Nkasi, Rukwa: Takribani Risasi 1500 zakamatwa baada ya wavuvi kuzivua Ziwa Tanganika


Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Peter Lijualikali amekamata risasi zaidi ya 1500 ambazo zimevuliwa na wavuvi wa kijiji Cha korongwe kata ya korongwe wilayani humo. Lijualikali amesema tayari kamati ya ulinzi na usalama inafanyia kazi swala hilo ili kutambua nani aliziweka risasi hizo katika ziwa hilo.

Akieleza kwa kina kuhusu tukio hilo, DC Lijualikali amesema:

Siku ya jana tarehe 8 mwezi wa 9 2021, nilipokea simu majira ya asubuhi saa mbili kutoka kwa mtu ninayemfahamu kwa jina la Mzee Gabile anayeishi kata ya Korongwe, Kijiji cha Korongwe wilayani Nkasi. Akinieleza kwamba kuna taarifa za wavuvi ambao yeye amekuwa akishirikiana nao katika utafiti wa madini katika mwambao wa Ziwa Tanganyika upande wa Korongwe, kwamba wamepata kiboksi ambacho baada ya kukifungua wakakuta kuna risasi lakini hawakuendelea kukifungua zaidi maana waliogopa.

Kwahivyo wakanijulisha ili niweze kuwajulisha wakuu wa vyombo vya usalama ili tuweze kwenda kuvichukua hivyo vitu. Nilikwenda mpaka eneo la tukio, nyumbani kwakwe nikakuta kweli kuna risasi 739 zikiwa nyumbani kwake akiwa amezifunga kwenye kiboksi, amezihifadhi. Lakini baadaye kuna zingine alimtuma kijana wake kwenda kuzichukua kwa wavuvi wengine ambao waliondoka na kiboksi kingine – jumla viboksi vilikuwa viwili.

Kwahiyo akawa amemtuma kijana wake kwenda kuchukua hicho kiboksi kingine. Ingawa kwa maelezo yake anadai kuwa yule aliyechukuwa anajua ile ni mali hivyo anahitaji fedha ili aweze kukiachia hicho kiboksi. Na yeye akatafuta hizo fedha akamtuma kijana wake aende kuzikomboa – kukomboa hicho kiboksi chenye hizo mali. Wao walikuwa wanahisi ni mali, hao wavuvi wengine. Hawakujua kuwa zile ni risasi, kwa mujibu wake.

Risasi za SMG na silaha nyingine kubwa. Kwahiyo pia tukaenda kwa huyo mvuvi mwingine na kwa bahati nzuri tukakuta tayari askari walishamweka chini ya ulinzi ili kuunganisha na zile zingene alizokuwa nazo Mzee Gabile.

Kwahiyo, kwa kifupi, tukafika pale tukamkuta yeye anazo 750. Kwahiyo tukazichukua zote kwa mujibu wa taratibu na baadaye tukafunga safari tukiongozwa na yule mvuvi aliyeziokota kwa mara ya kwanza ziwani.

Tukaingia ziwani kwa takribani masaa mawili kwenda kwenye huo mwamba ambapo walizikuta. Kwahiyo tukafika lakini hatukubahatika kupata chochote. Lakini baadaye mimi nikaviachia vyombo vaya ulinzi na usalama viendelee na utaratibu wa kiuchunguzi na upelelezi ili kubaini kama kuna makossa ya jinai katika hili jambo kwa hao wavuvi.

Lakini nichukue fursa kutoa wito kwa wananchi wote wa Nkasi au wanaoishi katika mwambao wa Ziwa Tanganyika kwamba wakiona kitu chochote ambacho si cha kawaida wasikimbile kukifungua na wazitaarifu mamlaka ili mamlaka ziweze kufanya utafiti kujua hicho ni kitu gani; kwasababu mwambao wetu unapakana nan chi za Congo ambapo kuna hali tete ya kiusalama. Kwahiyo, inawezekana vitu vikatoka Congo au maeneo mengine ambayo yana machafuko vikaingia kwetu.


========

Kama inavyoonekana hapo

Maswali ya kujiuliza hizi risasi zilitoka wapi?

Zilikuwa ziende wapi?

Nini hatima ya usalama wa Tanzania?

Mwisho hivi kumbe Lijualikali ni mkuu wa wilaya tena ya pembezoni?
Hakuzikamata yeye ila alikabidhiwa na wavuvi waliozivua ziwani.
 
Ndani ya Chadema wako kibao wazalendo ukipanga chochote kibaya wana ripoti serikalini

Ndio maana ya Chama tawala kinatawala vyama Vyote na kina watu huko

Panga chochote kibaya uone mziki wake utaamkia shikamoo serikali
Acha mzaha. CHADEMA mliishainyonga zamani. Haina hata mbunge wa maana wala haifanyi shughuli yoyote ya maana mitaani. Mwenyekiti wake mnasubiri kumnyonga. Hamza, kada wa CCM, ndiye aliyeua polisi wenu. Mziki wake mnaujua. Wao ndio walimwamkia shikamoo - mwanachama mwenzao. Mziki wa serikali ya JMT ni mbele ya raia wasio na silaha tu. Mbele ya magaidi wa ukweli ni mchecheto tu. Uliza habari za Mtwara.

Hofu kwa CHADEMA ya nini?; Mbowe gaidi? What a shame! Real embarrassment! Mnamkamata mtu kitandani usiku wa manane halafu mnajinasibu kumkamata gaidi? Mtu ambaye majuzi Rais wenu alimtumia salamu za rambirambi? Au mnaogopa wananchi?

Ongeeni na Lipumba na Zitto na timu za kimafia ndani ya CCM. Labda mtapata amani ya roho huko.

Amin nakuambia, siku CHADEMA ikitoweka ndipo utakapoielewa kauli ya Mwalimu JKN kuhusu watu waliozoea kula nyama ya binadamu. Inasikitisha kuona civility imepotea kabisa nchini; umebakia ushenzi tu. Polisi na CCM wanajinasibu kuvunja miguu raia wasio na silaha! Huo ndio mziki wao. Eti andamaneni tuwaone kama hamjawa vilema! Binti anatunguliwa risasi ndani ya dala dala, halafu washenzi wanakuja JF kuwasifu polisi kwa ukakamavu!?
 
Ndani ya Chadema wako kibao wazalendo ukipanga chochote kibaya wana ripoti serikalini

Ndio maana ya Chama tawala kinatawala vyama Vyote na kina watu huko

Panga chochote kibaya uone mziki wake utaamkia shikamoo serikali

Hamza unamjua?
 
Why unamweka chini ya ulinzi mtu aliyeokota kitu? Ndo maana watu huwa hawataki kuripoti matukio mbalimbali polisi kuepuka kuwekwa ndani
 
Mikoa hiyo si Jambo geni isitoshe hapo Ni karibu na ziwa Tanganyika..mzigo umetoka Congo au Burundi..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Thanks means ni ukanda uanahohitaji ulinzi/surveillance madhubuti maana ni hatari sana kwa usalama wa raia iwapo zingeangukia kwa maharamia.
 
Back
Top Bottom