Njoolay amsifu Said Afri asema ipo tofauti kubwa kati yake na wabunge wengine wa Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njoolay amsifu Said Afri asema ipo tofauti kubwa kati yake na wabunge wengine wa Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  BAADHI ya viongozi wa ngazi ya juu serikalini mkoani Rukwa na Katavi wamemwagia sifa Mbunge wa Mpanda Kati, Said Arfi (Chadema) kuwa ni mfano wa kuigwa kwa wabunge wengine hususani wa upinzani kwa vile ni muelewa na wanafurahia kufanya naye kazi pamoja.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti , baadhi ya viongozi hao wakizungumzia hali ya kisiasa mkoani hapa hususani baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, walidai kuwa hali ya kisiasa mkoani ni shwari kabisa.

  Miongoni mwa viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa , Daniel Ole Njoolay ambaye bila kuumauma maneno alimmwagia sifa kemkem Arfi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa ni mchapakazi na kwamba ipo tofauti kubwa kati yake na wabunge wengine wa Chadema.

  "Mheshimiwa Arfi hakika ni Mbunge wa mfano na yupo tofauti sana na wabunge wengine hususani wa Chadema kwani tunafurahia kufanya naye kazi pamoja.

  “Hata kwenye vikao anachangia kwa hoja za msingi na si kwa kubeza au vinginevyo kwa kweli anastahili sifa, hana matatizo kabisa labda ndiyo maana hatuna purukushani zozote za kisiasa mkoani hapa,” alisema.

  Akizungumzia kuhusu hali ya kisiasa mkoani hapa, Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa hali ya kisiasa mkoani hapa baada ya uchaguzi Mkuu ni imara na shwari kabisa na kwamba wakazi wanaendela na shughuli za kimaendeleo kwa amani na utulivu.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Dk. Rajab Rutengwe alimmwagia sifa Mbunge huyo akidai kuwa hajutii kuwa na Mbunge wa upinzani wilayani kwake kwani ametoa mchango mkubwa wa kuwahimiza wananchi kushiriki shughuli za maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa.

  “Mheshimiwa Arfi si mwanasiasa anayehubiri amani na utulivu na si mtu wa shari wala vurugu …kwa kweli sijutii kufanya naye kazi hakika yuko tofauti sana na wabunge wenzake wa upinzani hususani wa chama chake cha Chadema kwani amekuwa mstari wa mbele kuwahimiza wafuasi na mashabiki wa chama chake kushiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao wanakoishi,” alisema Arfi ambaye ni maarafu jimboni kwake kama ‘Babu’ ameweza kutetea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Mpanda Kati sasa Mpanda Mjini kwa tiketi ya Chadema kwa vipindi viwili mfululizo, ni mbunge pekee kutoka chama cha upinzani mkoani hapa.
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Kumfananisha Arfi na wabunge wengine wa upinzani ni kama kufanisha maziwa na tui la nazi, vyote ni vyeupe lakini tofauti zake ni kubwa saaaana. Arfi ni mtu makini na asiye kurupuka na wala hana papara, yeye ni mchapa kazi. Wala hana haja ya kujitafutia umaarufu usio na mpango kama wabunge wengine wa Chadema na vijikinda vyao vya juzi.
   
 3. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi Bw. Majimshindo huoni kwamba nchini kwetu tunapata matatizo/changamoto nyingi sana (hospitalini-huduma si nzuri, dawa hazi kidhi mahitaji, umeme matatizo, rushwa n.k), na kwamba kila moja akikaa kimya basi walewalio na majukumu watakaa tu wakifikiri kila kitu kiposhwari! nimuhimu kuwe na watu wanapiga kelele ili viongozi wetu wasisale! wazidi kututumikia........
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Kelele za mlango hazimshtuwi mwenye nyumba, kuna njia mbadala za upinzani kutumia badala ya makelele. Tumuulize Arfi, vipi jimbo lake anachaguliwa yeye na hana kelele na mambo huko mazuri kabisa, ana njia gani mbadala wa kelele?
   
 5. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Ndo tabu ya Mpemba mzoea taarab. Nani mwenye nyumba sasa, katiba haioneshi uhusiano kati ya chama tawala na uenye nyumba. Suck you !
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  majimshindo ana shangaza sana aurgument zake!
   
 7. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hao ndio viongozi tunaotaka,bwana Arfi nami namkubali sana na hana makeke kabisa kama wapinzni wengine esp yule bwana mdogo lema! siasa sio maandamano wala kelele ni vitendo,hongera sana bwana Arfi we tumikia wananchi wako na nina imani wananchi wa huko walikuchagua wewe na sio chadema na unaweza ukagombea chama chochote na ukashind tena coz we ni mtu wa vitendo,washauri wenzako watulie majimboni wawatumikie wapigakura wao na sio kwenda kuandamana kwani wananchi hatukuwatuma kwenda kuandamana bali kututumikia majimboni
   
 8. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  mmeanza kujiandaa kukabiliana na maandamano. tuko liberia tukirudi tutasona muda mwafaka kuja kulianzisha huko rukwa!
   
 9. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mmmmmmmmmh, sidhani kama hongera hii yatoka moyoni. Inonesha labda viongozi serikali wa mkoa wa katavi na wilaya ya mpanda ni waelewa na wanaweza kuchukua changamoto kama njia ya kujifunza; na mikoa mingine wako regid-km arusha ambao kitu kidogo tu-uhuru wa watu kuandamana na kutoa hisia zao uiwapa kiwewe na kutamani kuzuia. Hivyo, si suala la mbunge nani bali ni namna gani kiongozi wa serikali anavyoweza kuwa msikivu. Ndo maana hukusikia machafuko mz, kagera, syinganga na bukoba wakati wa maandamano.
   
 10. Mbeu

  Mbeu Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo mong'oo hana jipya, wabunge wote wa CDM safi, wanatekeleza duty yao ya kukeep the government on its toes, aache kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
   
 11. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mmh leo tena! Au kwa kuwa Babu? Hapa kutakuwa kuna kamchezo wanamchezea Mr. Arfi!
   
 12. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taabu ya mlevi mla nguruwe anayeishi Mbezi asiyejua Kiswahili vizuri lakini anadhani nchi hii ni ya kwake pekee yake!
   
 13. F

  Froida JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hakuna shida kama anatekeleza wajibu wake unavyopaswa ni kwa vile anatekeleza sera za chama chake kama wabunge wenzake wanavyofanya
   
 14. J

  Joblube JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mbinu zunu za kuigawa CHADEMA tumezishtukia hapa imekulakwenu manataka kumchooa Arfi muendeleze agenda ya Udini kama mnavyopanga na Zitto imekula kwenu mara mia.
   
 15. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Habari yako Kashanga vp huko Russia? napita tu
   
 16. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kazi ngumu kuliko zote ni kuwa kibaraka, kufanya kazi ambayo inapingana na nafsi yako na kusema vitu vya uongo ukitaka watu waviamini kuwa ni ukweli. Kuna watu hapa JF wanaonekana waziwazi kuwa ni vibaraka wakitumika kama vitendea kazi vya watu
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Asiye juwa maana haambiwi maana, hata bibilia ina kitu kinaitwa "parables", jee, nayo ni taarabu?
   
 18. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Hivii umesoma mada? mimi nimeishrehesha tu, sijaleta "argument" yeyote, lakini tunavyoendelea na mada zinaweza zikawepo.
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Heko kwa kuliona hilo, kwenye red ndio nnposema mimi hao wabunge wenzake badili ya kukaa na kupoteza muda kwa makelele, maandamano, watu kuumia na mpaka kupoteza maisha, kwa nini hawafati mfano wa kuigwa wa Arfi?
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Hayo ya udini unayasema wewe. Sisi tunasema, heko Arfi. Upinzani si fujo na maandamano, upinzani ni kuchapa kazi zaidi ya waliopo kwenye madaraka ili waonekane hawafai.
   
Loading...