mwanafyale
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 1,641
- 535
Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada. Hii ni story ya kweli na imenikuta mwenyewe. Ushauri tafadhali.
Ni mwezi wa sita sasa tangu haya yanikute. Jamani mchepuko mbaya sana bakini njia kuu.
Ilikuwa siku ya Ijumaa baada ya kutoka kibaruani, nikaamua kwenda kwa mchepuko wangu mida kama ya saa 12 jioni. Baadae tukaamua kutoka kwa ajili ya kinywaji. Wakati huo mke wangu alikuwa yuko busy na masomo hivyo sikuwa na wasiwasi kuwa mambo yangebumbuluka. Mida ya saa 4.30 usiku tukatoka ili nimrudishe bi mdogo home. Tukiwa njiani si unajua tena mambo ya wapendanao hasa ukichanganya na ulabu. Bi mdogo alikuwa anaishi TipTop na tulikuwa tunatokea mitaa ya Rose Garden kupitia njia ya Shekilango.
Bila kujitambua kumbe mke wangu naye alikuwa anatoka kumuona mdogo wake aliyekuwa amepata ajali jioni hiyo mimi nikiwa sina taarifa maana simu niliizima. Kumbe mke wangu aliniona na yule mwanamke tukipigana mabusu huku naendesha gari, aliamua kutufuata hadi nilipokuwa namshusha ule mchepuko. Huku tukiagana kwa mabusu, mke wangu alinipigia honi akiwa amepaki pembeni yangu. Niliposhituka na yeye kuhakikisha nimemuona, alinipungia mkono na kuondoa gari.
Tatizo linalonipata, niliporudi home nilimkuta keshalala na hivyo sikuweza kuongea naye. Asubuhi aliondoka mapema kwenda chuoni. Zikapita kama siku 5 hivi bila kuongea naye maana alikuwa ananikwepa. Siku nilipopata muda wa kuongea naye, nilipoanza tu kujielelza, alijibu kuwa nisiwe na wasiwasi kwani aliishanisamehe, na anachotaka ni mimi kufurahia maisha. Hadi leo amekataa kushiriki na mimi tendo la ndoa na hataki kuzungumzia masuala yaliyopita. Natamani kufa mwenzenu. Ushauri please