Njugu mawe za sukari

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
NJUGU MAWE ZA SUKARI.jpg

MAHITAJI
1.Njugu mawe robo kilo
2.Nazi 1
3.Hiliki punje 10
4.Sukari vijiko vya chakula 5
5.Custard kijiko cha chakula kimoja
6.Arki (Vanilla)kijiko cha chai 1
7.Chumvi kiduchu

MAANDALIZI
1.Chagua njugu mawe zako toa mawe yote
2.Weka kwenye chombo na uzikoshe vizuri
3.Kuna nazi na chuja nazi tui zito kikombe kikombe kidogo cha chai na kisha lilobakia chuja kibakuli
kimoja tui jepesi
4.Menya na kutwanga na sukari kiduchu hiliki yako
5.Weka custard kwenye tui lako zito kisha weka pembeni

JINSI YA KUPIKA
1.Weka njugu zako kwenye sufuria na maji kiasi
2.Chemsha njugu zako maji yakikauka weka maji kidogo kidogo ili njugu zako ziwive vizuri
3.Njugu zikiwiva mimina tui jepesi,hiliki,sukari na chumvi
4.Acha tui lipungue kisha mimina lile tui zito na arki
5.Acha lichemke kidogo na ikiwa nzito nzito epua
6.Unaweza kula na Chapati,Mkate wa ufuta,Boflo au mkate wowote
Angalizo:
1.Wakati wa kuchemsha njugu usiweke maji mengi ili zisivurugike na kubanduka maganda na kupelekea kuto kuiva
2.Usiweke custard nyingi inasababisha kuwa nzito zaidi na kupoteza ladha yake
3.Hakikisha hauweki tui jingi jepesi ili ziwe nzito na tamu
4.Usikoroge upishi wako mpaka una maliza kama ukitaka kuchanganya chukua banio la ugali ushikie sufuria yako kisha itikise au tumia kitambaa kisafi cha jikoni ushikie sufuria yako kisha itikise

Furahia Njugu Mawe Zako.
 
Nilikuwa sijawahi kuila, nilienda sokoni last month nikanunua kilo 1, nikawauliza jinsi ya kuipika, nikaja Facebook nako nikaulizia kwenye magroup ya mapishi, sijaregrett kutaka kujifunza na kujua, tamu balaa.
 
Haya madude siyapendi kuliko chakula chochote hapa duniani. Hasa ile harufu yake ndio mbaya balaa.
 
Hiki chakula ni kitamu sana lakini sharti lake ni kwamba wakati wa kula usiwe na stress na nafsi iwe imeridhika kimaisha,bila ya hivyo huwezi ona radha yake na utahisi kama unakula mbegu za ndimu
 
View attachment 360438

MAHITAJI
1.Njugu mawe robo kilo
2.Nazi 1
3.Hiliki punje 10
4.Sukari vijiko vya chakula 5
5.Custard kijiko cha chakula kimoja
6.Arki (Vanilla)kijiko cha chai 1
7.Chumvi kiduchu

MAANDALIZI
1.Chagua njugu mawe zako toa mawe yote
2.Weka kwenye chombo na uzikoshe vizuri
3.Kuna nazi na chuja nazi tui zito kikombe kikombe kidogo cha chai na kisha lilobakia chuja kibakuli
kimoja tui jepesi
4.Menya na kutwanga na sukari kiduchu hiliki yako
5.Weka custard kwenye tui lako zito kisha weka pembeni

JINSI YA KUPIKA
1.Weka njugu zako kwenye sufuria na maji kiasi
2.Chemsha njugu zako maji yakikauka weka maji kidogo kidogo ili njugu zako ziwive vizuri
3.Njugu zikiwiva mimina tui jepesi,hiliki,sukari na chumvi
4.Acha tui lipungue kisha mimina lile tui zito na arki
5.Acha lichemke kidogo na ikiwa nzito nzito epua
6.Unaweza kula na Chapati,Mkate wa ufuta,Boflo au mkate wowote
Angalizo:
1.Wakati wa kuchemsha njugu usiweke maji mengi ili zisivurugike na kubanduka maganda na kupelekea kuto kuiva
2.Usiweke custard nyingi inasababisha kuwa nzito zaidi na kupoteza ladha yake
3.Hakikisha hauweki tui jingi jepesi ili ziwe nzito na tamu
4.Usikoroge upishi wako mpaka una maliza kama ukitaka kuchanganya chukua banio la ugali ushikie sufuria yako kisha itikise au tumia kitambaa kisafi cha jikoni ushikie sufuria yako kisha itikise

Furahia Njugu Mawe Zako.
zinachukua mda gani kuiva...au kama maharage
 
MziziMkavu asante sana kwa hii makitu. Napigaga sana hii makitu kila wiki lazima nigonge hivi vyombo.
Leo nimeona kitu cja tofauti kidogo kwenye mapishi yako. Yaani madiko diko nyongeza uliyoongeza. Mi huwa nawaambia wapike na nazi tu kitaa.
Sasa hivi Hiliki punje 10, sukari vijiko vya chakula 5, Custard kijiko cha chakula kimoja, Arki (Vanilla) kijiko cha chai 1 ndo umeniacha hoi hapa.
Hizi bidhaa ulizoongeza hapa zina faida gani mwilini labda unisaidie nielewe ili nianze matumizi.
Asiyependa njugu mawe anakosa uhondo duniani.
 
Nadhani hizo ni kwa ajili ya flavour
 
Ila ukimaliza kula usikae Jirani na watu watakukimbia si kuachia Ishuzi ukila hiyo kitu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom