Nkasi, Rukwa: Mwanamke Mjamzito auawa kwa kuliwa na Mamba akioga Ziwa Tanganyika

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Mkazi wa Kijiji cha Msamba, Kata ya Ninde, wilayani hapa Magreth Ndasi (18), ameuawa kwa kuliwa na mamba wakati akiogelea katika Ziwa Tanganyika.

Akizungumzia tukio hilo, kaka wa marehemu Joseph Ndasi, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita (Julai 27) majira ya saa 12:30 jioni baada ya Magreth aliyekuwa pia ni mjamzito kwenda kuoga katika ziwa hilo.

Alisema alipofika katika ziwa hilo aliingia ndani ya maji na kuanza kuoga ndipo alipovamiwa na mamba huyo ambaye alimkamata mguu na kuondoka naye kuelekea katika kina kirefu cha maji.

“Wakati alipokuwa anavutwa na mamba huyo alipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo walipojitokeza wananchi kutaka kumsaidia,” alisema.

Alisema baada ya mamba huyo kuona kundi la watu likiwa linaingia ndani ya maji, alimzamisha Magreth na kumkalia juu huku akifoka kuwatisha watu waliokwenda kumuokoa.

Aidha, wananchi walioshuhudia tukio hilo, walisema watu wenye silaha za jadi walipofika karibu na mamba huyo ili kumshambulia, alimwachia mwanamke huyo ambaye tayari alikuwa ameshakufa na kukimbia.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuacha kwenda kuogelea ziwani hasa nyakati za jioni.
 
Kwanza natoa pole kwa wahusika wote wa huu msiba.

Alikwenda kuoga ama kuogelea? Tatizo la maji Rukwa lilipotokea tukio ni kubwa kiasi gani?
 
Huduma za jamii maji safi na salama ni muhimu. Marehemu angekuwa na maji ya bomba karibu na nyumbani kwake asingekwenda kuoga ziwani.

Dreamliner, Chato International Airpot havijuwa kipaumbele kama huduma za jamii.
 
Last edited:
Huduma za jamii maji safi ni salama ni muhimu. Marehemu angekuwa na maji ya bomba karibu na nyumbani kwake asingekwenda kuoga ziwani.

Dreamliner, Chato International Airpot havijuwa kipaumbele kama huduma za jamii.
Watakao kuelewa si wale wa Lumumba. Waliojitoa ufahamu siku nyingi hawatakuelewa ndo maana hata teuzi hawapati kwasababu ya akili ndogo
 
Rekebisha kichwa cha habari.
Maana umeandika ameliwa na stori inaonyesha mamba alimuachia na kukimbia
 
Back
Top Bottom