Jifunze kilimo cha nyanya

swali tafadhali:hivi madawa ya kupulizia minyanya huweza kudumu kwenye majani ikizuia wadudu kwa muda gani?na je,mvua ikinyeshea inabidi upulizie tena?
mvua ikinyesha itabidi urudie kupiga dawa, na ndio umakini tunaozungumzia dawa inapigwa jua likianza kutoka kusiwe na umande lazima uangalie hali ya hewa kabla ya kupiga dawa na ikitokea mvua ya ghafla acha kupiga dawa na kama umemaliza kupiga dawa mvua ndio ikanyenya kama imepita hata lisaa moja dawa imefanya kazi haina haja ya kurudia.
kuhusu dawa inadumu muda gani kila dawa imeandikwa inadumu muda gani ila mara nyingi ni siku 7 na siku 14
 
dokta ; matunda ya nyanya yanaharibika kwa kuanzia kwenye kitako cha tunda la nyanya. Wengi wanasema tatizo ni joto. nipo tabora. je ni kweli tatizo ni joto? nifanyeje?

Sent using Jamii Forums mobile app
ni joto kweli zinakuwa kama zimeungua,
mwagilia maji mengi hasa jioni ardhi ikiwa imepoa na asubuhi mapema sn usimwagilie wakati wa jua kali
 
Mimi ni mkulima wa nyanya na mpunga kijiji cha Mbigili, Dumila mkoani Morogoro. Wakulima wenzangu wa nyanya, tubadilishe uzoefu wa kilimo hiki kuhusu mbegu, mbolea, magonjwa, madawa na masoko.

Karibuni sana!
56cf2ca6970ba3ac157c53c37b1085ec.jpg
0ab7cb4ef777665dcd561f3fd8542a25.jpg
d5bdacda633cb03c38ae62bd31849565.jpg
f049f2f4fc7fda2d32ffc798a38732dc.jpg

Habar yako mkuu hizo zote zimechukua muda gani tangu umepanda mpaka kukuletea mavuno yote hayo .?
Kwanza nikupongeze Kwa kazi kubwa uliofanya.

Pia ni magonjwa gani mwenyew umepambana nayo mpaka ku win kiasi cha kuvuna mavuno hayo mkuu?

Nikitaka kuingia katika Kilimo cha nyanya ungali mzoefu kwa kipindi chote tangu umeanza unanishauli vipi Mimi nisie elewa chochote kuhusu hichi Kilimo mkuu.

(changamoto ambazo nijiandae kisaikolojia kukabikiana nazo, mazingira yapi ambayo ni favourable na njia zipi nitumie kupata mazao mengi?) nakutegemea mkuu Kwa hayo
 
Nyanya zinachukua miezi mitatu baada ya kupanda unaanza kuvuna

Changamoto ya magonjwa sio kubwa sana ni kuwa makini tu shambani na kupiga dawa mapema kila unavyoona dalili za ugonjwa na zipo dawa za kuzuia wadudu kabla hawajaanza kushambulia mazao.
 
Habar yako mkuu hizo zote zimechukua muda gani tangu umepanda mpaka kukuletea mavuno yote hayo? Kwanza nikupongeze Kwa kazi kubwa uliofanya*
Pia ni magonjwa gani mwenyew umepambana nayo mpaka ku win kiasi cha kuvuna mavuno hayo mkuu?

Nikitaka kuingia katika Kilimo cha nyanya ungali mzoefu kwa kipindi chote tangu umeanza unanishauli vipi Mimi nisie elewa chochote kuhusu hichi Kilimo mkuu.

(changamoto ambazo nijiandae kisaikolojia kukabikiana nazo, mazingira yapi ambayo ni favourable na njia zipi nitumie kupata mazao mengi?) nakutegemea mkuu Kwa hayo

Changamoto kubwa ni shamba zuri, mbegu nzuri na Huduma nzuri shambani ukifanikiwa hayo utakumbana na changamoto ya bei kuhusu soko ni uhakika.

Kwa Moro hakuna changamoto kubwa ila nyanya inahitaji uangalizi sn na umakini wa hali ya juu.
 
changamoto kubwa ni shamba zuri, mbegu nzuri na Huduma nzuri shambani ukifanikiwa hayo utakumbana na changamoto ya bei kuhusu soko ni uhakika

kwa Moro hakuna changamoto kubwa ila nyanya inahitaji uangalizi sn na umakini wa hali ya juu
Mkuu hii mbegu nibei gani: Mbali na mbegu hiyo ya asilla ipi mbegu nyingine nzuri yenye bei nafuu
Vip kuhusu mbegu ya riogrand ina ubora na sifa gani Je, nyanya inahasara hatakama ukiuza tenga kwa bei ya 10000 itakulipa ikiwa umezihudumia vizuri?
 
Mkuu hii mbegu nibei gani. Mbali na mbegu hiyo ya asilla ipi mbegu nyingine nzuri yenye bei nafuu. Vip kuhusu mbegu ya riogrand ina ubora nasifa gani. Je, nyanya inahasara hatakama ukiuza tenga kwa bei ya 10000 itakulipa ikiwa umezihudumia vizuri?
Mbegu zipo kwenye makundi mawili, kuna mbegu za kawaida na mbegu za kisasa. Kwenye mbegu za kisasa assila inafanya vzr sn japo bei yake kubwa Ila zipo mbegu zengine za kisasa zenye bei nafuu mf kilele, Monica f1, kipato nk
 
Mkuu hii mbegu nibei gani. Mbali na mbegu hiyo ya asilla ipi mbegu nyingine nzuri yenye bei nafuu. Vip kuhusu mbegu ya riogrand ina ubora nasifa gani. Je, nyanya inahasara hatakama ukiuza tenga kwa bei ya 10000 itakulipa ikiwa umezihudumia vizuri?
Kwa mbegu za kiwaida riogrand inafanya vizur Ila sio kama sawa na mbegu za kisasa.

Kuhusu bei ikianzia 10000 ni bei nzuri inalipa gharama na faida unapata kubwa tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom