kuna ubaya katika kuyaelezea mazingira kama hayo ya mtu alikotokea. Tatizo letu Watanzania huwa tunaona aibu hata kutaja majina ya vijiji tulivyozaliwa au kule wazazi wetu walikozaliwa. Ni hali ya kushindwa kujitambua, kujiamini na kuthubutu.

Ni fikra zangu tu.
Maggid
Sioni kwanini unahangaika na kutupotezea muda wetu kujadili swala la wewe kusimama mbele ya hadhara na kuongea!Mimi nilidhani ungekuja kujazia yale uliyoshindwa kuyasema pale Nkurumah hall kwa kuwa muda uliopewa haukutosha! sasa kutamani marehemu baba yako angekuwapo kusikiliza upuuzi wako kunatusaidia nini sisi watanzania tulioingizwa katika chuki za kidini na viongozi dharimu wa CCM? Wacha ulimbukeni bwana mdogo eboo!
 
tell us what you presented at nkrumah hall c'z you are telling us pleasure that you got from the presentation that you did of which is not important but the content in your presentation
i don't have any problem about the dedication that you are giving to your late father but you could have given even a little content for that case you are telling us that you was not sure with what you prepared
 
Maggid,

Hongera kwa kuweza kusema kile ulichokisema lakini it's very unfortunate to reveal to us that you made trouble half way. Kabla hujaenda kuelezea mada uliyosema wewe ulishaanza kuogopa na labda ni kwa sababu hukumpa mtu mwenye uzoefu wa uwasilishaji mada ili akusaidie proof reading that could have added value in your presentation. A man is a child of prevailing circumstances na kwa kweli kufanya presentation bila kugusia matukio ya hivi karibuni ya EPA, Richmond, IPTL, RADA, Buzwagi, ununuzi wa ndege ya rais, utoroshaji wa wanyama, uuzwaji wa mbuga ya Loliondo, Meremeta, mauaji ya raia yanayofanywa na jeshi la polisi, utitiri wa shule za kata ambazo watoto wa masikini wanasukumwa na mengine ni kutokuitendea haki mada nzima ya Haki na Amani.

Taifa ambalo viongozi wake hawashtuki na kufanya bidaa kuzuia hayo niliyotaja yasije kutokea now and in near and distant future, miaka hamsini unayoiongelea ni ndoto na usanii. Hivi ni vitu tangible na vimetokea na kufanywa na viongozi wetu wakiwa na akili timamu na vina nguvu ya kisheria. Haki itatoka wapi wakati matukio hayo yamebabaka haki za msingi za binadamu. Sijagusia ardhi inayochukuliwa na wageni, madini yanagawiwa bure na Dr. Haji alienelezea vizuri sana.

Kwa hiyo wewe na Makamba mlitaka kutufanya watumwa wa historia na kibaya hamkutaka kusema kama yale yaliyofanywa na viongozi waliopita kama walikuwa na purpose, na vision au mission au walikuwa wakifata mood of public na asubuhi wanakurupuka na kuamua kufanya ili kuufurahisha umma kwa muda mfupi ili wapate kutawala
 
Sioni kwanini unahangaika na kutupotezea muda wetu kujadili swala la wewe kusimama mbele ya hadhara na kuongea!Mimi nilidhani ungekuja kujazia yale uliyoshindwa kuyasema pale Nkurumah hall kwa kuwa muda uliopewa haukutosha! sasa kutamani marehemu baba yako angekuwapo kusikiliza upuuzi wako kunatusaidia nini sisi watanzania tulioingizwa katika chuki za kidini na viongozi dharimu wa CCM? Wacha ulimbukeni bwana mdogo eboo!
Sasa huu tuuite wivu,chuki au nini? Kama ule unauita ni upuuzi basi sijui kitu cha maana kwako ni nini.
 
hongera! binafsi napenda mtu anapoeleza feeling zake, inakujenga na kujenga wengine wanaopenda kupita ktk napito yako. napenda...
 
