Njooni tukumbuke nyakati ngumu tulizowahi pitia

In summary...

Mshua na Mama walizinguana.
Mshua akasepa.
Mama alipatwa na redubdancy nikiwa F2.
Maisha yakaChange.
Mlo m1 ilikuwa issue.
As an older boy nlipaswa kwenda shule. Nikitoka naingia Mtaani kuHustle ili Mother na wadogo zangu wawili wapate cha kuingiza Mdomoni.
Umbali wa shule na Home ilikuwa 7km. No daladala by then.
Sikuwa kuipenda Jumatatu - Ijumaa asilani.
Nilizipenda weekend tu.

Maza aliumwa.
Ndugu zake wakala buyu.
Jukumu la kumuuguza mama likabaki kwangu.
Maza aliumwa kiasi kila kitu anafanya hapo hapo.
Nlikuwa Nampikia. Namnywesha. Namuogesha. Naenda mtoni kumfulia. Imagine Mtoto wa Kiume wa F2 kufanya haya...
Daaah....

Kabla kumaliza Secondary, Maza akadondoka.
Acheni kabisa.
Street bro m1 alikuwa ananisaidia hela ndogo ndogo coz alikuwa anaijua familia yetu.
Kumbe PUSHA.
Nikaanza kuuza MZIGO.
Nikaanza kupata pesa.
Shule sikuona tena km ina umuhimu.
Japo sikuacha.
Ulifanikiwa kutusua?
 
Lecturer aliniwekea nia nifeli kwa namna yoyote ile semester ya kwanza akanipa F somo lake, nilipo appeal nikapata A hapo hasira zake ziliongezeka mara 2 zaidi.

Semester ya pili akapangiwa kutufundisha tena kufundisha darasani, dah nilikosa furaha na amani kabisa nikijua tayari nimekwisha.

Asante Mungu, nilimaliza salama
 
Mapito ya mtu toka udogo mpaka ukubwa huwa Ni mengi sana, iwe wa kishua ama wa kikwetu.

Kila mmoja ana magumu yake.
Langu moja wapo la kale kidogo, nilikulia mazingira ambayo usipoenda kanisani jumapili Ni Kama kosa kubwa sana, hivyo nilazima kwenda. Na pia ilikua Ni lazima kwenda ibada za watoto au ya pili kwa kule kwetu haswa walio katika ngazi ya mafundisho.

Nilikua na nguo moja tuu ya kanisani karibu miaka 3, aibu nilio kua napata sio ya nchi hii, kuchekwa kulipozidi ilinifanya nisiwe napita barabarani wakati wa kwenda kanisani ama kutoka.
Nilikua nakatiza kwenye migomba ya watu huko uchagan mpaka kufika parokian sio safari fupi, mradi tu niingie kanisani. Nakisha kutoka nakatiza shamba kwa shamba mpaka nyumbani, bahati mbaya sana nilikua naishi na bibi ambae alikua kua kipofu so hakujua ninavaaje ama nikoje.

Hii ilinipelekea kujitenga na kutengwa ambayo mpaka Leo hivi imeniathiri kwa kweli, sio mtu wa kujichanganya kabisa yaani.
Pole sana mkuu. Mimi nikiwa mdogo pia niliwahi kupitia changamoto nyingi sana za maisha ya umasikini katika mavazi mpaka nikaachana na kwenda kanisani, sema tu ninakwepa sana kuzikumbuka kwa maana nafsi yangu itaniuma tena.

Nilijipa jina hili la INFANTRY SOLDIER kwa sababu ya maisha ya umasikini na shida nilizozipitia ila mimi sio mwanajeshi. Hakika Mungu ni mwema.
 
Mkuu, vp wale akina mama wanaowatupa watoto wao chooni, nao pia unamuomba Mungu awape wepesi?
Naam, maisha ya wakina mama ndugu yangu sio mepesi kabisa, kile kinachompelekea mpaka kufika hatua hio naamini kabisa ni nje ya jaliwa la Mungu.

Na ninaamini mama wa namna hio huwa anapitia wakati mgumu sana tena sana kabla ya kufanya maamuzi hayo ambayo huongozwa mpaka kufanikiwa na roho ilio nje ya mwanamke alieumbwa na Mungu.
 
Pole sana mkuu. Mimi nikiwa mdogo pia niliwahi kupitia changamoto nyingi sana za maisha ya umasikini katika mavazi mpaka nikaachana na kwenda kanisani, sema tu ninakwepa sana kuzikumbuka kwa maana nafsi yangu itaniuma tena.

Nilijipa jina hili la INFANTRY SOLDIER kwa sababu ya maisha ya umasikini na shida nilizozipitia. Hakika Mungu ni mwema.
Hongera mkuu kwa kuvuka, nyakati za namna hio hata Kama zitadumu namna gani wakati fulani hazitakuwepo.
 
Back
Top Bottom