Njooni hapa, mambo yamekuwa magumu sana kwenye hii ndoa

mwanafyale

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,641
1,250
Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada. Hii ni story ya kweli na imenikuta mwenyewe. Ushauri tafadhali.
Ni mwezi wa sita sasa tangu haya yanikute. Jamani mchepuko mbaya sana bakini njia kuu.

Ilikuwa siku ya Ijumaa baada ya kutoka kibaruani, nikaamua kwenda kwa mchepuko wangu mida kama ya saa 12 jioni. Baadae tukaamua kutoka kwa ajili ya kinywaji. Wakati huo mke wangu alikuwa yuko busy na masomo hivyo sikuwa na wasiwasi kuwa mambo yangebumbuluka. Mida ya saa 4.30 usiku tukatoka ili nimrudishe bi mdogo home. Tukiwa njiani si unajua tena mambo ya wapendanao hasa ukichanganya na ulabu. Bi mdogo alikuwa anaishi TipTop na tulikuwa tunatokea mitaa ya Rose Garden kupitia njia ya Shekilango.

Bila kujitambua kumbe mke wangu naye alikuwa anatoka kumuona mdogo wake aliyekuwa amepata ajali jioni hiyo mimi nikiwa sina taarifa maana simu niliizima. Kumbe mke wangu aliniona na yule mwanamke tukipigana mabusu huku naendesha gari, aliamua kutufuata hadi nilipokuwa namshusha ule mchepuko. Huku tukiagana kwa mabusu, mke wangu alinipigia honi akiwa amepaki pembeni yangu. Niliposhituka na yeye kuhakikisha nimemuona, alinipungia mkono na kuondoa gari.

Tatizo linalonipata, niliporudi home nilimkuta keshalala na hivyo sikuweza kuongea naye. Asubuhi aliondoka mapema kwenda chuoni. Zikapita kama siku 5 hivi bila kuongea naye maana alikuwa ananikwepa. Siku nilipopata muda wa kuongea naye, nilipoanza tu kujielelza, alijibu kuwa nisiwe na wasiwasi kwani aliishanisamehe, na anachotaka ni mimi kufurahia maisha. Hadi leo amekataa kushiriki na mimi tendo la ndoa na hataki kuzungumzia masuala yaliyopita. Natamani kufa mwenzenu. Ushauri please
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,272
2,000
Rip

Tukushauri nini? Mkeo yipo sahihi kwa nini akupe tendo la ndoa? Maradhi mengi. Imagine yeye atulize kujilinda halafu wewe unakitembeza starehe zako zisimcost maisha yake.

Pia hapo hatuna la kukushauri. Maana inategemea na kiasi gani umemuumiza mkeo. Ujue hakuna kitu kigumu kukijenga kama trust na hakuna kitu rahisi kukiharibu kama trust.

Mwache mpaka moyo wake utakapoamua kufunguka. Kwa sasa acha michepuko na omba sana moyo wa mkeo ulainike
 
kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,929
2,000
Kuna ajali na ajali ya kujitakia. Ogopa sana mwanamke akikuambia powa, nimekusamehe pasipo kupatikana muhafaka. Cha muhimu hakikisha unakaa naye japo si sasa ila kipindi mawasiliano ya kirudi. Kama alikuamini sana pole sana. kama alikufahamu wewe utulivu sifuri toka kabla hamjawa wanandoa hapo hamna tabu sana. Kila la kheri, jenga ndoa yako, familia yako iwe na furaha.
 
badiebey

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
5,877
1,500
Hehheeh jiandae kufa na sumu siku yoyotee,ana hasira beyond measure ogopa sana hasira ya aina hyo....ni kama vile mwili unapopata maumivu sanaa hadi kujitengenezea natural anesthesia,..
 
mwanafyale

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,641
1,250
Hehheeh jiandae kufa na sumu siku yoyotee,ana hasira beyond measure ogopa sana hasira ya aina hyo....ni kama vile mwili unapopata maumivu sanaa hadi kujitengenezea natural anesthesia,..
Mmmmmh! Mbona unanitisha tena, badala ya kunipa faraja?
 
lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,663
2,000
Mmmmmmh!Anakufanyia hivo coz anajua vitakuuma! Atleast un concious left! Nyie ndo michepuko mnaiibukia ukubwani! Guilty kibaoooo! Roho inakudunda 24/7

Kuna ZEE LA MICHEPUKO, mkewe alilifanyia hivo, likaita kikao, likajieleza limekosea, itafutwe suluhu, likachambwa mwanzo, mwisho,.

Likaja kutuambia bar yetu moja hivi, wezee wa kuchepuka, "Mke wangu hana adabu! Ananibania mimi!? Mimi baba gati? Mjitaaa! Mwanamke nimemuomba msamaha anakaa nachambwa anaangalia? Ameota pembe! Sasa namkomeshaaaa!

Tukamwambia lakini zee la kuchepuka kumbuka wewe ndo mkosefu, usigeuze kibao!

Nooo! Siwezi kuzeeka nasubiria huruma yake? Mimi mjita banaaa! Akahama kabisaaaa home! Akawa anakaa kilodge flani! Mkewe kaendelea kubanaa mambo!

Akaenda kumposa mwarabu mmoja pale pale mtaani, na mshenga rafiki yake kabisaa! Akaipitisha barua kwa mkewe! Weeee! Wajita walikuja fastaa toka musoma, zee la kuchepuka likakomaa lina oa mwarabu, mkewe kazi imemshinda kachoka kula baa! Na suluhu si walikataa mara ya kwanza! Ilikuwa kazi nzito, saivi lipo na mkewe na linachepuka kama kawaida!

The funny thing about marriage is hata ukikosea makusudi 90% utasemehewa tu, because the woman will try harder n harder to make it work by taking tones of bullahit!

