Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,230
- 6,469
Habari wadau wa JF Siasa, niende kwenye mada hapo juu.
Itakumbukwa tarehe 7/7/1954 kuna Wajumbe 17 wanaokumbukwa katika historia kwenye kuchangia pakubwa kuanzishwa Chama cha TANU.
Miongoni mwao ni Julius Kambarage Nyerere, Tewa Said Tewa, Oscar Kambona, Saadan Kandoro, Aby Sykes, John Rupia nk.
Kiini cha swali: Wameacha nasaba zao katika siasa?
- Naanza na Nyerere, amemuacha Makongoro Nyerere.
- Abby Sykes amemuacha Abdul Sykes aliyekuja kuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam baadae.
- Saadani Kandoro mtoto wake alikuja kuwa Mkuu wa Mkoa Dar, Arusha, Mwanza na Mbeya.
Kumbuka wengine historia ya Tanganyika na Tanzania ilikuja kuwachukia na kutotaka chochote kizuri kiandikwe juu yao.
Na wewe tiririka kuhusu wengine hata kama waliacha alama kama watoto, wajukuu au hata vilembwe katika siasa za kitaifa.
Karibuni.