Njooni hapa mliowahi kulipwa fidia baada ya ajali

fatherhood

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
530
551
Huu ni uzi wangu wa pili kuhusu kulipwa fidia, hii ni kwa sababu watu wengi kila siku wanapata ajari na wakifatilia fidia wanaishia kati kutokana na hatua nyingi au wengine kupotezea kutokana hawajui waazie wapi.

Mi ya kwangu ni hivi nilipata ajar mwezi wa kumi, sasa kuna ndugu yangu anafatilia ila ameambiwa kesi ipo mahakaman hii inamaana kama mambo ya fidia baada ya maamuzi ya mahakama bado tupo kwenye hatua ya kusubiri.

Sasa kama wewe ulishawahi kupata ajari na ukalipwa fidia njoo utupe experience yako ya kufatilia kesi za fidia , kwa kutuambia process zote ulizopitia hadi kupata fidia yako.

Hii sio lazima uwe uliwahi pata ajari lakini pia kwa yetote anayejua jinsi ya kufatilia fidia.

Karibuni sana.

20211106_153823.jpg
20211013_072627.jpg
 
pole mkuu, kama wewe/ndugu anaefuatilia hampo vizuri kipesa mtazungushwa sana hadi kesi mtaiona chungu.
 
Hifadhi risiti za matibabu na gharama nyingine zote bila kusahau tiketi uliyokata siku ajali ilipotokea. Hakikisha vyote vina majina yako halisi.

Nenda kaidai kampuni ya Bima ya bus ulilopata nalo ajali. Watakulipa.
 
Tufanye umegongwa na bodaboda au umeangukiwa na ukuta. Hapo vipi mdau maana tafsri ya ajali ni pana sana
 
Hifadhi risiti za matibabu na gharama nyingine zote bila kusahau tiketi uliyokata siku ajali ilipotokea. Hakikisha vyote vina majina yako halisi.

Nenda kaidai kampuni ya Bima ya bus ulilopata nalo ajali. Watakulipa.
Ahsante kwa elimu, lakini inakuwaje mfano nikigongwa na gari au ndugu yangu kagongwa na gari na akafa taratibu zimakuwaje?
 
Huu ni uzi wangu wa pili kuhusu kulipwa fidia, hii ni kwa sababu watu wengi kila siku wanapata ajari na wakifatilia fidia wanaishia kati kutokana na hatua nyingi au wengine kupotezea kutokana hawajui waazie wapi.

Mi ya kwangu ni hivi nilipata ajar mwezi wa kumi, sasa kuna ndugu yangu anafatilia ila ameambiwa kesi ipo mahakaman hii inamaana kama mambo ya fidia baada ya maamuzi ya mahakama bado tupo kwenye hatua ya kusubiri.

Sasa kama wewe ulishawahi kupata ajari na ukalipwa fidia njoo utupe experience yako ya kufatilia kesi za fidia , kwa kutuambia process zote ulizopitia hadi kupata fidia yako.

Hii sio lazima uwe uliwahi pata ajari lakini pia kwa yetote anayejua jinsi ya kufatilia fidia.

Karibuni sana.

View attachment 2021462View attachment 2021463
Mkuu umenikumbusha jambo la muhimu mno, last week tumezika bint yetu ambaye alipata ajali maeneo ya nanenane dom, lakini hatukufikria chochote kutokana na mstuko wa ule msiba, ngoja tuanze kufuatilia tuone.
 
Pole sana mkuu, sijui sijasoma vizuri au nimepitiwa lakini sijaona ulipata ajali ya aina gani, ulikua unaendesha pikipiki, ulipakiwa, ulikua kwenye basi, gari binafsi au umeumia katika mazingira gani? Ni kazini au kwenye mambo binafsi?

Bima unayoiongelea hapa ni ya chombo ulichopanda au ya kazini? Ukitoa hizo taarifa, zinnaweza kusaidia kupata msaada wa maelekezo vizuri. Ahsante
 
Pole sana mkuu,nimejitafakari uzima nilionao natakiwa kumshukuru Allah!Kwanza fuatilia afya yako iimarike na mimi nakuombea uweze kusimama tena uendelee na shughuli zako za kila siku.Sijui utaratibu unaotumika ila nitakupa namba ya mtu aliyewahi kupata ajali na bus la Zuberi akakatika mkono.Niliwahi kukutana na mwenye bus la Zuberi akamuambia yule dada mimi sipaswi kukulipa akatupeleka kwenye insurance ya mabus yake inaitwa Assurance iko pale opposite na Saphire Hotel kule maeneo ya Kisutu!
 
Kuna urasimu wa kutisha unapofuatilia fidia. Hata ukiwa na vielelezo vyote. Sijui wanafanya maksudi kukukatisha tamaa utemane nayo. Ni psychological torture ya hatarii
 
Back
Top Bottom