QUOTE]A

Hongera kwa kuweza kusema kile ulichokisema lakini it's very unfortunate to reveal to us that you made trouble half way. Kabla hujaenda kuelezea mada uliyosema wewe ulishaanza kuogopa na labda ni kwa sababu hukumpa mtu mwenye uzoefu wa uwasilishaji mada ili akusaidie proof reading that could have added value in your presentation. A man is a child of prevailing circumstances na kwa kweli kufanya presentation bila kugusia matukio ya hivi karibuni ya EPA, Richmond, IPTL, RADA, Buzwagi, ununuzi wa ndege ya rais, utoroshaji wa wanyama, uuzwaji wa mbuga ya Loliondo, Meremeta, mauaji ya raia yanayofanywa na jeshi la polisi, utitiri wa shule za kata ambazo watoto wa masikini wanasukumwa na mengine ni kutokuitendea haki mada nzima ya Haki na Amani. Taifa ambalo viongozi wake hawashtuki na kufanya bidaa kuzuia hayo niliyotaja yasije kutokea now and in near and distant future, miaka hamsini unayoiongelea ni ndoto na usanii. Hivi ni vitu tangible na vimetokea na kufanywa na viongozi wetu wakiwa na akili timamu na vina nguvu ya kisheria. Haki itatoka wapi wakati matukio hayo yamebabaka haki za msingi za binadamu. Sijagusia ardhi inayochukuliwa na wageni, madini yanagawiwa bure na Dr. Haji alienelezea vizuri sana. Kwa hiyo wewe na Makamba mlitaka kutufanya watumwa wa historia na kibaya hamkutaka kusema kama yale yaliyofanywa na viongozi waliopita kama walikuwa na purpose, na vision au mission au walikuwa wakifata mood of public na asubuhi wanakurupuka na kuamua kufanya ili kuufurahisha umma kwa muda mfupi ili wapate kutawala
Sasa ulitaka kila mtu pale aeleze hayo mawazo yako hapo juu ndiyo uone amesema cha maana? Hata mimi nina mawazo yangu ambayo ninaona ni ya maana kwa mustakabali wa taifa letu lakini hayakusemwa pale. Hiyo haifanyi kilichosemwa pale kisiwe na maana.
 
Sasa huu tuuite wivu,chuki au nini? Kama ule unauita ni upuuzi basi sijui kitu cha maana kwako ni nini.
Habari za siku nyingi bwana Sweke! Nasema hivi, hiki alichokiandika hapa ni upuuzi! Yeye alialikwa na kupewa mada ya kuongelea na akaongea watu wakamsikia, wakumukubali walimukubali na waliombeza walimbeza, sasa cha kuja hapa tena na talalila za oh, laiti baba yangu angekuwepo......... kama sio upuuzi ni nini? au tuseme alikuwa hajiamini? By the way, ninini kipya alichokisema pale Nkurumah hall?
 
Yafaa mleta uzi wetu ajiulize mbona mwana JF mahiri ndugu Kitila Mkumbo, alizungumza masuala ya msingi lakini hakuanzisha uzi wa kujielezea kama alivyofanya yeye?
Mathalani ,hoja ya Ndugu Aldin Mutembei iliyosisitiza umuhimu na haja ya kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika ngazi ya sekondari na vyuoni kama mkakati wa kuongeza ufaulu ilipingwa na Kitila Mkumo aliyehoji pamoja Elimu ya Msingi kutolewa kwa lugha ya Kiswahili mbona tafiti na takwimu zinaonyesha bado ufaulu katika ngazi hiyo upo chini kulinganisha na Sekondari kunapotumiwa Kiingereza?
Kuzungumza ktk ukumbi wa Nkurumah kamwehakuwezi kuwa suala kubwa kiasi cha kuhadithia watu maana hata wasanii wengi wa Bongo Fleva nao wamepata kupata fursa ya kutumbuiza wanazuoni!
Badala ya kuleta hapa jamvini mawazo usiyokubaliana ama unayokubaliana na wawasilishaji wenzako,wewe unaleta porojo za kutaka kuchukua maji ya Prof.Gaudence Mpangala!!Hii ni nini sasa?
Kiu yako ya maji jana inahusiana na chochote kuhusu miaka 50 ijayo kweli?
Hapana.
 
Ingekua vyema kama ungetuwekea hapa hiyo presentation yako. Pamoja na kwamba si kitu kibaya kuona fahari baada ya presentation "nzuri" uliyofanya; mimi nilitegemea zaidi kutoka kwako...

Binafsi nakupongeza ni mmoja wa watu waliojieleza vizuri na kwa ufasaha tena bila kusoma na umeonyesha uzalendo wa hali ya juu sana ahsante mjengwa
 
Yafaa mleta uzi wetu ajiulize mbona mwana JF mahiri ndugu Kitila Mkumbo, alizungumza masuala ya msingi lakini hakuanzisha uzi wa kujielezea kama alivyofanya yeye?
Mara unaleta porojo za kutaka kuchukua maji ya Prof. Mpangala!!Hii ni nini sasa?
Kiu yako ya maji jana inahusiana na chochote kuhusu miaka 50 ijayo kweli?
Hapana.
Labda sababu ni hii hapa

Mbunge wa ilula :Hongera Maggid, that was a very good beggining, as nobody could discover it, to be your first presentation at nkurumah


Tuondoe uchama, tumpongeze na kumtia moyo zaidi.
 
Why we Tanzanian? U made it na kujipongeza ni muhimu. Wabongo kazi yetu ni kubeza tu. Go go go Maggid.
 
Sinshoo,
Asante sana, lakini sidhani kama kuna ubaya katika kuyaelezea mazingira kama hayo ya mtu alikotokea. Tatizo letu Watanzania huwa tunaona aibu hata kutaja majina ya vijiji tulivyozaliwa au kule wazazi wetu walikozaliwa. Ni hali ya kushindwa kujitambua, kujiamini na kuthubutu.

Ni fikra zangu tu.
Maggid
Wangelijua kuwa Dreams ambazo wewe ulikuwa nazo ndizo uwa zinadrive watu kufanya makubwa!!!Bill Clinton alikuwa Rais wa Marekani kwa ndoto baada ya kumshika mkono aliyekuwa Rais wa USA miaka ya 1960s, Marehemu JF Kennedy pale alipokwenda kutembelea Ikulu ya Marekani kama Mwanafunzi.Vivyo hivyo Obama amekuwa Rais wa Marekani kwa kufuata ndoto za Baba yake ikiwemo ndoto ya matamanio pale nae alipotembelea Ikulu ya Marekani miaka ya 1980s.Hizo dreamz ukiziweka huru ndio ukamilifu ambao wanao watanzania wachache.Wababaishaji watu wasiojiamini hawawezi kusema hisia na ndipo unafiki unapochukua sura yake.Na wana siasa wengi ndani ya Taifa letu sio wasema hisia zao,kwa kuwa kusema kwao hisia zao nikujionyesha kuwa wanamapungufu,na kumbe mapungufu ndio ukamlifu kama viumbe wenye uhai.

Mjengwa umetushirikisha na nimependa kuwa umeonyesha furaha ambayo baba yako angekuwa hai,yeye kama yeye binafsi angejiskia.Duniani watu wawili Baba na Mama wakifurahi jambo ulilolipenda kuwapendeza wao machoni na mioyoni mwao ni nani tena hapa duniani watazidisha furaha zaidi yao kama si watoto wako nao watakapokutendea wewe kama ulivyowatendea wao wazazi wako.

Big Up Mjengwa ulivyojisikia kwa kutwambia kwa sie baadhi tunao feel hakika umemtendea invyostahiki believe he is Happy Mzee Mjengwa[R.I.P]!!!Achana na watu nusu, nyota ndogo anawaita viatu!!!!
 
Mjengwa hapa umeelezea furaha yako lkn sio kile ulichoelezea its pity kuelezea your private ktk Natioanal Dialogue of Next 50 years Is not about you! Maggid is about Tanzanian Sorry kuteleza~!
wewe ndo umeamua kuandika nini? au ndo U-GT?.........aisee, can't you share your achievement, memories and fun to your fellows?............read between lines GT
 
Tuache chuki tu,Maggid ni binadamu mwenye yake ya moyoni kutokana na historia yake.Si vibaya akitushirikisha kama Wanajamii wenzake.Alichonifurahisha hajajikweza bali kaonesha heshima kwa nafasi aliyopewa.

Hongera Maggid,unapotimiza ndoto fulani maishani ni mafanikio makubwa na naamini wapo wengi tu humu wanaotamani nao siku moja kualikwa kwenye kongamano kama hilo tena mbele ya wanazuoni kumwaga nyanga.

Hongera sana.
 
Kwa wale tuliokuwepo tuliona ulikuwa wa kawaida 2 na mimi sikushangaa kumwona maggid mjengwa kuwa ni mmoja wa waalikwa kwenye kongamano kama hilo.Cha kushangaza ni jinsi ulivyojiexpress hapa kuwa umelichukulia hilo tukio kama vile hukustahili! Nakushangaa majjid kwa sababu wewe una media attention.Je tungekuwa akina sisi ambao jf na mitandao mingine ya kijamii ndo inayotutambia ingekuwaje kwa mtazamamo wako? Mi nadhani kongamano hilo yeyote anayejua kuongea angeweza kuwa msemaji kwa sababu watanzania wote tuko sawa tu na wala usichukulie kwamba kilikuwa ki2 pecurior saaana



Ww unafikiri kwa nn hukualikwa kupresent?tuache wivu wa kijinga he made his day mkubwa acha afurahie ni wakati wake.

Big up brother Maggid

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom