Njoo utupe mbinu za kupata wateja online kwa wepesi

CHENGU MANURE

JF-Expert Member
May 26, 2015
913
1,000
Wasalaam

Watu wengi sasa wameanza kuamini biashara kwa njia ya mtandao. Leo jioni nimekuwa kwenye ofisi moja idadi ya wateja na Mahala ilipo hakuna uhusiano. Baadae nikagundua wote wanawatolea online.

Kuna jamaa aliishiwa hadi akataka kurudi kwao kigoma kutoka Dar. Jamaa sio msomi Hata wa form four. Alitokea mtu akampa ramani ya kuuza bidhaa za madukani online. Akiwa na bodaboda yake ndani ya mwaka alijenga Nyuma Mbili DSM na Kigoma. Platform yake ilikuwa ni instagram na FB tu.

Binafsi nimekuwa nikijaribu lakini matokeo ni hafifu na yanapanda na kushuka.

Karibu unishauri, mbinu za haraka ila za uhakika wa kufanya digital marketing kwa bidhaa yoyote ili iwe faida na kwa wengine.

Unaweza kutoa ushuhuda wako na uzoefu wako binafsi wa online au digital marketing.
 

Luckytz

Senior Member
Jul 5, 2018
120
250
Unaweza kufafanua zaidi hapa?

Nini hasa muuzaji anapaswa kufanya ili kufikia hilo lengo la ku_tengeneza Authority?

Ahsante
Muuzaji anatakiwa kuwa na uweledi wa kutosha juu ya kile anachokiuza kwa mteja...mfano wewe unauza handbags unatakiwa kuwafundisha wafuasi wako namna ya kutambua handbags original na fake...hapa utawaaminisha wateja wako kuwa una utaalam katika eneo lako hivyo wengi wataamua kutoa oda au kununua kutoka kwako kwani wanaamini wewe ndiyo mtu sahihi kwao...ahsante.
 

left eye

Member
Jun 30, 2018
62
125
Me nafanya hizo biashara na kiukwel inalipa sana ,ila ili uweze kuuza online ni kama kawaida tu ,iko kitu unachouza kinahitajika kias gan na watu na utofaut uko kias gan na sehem zingine.
 

Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,149
2,000
Karibu unishauri, mbinu za haraka ila za uhakika wa kufanya digital marketing kwa bidhaa yoyote
Mbinu za haraka ni utapeli na hazina uhakika kama hutaishia mikononi mwa manjagu.

Online marketing sio rahisi kwa sababu unahitaji kutumia jasho na machozi na wakati mwingine pesa.

Hatua ya kwanza jifunze namna ya kuuza bidhaa. Jinsi ya kuleta watu kwenye wavu wako, kuwachuja na kuwashawishi wateja. Hii sio rahisi na itachukua muda sana kujifunza.

Then ukiisha kupata watu ambao unadhani bidhaa yako inatatua matatizo yao, watafute na uwashawishi.

Hakikisha hiyo hatua ya mwisho unaifanya kwa
1. Watu walio na tatizo ambalo bidhaa yako inatatua
2. Tatizo hilo wanatamani kuondokana nalo
3. Wana nguvu ya maamuzi ya kununua au wana influence kwa mwenye maamuzi
4. Wana pesa ya kulipia bidhaa yako

Hakikisha unaepuka kila aina ya utapeli na unakuwa muwazi na mwadilifu katika kila hatua!
 

Mr sule

Member
Oct 14, 2021
6
45
Biashara ya online ni ngumu, ila ukitaka biashara ya online fanya matangazo kila siku utaona faida yake. Namaanisha natangazo ya kulipia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom