Njooni Mbomoe na Huku kwetu, mkituacha mnatuogopa.

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Mi nimeamua kuwaita maana inaonekana wamesahau kuja kutubomolea nyumba za huku kwetu. Sisi tunaishi bondeni tupo miaka mingi sana zaidi ya 20. ina maana serikali haikutuona? Na umeme ilituletea. Nkakumbuka hata Rasi aliwah kuja kututembelea huku msanii fulani alipofariki. Je, ina maana rais alikosea? Alikujaje wakati sis tunaishi maeneo yasiyo halali?

Njooni mbomoe bwana....mnatuacha muda mrefu tupo huko na mafuriko yanaweza kuja. Au mnataka mafuriko ndo yaje kutuondoa? Mnataka mafuriko ndo yaje kutubomolea nyumba? Acheni ubahili wa kutumia pesa zetu kuwabomolea wengine na wakati sisi mnatuacha. Njooni mtubomolee hata kama hamna mafuta sisi tutachangia pesa za kuwekea mafuta kwenye gari zenu.

Sisi huku mvua ikinyesha hatulali usiku kucha tunawaza je kutakucha tukiwa salama. Tunasali na kumwomba Mungu, viwanja vyetu vipo kwenye mkondo wa maji kabisa. Ndiyo vipo kwenye mkondo wa maji nasi ndo tulifanikiwa kupata uwanja hapo maana huko sehemu za kwenu bei yake hatukuiweza na hatuwezi mpaka sasa.

Mnataka tukaishi nje ya jiji la Dar hivi mnatutakia mema kweli? Ninyi ofisini zenu mnazidi kufungua kati kati ya jiji la Dar maji mnapeleka huko kwenu sisi mnatusukumia pembezon mwa jiji. Hatuhami, acha mvua na mafuriko yaje. I9la tumegoma kuhama maana hii sasa inakuwa ni manyanyaso kwenye nchi yetu wenyewe.

Kama tunagoma kuhama kwani tukifa ninyi inawahusu nini. Mbona kila siku tunakufa kwa kukosa madawa hospitali na ajali zinazozuilika? Kwani tunakufa wangapi kwa siku wakati akina mama wakijifungua? Aaahh tuacheni bwana. Tuacheni tuishi tunavyotaka wenyewe. Kwanza haya maisha yenyewe hamkuta sisi. kama mnatujal boresheni huduma za hospital basi. Okoneni maisha ya maskini sisi. Okoeni maisha ya albino.

Ila tuacheni tuishi mabondeni. Tumekuja kuishi huku kwa sababu huko milimani hatupati maji, hali ya huko miliman ni ngumu sana kwetu sisi. Huku mabondeni maji ni mengi sana. Mpaka tunamwaga. sasa mnataka tukaishi wapi?

Kama mnataka kuja kubomoa njooni tu mbomoe wala msiogope. Na kama hamna bajeti ya pesa za kubomolea sisi wenyewe tumeamua kuchangishana mje kutubomolea nyumba zetu.

Nasikia kuna masika inakuja. Tafadhirini muwahi kuja kabla ya mafuriko kuja.Mkiacha kuja kubomoa mtakuwa mnatuogopa.
 
Last edited by a moderator:
Kumbe ulipewa ja kiwanja haukuhama sababu mbali. Basi wasubiri maana lazima na kiwanja mlivyopewa mliviuza.

Hawaonei mtu wanawatakia mema.
 
Ha ha ha unaleta mashairi kwenye kazi?
huyu si kwamba anamaanisha alichokiandika nadhani ni kufikisha ujumbe kwa ofisi husika juu ya hii bomoabomoa walikuwa wapi wakati watu wanajenga na viwanja walipewa na nani , tuseme kwamba serikali haikuwepo kipindi hicho na ama haikujua kwamba watu wanajenga mabondeni. Maswali mengi sana ambayo mtu unaweza kujiuliza kuhusu zoezi hili linaloendelea kwa sasa
 
Mimi nawaomba wakabomoe na Oysterbay. Waliuziana nyumba za serikali kwa masharti wasiuze wala kuzibadili kwa miaka 25! Sasa hivvi zipo zilizojengwa ghorofa mpaka tano kwenda juu,kuna nyingine zimejengwa nyumba zaidi ya tano kiwanja kimoja. Wakaanze na hizo.

Kuna nyumba kibao zipo Masaki kwenye viwanja vya wazi,wanazimiliki wenyewe....wakavunje na hizo sio kuvunja za masikini tu bondeni. Sheria si msumeno wafuate sheria.

Siku wakivunja nyumba za bondeni nitakuja kuorodhesha nyumba zote zilizojengwa kwenye open space Masaki, na nitaorodhesha nyumba zote walizokiuka taratibu za ujenzi na makubaliano walipouziana, halafu wakabomoe hizo....kwa akili ya kawaida Masaki kunaweza kukosa playground,sokono,shule??? Ni kwamba kote wamejenga!!!
 
Kama ni wanaume kweli Lukuvi na genge lake aende akabomoe hotel ya Ladwa aliyojenga pale ufukweni Oysterbay kinyume na masharti ya ujengaji ufukweni!! Lukuvi pia aeleze sababu zilizopelekea kumpa Ladwa hati nyingine ufukweni karibu na hotel hiyo. Magufuli amebugi kumpa huyu jangili uwaziri!!
 
Mwandishi we ni hatari

Back
Top Bottom