Njozi tamu Afrika

Malima pamba

New Member
Jul 14, 2021
1
0
NJOZI TAMU YA AFRIKA
Afrika bara langu nilipendalo sana zaidi ya mabara yote saba yaliyopo katika ulimwengu huu dunia, ukitazama katika ramani ya dunia upande wa katikati utaliona bara zuri na lenye kuvutia sana hapo nazungumzia Afrika. Bara zuri lenye watu wenye ngozi nyeusi na yenye kupendeza.

Bara hili la Afrika linakadiliwa kuwa na watu zaidi ya bilioni 1.3 (sensa 2018) kutoka mataifa 54 tofauti yanayounda bara zuri la Afrika, hii ni kutokana na taarifa kutoka umoja wa mataifa.

Afrika ni mojawapo ya mabara yanayosumbuliwa na matatizo mbalimbali Kama elimu duni, magonjwa, njaa na matatizo mengi sana lakini ipo njozi nzuri na tamu kuhusu bara hili zuri la Afrika na ifuatayo ni njozi yenye kuleta matumaini na mwangaza katika bara letu hili la Afrika.

Shida na mahangaiko bado vipo Afrika,
Vita, ukame na magonjwa bado ni changamoto
Imani yetu kuna siku hivi vyote vitaondoka
Hii ndiyo njozi yangu tamu ya Afrika

Agenda 21 kwa lengo la kuondoa umaskini
Lakini bado kuna umaskini sudani ya kusini
Ipo siku umaskini huu utaisha sudani ya kusini
Hii ndiyo njozi yangu tamu ya Afrika

Macho yangu yameona njozi nzuri kwa siku zijazo
Amani itarejea katika nchi ya demokrasia ya Kongo
Utapiamlo kwa watoto utapungua na kuondoka kabisa
Hii ndiyo njozi yangu tamu ya Afrika

Upatikanaji wa elimu yenye viwango Limpopo-Afrika kusini
Uwepo wa miundombinu mizuri nchini Uganda
Kutokuwepo na migogoro tena Zimbabwe
Hii ndiyo njozi yangu tamu ya Afrika


Ebora haitokuwepo tena nchini Kongo
Kutokomezwa kwa ugaidi nchini Nigeria
Rushwa haitakuwepo tena Tanzania
Hii ndiyo njozi yangu tamu ya Afrikaa.

Uwekezaji mkubwa wa viwango nchini Malawi
Uwepo wa ajira nyingi nchini Eritrea
Miundombinu bora na imara Uganda
Hii ndiyo njozi yangu tamu ya Afrika.

Kutokomea kwa njaa kabisa Afrika ya Kati
Kutokuwepo kwa vita vya kidini Somalia
Hakutakuwa na maumivu tena Afrika
Hii ndiyo njozi yangu tamu ya Afrika.

Haijalishi itachukuwa mda gani njozi hii kutimia
Lakini njozi hii tamu ni lazima itimie
Tuungane kwa pamoja Kama waafrika ili njozi hii itimie
Hii ndiyo njozi yangu tamu ya Afrika.

HITIMISHO
Sisi kama waafrika bado tunayo nafasi ya kuungana kwa Pamoja na kuondoa tofauti zetu ili njozi hii nzuri na yenye kuvutia iweze kutimia,Hatuwezi kufikia njozi hii iwapo tofauti zetu zitaendelea kuwepo. AMKA AFRIKA NI MUDA WA MABADILIKO.
 
Back
Top Bottom