Nkasi, Rukwa: Takribani Risasi 1500 zakamatwa baada ya wavuvi kuzivua Ziwa Tanganika

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
6,276
12,335
tempsnip i.png

Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Peter Lijualikali amekamata risasi zaidi ya 1500 ambazo zimevuliwa na wavuvi wa kijiji Cha korongwe kata ya korongwe wilayani humo. Lijualikali amesema tayari kamati ya ulinzi na usalama inafanyia kazi swala hilo ili kutambua nani aliziweka risasi hizo katika ziwa hilo.

Akieleza kwa kina kuhusu tukio hilo, DC Lijualikali amesema:

Siku ya jana tarehe 8 mwezi wa 9 2021, nilipokea simu majira ya asubuhi saa mbili kutoka kwa mtu ninayemfahamu kwa jina la Mzee Gabile anayeishi kata ya Korongwe, Kijiji cha Korongwe wilayani Nkasi. Akinieleza kwamba kuna taarifa za wavuvi ambao yeye amekuwa akishirikiana nao katika utafiti wa madini katika mwambao wa Ziwa Tanganyika upande wa Korongwe, kwamba wamepata kiboksi ambacho baada ya kukifungua wakakuta kuna risasi lakini hawakuendelea kukifungua zaidi maana waliogopa.

Kwahivyo wakanijulisha ili niweze kuwajulisha wakuu wa vyombo vya usalama ili tuweze kwenda kuvichukua hivyo vitu. Nilikwenda mpaka eneo la tukio, nyumbani kwakwe nikakuta kweli kuna risasi 739 zikiwa nyumbani kwake akiwa amezifunga kwenye kiboksi, amezihifadhi. Lakini baadaye kuna zingine alimtuma kijana wake kwenda kuzichukua kwa wavuvi wengine ambao waliondoka na kiboksi kingine – jumla viboksi vilikuwa viwili.

Kwahiyo akawa amemtuma kijana wake kwenda kuchukua hicho kiboksi kingine. Ingawa kwa maelezo yake anadai kuwa yule aliyechukuwa anajua ile ni mali hivyo anahitaji fedha ili aweze kukiachia hicho kiboksi. Na yeye akatafuta hizo fedha akamtuma kijana wake aende kuzikomboa – kukomboa hicho kiboksi chenye hizo mali. Wao walikuwa wanahisi ni mali, hao wavuvi wengine. Hawakujua kuwa zile ni risasi, kwa mujibu wake.

Risasi za SMG na silaha nyingine kubwa. Kwahiyo pia tukaenda kwa huyo mvuvi mwingine na kwa bahati nzuri tukakuta tayari askari walishamweka chini ya ulinzi ili kuunganisha na zile zingene alizokuwa nazo Mzee Gabile.

Kwahiyo, kwa kifupi, tukafika pale tukamkuta yeye anazo 750. Kwahiyo tukazichukua zote kwa mujibu wa taratibu na baadaye tukafunga safari tukiongozwa na yule mvuvi aliyeziokota kwa mara ya kwanza ziwani.

Tukaingia ziwani kwa takribani masaa mawili kwenda kwenye huo mwamba ambapo walizikuta. Kwahiyo tukafika lakini hatukubahatika kupata chochote. Lakini baadaye mimi nikaviachia vyombo vaya ulinzi na usalama viendelee na utaratibu wa kiuchunguzi na upelelezi ili kubaini kama kuna makossa ya jinai katika hili jambo kwa hao wavuvi.

Lakini nichukue fursa kutoa wito kwa wananchi wote wa Nkasi au wanaoishi katika mwambao wa Ziwa Tanganyika kwamba wakiona kitu chochote ambacho si cha kawaida wasikimbile kukifungua na wazitaarifu mamlaka ili mamlaka ziweze kufanya utafiti kujua hicho ni kitu gani; kwasababu mwambao wetu unapakana nan chi za Congo ambapo kuna hali tete ya kiusalama. Kwahiyo, inawezekana vitu vikatoka Congo au maeneo mengine ambayo yana machafuko vikaingia kwetu.

========

Kama inavyoonekana hapo

Maswali ya kujiuliza hizi risasi zilitoka wapi?

Zilikuwa ziende wapi?

Nini hatima ya usalama wa Tanzania?

Mwisho hivi kumbe Lijualikali ni mkuu wa wilaya tena ya pembezoni?
 
Wana bahati, hizo zingekutana na moto ingekuwa habari nyingine saa hizi.
 
Hongera Lijuakali

Chadema mngepanga Mipango ya kuhujumu nchi lazima Lijuakali angeripoti vyombo vya usalama

Muwe Wapole mkiambiwa Mbowe gaidi msikurupuke kupinga

Ndani ya Chadema wako kibao wazalendo
 
Ndani ya Chadema wako kibao wazalendo ukipanga chochote kibaya wana ripoti serikalini

Ndio maana ya Chama tawala kinatawala vyama Vyote na kina watu huko

Panga chochote kibaya uone mziki wake utaamkia shikamoo serikali
 
Movie hii
 
Huyu ni mwanachama wa chama gani ?
IMG-20210825-WA0072.jpg
IMG-20210827-WA0010.jpg
 
Hongera Lijuakali

Chadema mngepanga Mipango ya kuhujumu nchi lazima Lijuakali angeripoti vyombo vya usalama

Muwe Wapole mkiambiwa Mbowe gaidi msikurupuke kupinga

Ndani ya Chadema wako kibao wazalendo
Sikuwahi kukifikiria kuwa una uwezo mdogo hivi lakini Leo nakufikiria hivyo kwani unamhukumu mtu aliyetuhimiwa pasi na kuwa na ushahidi! Uliwahi kujitanabaisha humu kuwa wewe ni msomi japo siijui level ya usomi wako. Kwa usomi wako, unadhani kwanini pilato hakumhukumu Yesu japo alikuwa na mamlaka yote? Wewe unapata wapi mamlaka ya mahakama kumhukumu?Nai Kama unajilaumu Kwa uchaguzi mbaya wa carrier unayoitumikia!
 
Back
Top Bottom