Njooni hapa, mambo yamekuwa magumu sana kwenye hii ndoa

Kwa hali hiyo ya kumkomoa utaenjoy vekesheni? Manake adventure ya vekesheni is sex on the beach, or in the garden. Wewe mawazo yote kwenye bili?

bora umkomoe na house upgrading kwanza, now sofas, new fridge, new beds and curtains ama new car. Ukishamsamehe wewe ndo umpeleke vekesheni
Una point hapo, umeeleweka mamito
 
Mmmmmmh!Anakufanyia hivo coz anajua vitakuuma! Atleast un concious left! Nyie ndo michepuko mnaiibukia ukubwani! Guilty kibaoooo! Roho inakudunda 24/7......
Utoto unawasumbua, kama hujiamini small house ya nini?
 
Inaelekea hujui kuomba msamaha, miezi 6 hujasamehewa?
Tatizo wanaume hampendi kujishusha hata kama mmekosea. Hebu jishushe, onyesha kujuta, badili ratiba, kama ulikuwa unachelewa kurudi hebu jitahidi kuwahi.

Halafu swali la kizushi...We mchepuko umeuacha kweli? Hiyo miezi yote unaponea wapi wakati huduma ya ndani imesitishwa?
Kim nana huwezi kuamini, sina pa kuponea, kila cku nachafua mashuka mpaka naona aibu. Kwa kweli inabidi nifanye kazi ya ziada. Mchepuko nimeuacha kabisa ili nisawazishe ndoa yangu
 
Shida za kujitakia? Huu ni usemi niliokuzwa nao: 'you can do anything in this world, as long as you are prepared and have a good plan for its cosequences'

umepanda mbigili, unaona shida kuvuna? Majanga
Asante sana kaka. Wanaume tuna shida kweli kweli
 
Ulikosea kuchukua mwanamke mbovu..ndo maana mkeo alipomuona akawa na guts za kuwafuata..ungechukua kifaa cha nguvu angeenda straight home kulia..sasa hapo ana kuona ovyo ume toka nje umeacha home kifaa..yuko angry mno
Mkuu hata angechukua nini the wife was smart yeye alitaka tu kumuonyesha mumewe nimekuona usije kuruka baadae. Hakuwa na haja ya ugomvi na mi mdogo. Mi nimempenda bure... hata kama alilia mwanamke jasiri anafuta machozi yake hamuonyeshi jamaa kulia utalilia mbele huko wakati unatwangwa na mchepuko wako na wewe...!
 
Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada. Hii ni story ya kweli na imenikuta mwenyewe. Ushauri tafadhali.
Ni mwezi wa sita sasa tangu haya yanikute. Jamani mchepuko mbaya sana bakini njia kuu.

Ilikuwa siku ya Ijumaa baada ya kutoka kibaruani, nikaamua kwenda kwa mchepuko wangu mida kama ya saa 12 jioni. Baadae tukaamua kutoka kwa ajili ya kinywaji. Wakati huo mke wangu alikuwa yuko busy na masomo hivyo sikuwa na wasiwasi kuwa mambo yangebumbuluka. Mida ya saa 4.30 usiku tukatoka ili nimrudishe bi mdogo home. Tukiwa njiani si unajua tena mambo ya wapendanao hasa ukichanganya na ulabu. Bi mdogo alikuwa anaishi TipTop na tulikuwa tunatokea mitaa ya Rose Garden kupitia njia ya Shekilango.

Bila kujitambua kumbe mke wangu naye alikuwa anatoka kumuona mdogo wake aliyekuwa amepata ajali jioni hiyo mimi nikiwa sina taarifa maana simu niliizima. Kumbe mke wangu aliniona na yule mwanamke tukipigana mabusu huku naendesha gari, aliamua kutufuata hadi nilipokuwa namshusha ule mchepuko. Huku tukiagana kwa mabusu, mke wangu alinipigia honi akiwa amepaki pembeni yangu. Niliposhituka na yeye kuhakikisha nimemuona, alinipungia mkono na kuondoa gari.

Tatizo linalonipata, niliporudi home nilimkuta keshalala na hivyo sikuweza kuongea naye. Asubuhi aliondoka mapema kwenda chuoni. Zikapita kama siku 5 hivi bila kuongea naye maana alikuwa ananikwepa. Siku nilipopata muda wa kuongea naye, nilipoanza tu kujielelza, alijibu kuwa nisiwe na wasiwasi kwani aliishanisamehe, na anachotaka ni mimi kufurahia maisha. Hadi leo amekataa kushiriki na mimi tendo la ndoa na hataki kuzungumzia masuala yaliyopita. Natamani kufa mwenzenu. Ushauri please

pole mkuu,huyo hajakusamehe na inawezekana she is doing the worst thing that hatak ujue so anatumia kigezo cha kosa lako usimstukie think twice bro miezi6 hujakupa game its more than disaster vip na anakupikia chakula unakula?!. Nakushauri fanya toba kwa Mungu kwa kumaanisha that unajutia na hautarudia tena,then jisamehee nafsi yako and dont feel like we peke yako ndo umetenda dhambi kubwa ambayo hustahili msamaha then ongea na Mungu wako aliewaunganisha awe hakimu wa kesi iyo kwa kuwa umetubu kweli.Do that am sure utapata jibu.NOTE ukifanya ivi usirudie tena otherwise utajuta na n bora usifanye kama nlivyoshauri kama lengo lako n kuomba msamaha kisheria tu ili uwe na aman moyoni then urudie tena kwa mchepuko
 
Kumbuka marehem ndugu zako wote lia saaana harafu omba msamahaa ila utulie sasa huyo atakuua shauli yako na michepuko yako.
 
Kwa hiyo umekuja hapa kuomba faraja na sio ushauri.
Jaribu kufikiri wewe ungekuwa ndio umemuona anamiminiwa mabusu kwenye gari yake kisha ukampigia honi ili kumhakikishia ya kwamba umemuona ukampungia mkono ukaondoka alafu anarudi nyumbani anajaribu kuliongelea unamuambia nimeshakusamehe,swali langu kwako je utakuwa umesamehe kweli?
Huyo mke wako ana hasira ambayo haielezeki inawezekana usiku huwa anaamka anakuangalia unavyokoroma anatamani akate hicho lakini akikumbuka pengine mna na watoto anafikiria itakuwaje anaacha.
Ushauri wangu kwako mtafute mshenga au wazee wenye hekima mkae na mkeo chini myamalize.
Wanawake ni watu wenye huruma sana na vilevile ni makatili sana pale unapowakorofisha
Mmmmmh! Mbona unanitisha tena, badala ya kunipa faraja?
 
Usawazishe ndoa mwezi wa 6 sasa kaka? hivi umeshajiuliza haya maswali kwamba ndani ya miezi sita ni nani anampa huduma ya tendo la ndoa
Kim nana huwezi kuamini, sina pa kuponea, kila cku nachafua mashuka mpaka naona aibu. Kwa kweli inabidi nifanye kazi ya ziada. Mchepuko nimeuacha kabisa ili nisawazishe ndoa yangu
 
Kwa hiyo umekuja hapa kuomba faraja na sio ushauri.
Jaribu kufikiri wewe ungekuwa ndio umemuona anamiminiwa mabusu kwenye gari yake kisha ukampigia honi ili kumhakikishia ya kwamba umemuona ukampungia mkono ukaondoka alafu anarudi nyumbani anajaribu kuliongelea unamuambia nimeshakusamehe,swali langu kwako je utakuwa umesamehe kweli?
Huyo mke wako ana hasira ambayo haielezeki inawezekana usiku huwa anaamka anakuangalia unavyokoroma anatamani akate hicho lakini akikumbuka pengine mna na watoto anafikiria itakuwaje anaacha.
Ushauri wangu kwako mtafute mshenga au wazee wenye hekima mkae na mkeo chini myamalize.
Wanawake ni watu wenye huruma sana na vilevile ni makatili sana pale unapowakorofisha
Nashukuru mkuu
 
Usawazishe ndoa mwezi wa 6 sasa kaka? hivi umeshajiuliza haya maswali kwamba ndani ya miezi sita ni nani anampa huduma ya tendo la ndoa
Si ndio hapo mkubwa, lakini niamua kuwaza hayo nahisi ndio kabisa ntakuwa naharibu. Ngoja kwanza nijitahidi kusawazisha mengine baadae. Ngoja nivuke daraja moja baada ya jingine
 
Hiyo inaitwa psychological torture
Kweli mkubwa, kisaikolojia niko vibaya sana. Sina kawaida ya kurusha uzi unaonihusu humu jamvini, lakini leo maji yamenifika shingoni, sina jinsi. Kuna wakati nashindwa hata kufanyakazi mpaka naogopa naweza kufukuzwa.
 
Back
Top Bottom