NOTHING IS PERSONAL HERE! Na wala simshauri mtoa mada afanye haya bali hii ni KIBWAGIZO TU CHA HABARI! Bakini kwenye mada kuu! Kuchepuka kwenye mada kuusio dili!
 
mwanafyale

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,641
1,250
Kuna ajali na ajali ya kujitakia. Ogopa sana mwanamke akikuambia powa, nimekusamehe pasipo kupatikana muhafaka. Cha muhimu hakikisha unakaa naye japo si sasa ila kipindi mawasiliano ya kirudi. Kama alikuamini sana pole sana. kama alikufahamu wewe utulivu sifuri toka kabla hamjawa wanandoa hapo hamna tabu sana. Kila la kheri, jenga ndoa yako, familia yako iwe na furaha.
Kaka, nimejaribu sana kujikomba kwake na kuwa karibu naye imeshindikana. Nimemthibitishia kuwa yule mwanamke nimemuacha na kwamba ilikuwa bahati mbaya lakini huwa hajibu chochote. Mwanamke huyu ni mgumu sana kukubali ukweli
 
JJ10

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
282
0
Kama ukiamua kufa basi nakurestisha in peace kabisa!! Ila usisahau kumsalimia mwalimu' mfahamishe kwamba nchi imeuzwa na chama alichokiasisi!! R.I.P kabisa!
 
NANDERA

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,028
2,000
Nimeishia tu kucheka uliposema unataka kufa! Kufa hufi....sasa hivi mchepuko hata kuuskia hutaki, njia kuu nayo imekuwekea mawe. Aisee lazma utamani kufa..hahahahaaaa. We endelea kutumikia adhabu yako ya kufungiwa vioo. Mama akiishiwa ganzi atafunguka tu, au akishaamua la kufanya atafunguka na wewe utapata pa kuanzia. Kweli mchepuko NI dili.
 
charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,322
1,225
Kama kuna mapanga,sururu,mishale na dawa za kuulia wadudu nyumbani kwako hakikisha unazijengea safe.Nyumbani si sehemu salama tena ya kuishi.
 
CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,113
2,000
RIP marehemu.mtarajiwa....

Muwaheshimu wake zenu jamani si mliwaoa wenyewe na mkaapa kuwa waaminifu??

Safi sana mke wa marehemu mtarajiwa!
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,620
2,000
Duh!!!!! Pole zako nyingi sana.

Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada. Hii ni story ya kweli na imenikuta mwenyewe. Ushauri tafadhali.
Ni mwezi wa sita sasa tangu haya yanikute. Jamani mchepuko mbaya sana bakini njia kuu.

Ilikuwa siku ya Ijumaa baada ya kutoka kibaruani, nikaamua kwenda kwa mchepuko wangu mida kama ya saa 12 jioni. Baadae tukaamua kutoka kwa ajili ya kinywaji. Wakati huo mke wangu alikuwa yuko busy na masomo hivyo sikuwa na wasiwasi kuwa mambo yangebumbuluka. Mida ya saa 4.30 usiku tukatoka ili nimrudishe bi mdogo home. Tukiwa njiani si unajua tena mambo ya wapendanao hasa ukichanganya na ulabu. Bi mdogo alikuwa anaishi TipTop na tulikuwa tunatokea mitaa ya Rose Garden kupitia njia ya Shekilango.

Bila kujitambua kumbe mke wangu naye alikuwa anatoka kumuona mdogo wake aliyekuwa amepata ajali jioni hiyo mimi nikiwa sina taarifa maana simu niliizima. Kumbe mke wangu aliniona na yule mwanamke tukipigana mabusu huku naendesha gari, aliamua kutufuata hadi nilipokuwa namshusha ule mchepuko. Huku tukiagana kwa mabusu, mke wangu alinipigia honi akiwa amepaki pembeni yangu. Niliposhituka na yeye kuhakikisha nimemuona, alinipungia mkono na kuondoa gari.

Tatizo linalonipata, niliporudi home nilimkuta keshalala na hivyo sikuweza kuongea naye. Asubuhi aliondoka mapema kwenda chuoni. Zikapita kama siku 5 hivi bila kuongea naye maana alikuwa ananikwepa. Siku nilipopata muda wa kuongea naye, nilipoanza tu kujielelza, alijibu kuwa nisiwe na wasiwasi kwani aliishanisamehe, na anachotaka ni mimi kufurahia maisha. Hadi leo amekataa kushiriki na mimi tendo la ndoa na hataki kuzungumzia masuala yaliyopita. Natamani kufa mwenzenu. Ushauri please
 
NANDERA

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,028
2,000
Kaka, nimejaribu sana kujikomba kwake na kuwa karibu naye imeshindikana. Nimemthibitishia kuwa yule mwanamke nimemuacha na kwamba ilikuwa bahati mbaya lakini huwa hajibu chochote. Mwanamke huyu ni mgumu sana kukubali ukweli

Ilikuwa bahati mbaya kweli? Kama ni bahati mbaya basi inaweza kutokea tena maana bahati iko nje ya udhibiti wako. Siku 5 za kukaushiwa si nyingi. Mwache mwenzio nae apate muda wa ku-absorb shock hata kama itachukua miezi miwili. Unafikiri hili jambo ni rahisi kwake? Ana maswali kama 3000 hivi kichwani bado anajiuliza. Au anafikiri yuko usingizini anaota. Kumhakikishia kuwa umeuacha mchepuko haiwezi kuwa dawa ya imani iliyovunjika. Usipoweza kurudisha imani hata ukiacha mchepuko hataamini maana wakati anakuamini hakujua kama una mchepuko. Mi sijui imani inarudishwa vipi ila inawezekana baada ya muda mrefu na bidii ya ziada.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom