Njoo tusimualiane Mambo ya kutisha/kuogopesha uliyowahi kushuhudia hapa Duniani

Fugeni paka, mbwa hapambani na mauzauza anapambana na wizi tu, kikubwa anabweka tu na kusepa. Ila paka bob, haondoki mpaka kieleweke, ama afe yeye au afe mchawi/shetani. Paka ni mlinzi mzuri kwenye haya maswala, hatuwaelewi tu mana wanajiskia sana wanyama hawa.

Watalaamu wanakwambia ukiona paka amekujua mguuni na kukuzonga sana haondoki ujue anakulinda na ubaya wa mauzauza, ila sisi tunaona anatusumbua tunampiga teke :D
 
Paka ni kiumbe dhajfu sana, hata mchawi hawezi kumwona ndiyo atapambana naye vipi. Kama ulikuwa hujui wachawi hawawezi mtumja kiumbe ambaye anawaona wakifanya yao, ndiyo maana husikii wakimtumia mbwa, nguruwe au punda. Ila paka anatumiwa sana
 
Mzee baba sifikiri kama kuna mnyama hana jicho la kuona mambo ya giza.

Ngoja tumwite mtaalamu atwambie kama paka kweli ni dhaifu kama usemavyo, nijuavyo mie paka ndio mnyama bora wa kumfuga na ni mlinzi mzuri kwenye mambo ya giza. Hao uliwataja wote ni kupiga kelele tu kama jogoo. Hawana kupambana kumoja.

Mshana Jr
 
Paka ndiyo dhaifu sana kuona mambo ya giza, wewe labda unasikia akipigana na paka wenzie usiku akitoa mlio kama watoto ndiyo unadhani wanapigana na wachawi.. Mchawi hawezi kumtumia mnyama anayemwona akifanya mambo yake, ndiyo maana hamtumii Mbwa, Nguruwe au Punda hata siku moja. Hao wanamwona bila chenga akija kuwanga, hawezi wagusa kumtumia.

Mbwa ndiyo mlinzi mzuri ila hawezi kuingia ndani ya nyumba, ndiyo maana wachawi muda mwingine wanaua mbwa wakiona anawawekea zengwe
 
msome huyu mtaalamu apa

MAAJABU YA PAKA
 
*****Kuna siku moja hapo hotelini, kuna mfanyakazi mmoja alienda choo cha kufanya haja kubwa usiku, kufungua mlango akamkuta paka amejifia katikati ya sink ya choo, na alikuwa paka ameshiba kweli, yaani hakuwa na madonda labda ukasema alipigwa akaja akafia pale. Ebana, wee, staff wote waligoma kwenda kumtoa. Apo hoteli walinzi wetu walikuwa ni JKU, ni jeshi la Zanzibar, akatoka mmoja akaenda kumtoa na kwenda kumzika nje ya hotel. Kila staff akawa ameingiwa na woga, mana wanaona sasa yale mambo ya Zamani ya kukoseshana amani yamerudi tena kwa kasi. Hakuna aliekuwa anaenda chooni ikifika Saa nne usiku.

Sasa mimi kama nlivosema awali, naamini haya mambo yapo, lakini kabla ya ku conclude na assume ni kitu kingine cha kawaida tu.

Siku moja kama kawaida yangu baada ya kumaliza Youtube, navuta taulo naenda zangu choo cha haja kubwa halafu ndio niingie shower. Mara nakaribia chooni, nasikia kama vile mtu anajimwagia maji, lakini hio haikuwa chooni sasa, kuna sehemu karibia na kona ya fensi kuna generator, hapo ndipo nikawa naskia sauti inatokea hapo. Kiroho kikaanza kunidunda, sijui nirudi tu chumbani nikaushie ama vipi. Lakini nkasema hapana, ngoja nipate ushahidi kamili, nikasogea sogea ata kufika lile eneo bana, kuna bidada alikuwa anajimwagia maji kumbe staff wa hotel :D :D :D Alishtuka kuniona, nikarudi nyuma kwenye position ambayo simuoni kumpa stara uku nikamuelewesha aache kuoga chini ya generator atasababisha matatizo. Nikamuuliza, choo kipo, tena kina maji ya moto na baridi, unaoga kwa raha, kilichokufanya uoge maji ya baridi usiku huu pembezoni mwa generator nini? Akanijibu hakuna anaekwenda chooni baada ya saa nne tangu tukio la yule paka! nikamwambia aache upumbavu tu. Mi nikaingia zangu chooni nikiwa nimejikaza kisabuni tu. Mana nlikuwa na wasiwasi ivo ivo. lakini nlimaliza yangu fresh.

Kutoka sasa naskia tena kuna pirika pirika, katika hilo eneo kuna kontena ya mambo ya maintainance, kama kawaida nkasema ngoja nikatafute ushahidi kamili, akatokea fundi kwa nyuma uku akiwa amemaliza kukojoa, Nilimchana kidume kizima na yeye anasita kuingia chooni kufanya haja zake.

*****Hii hapa nilijiroga tu mwenyewe..... Usiku wa manane nilitoka room kwangu nikaenda jikoni kujipikia mana njaa ilinibana sana. Mzee baba nikasikia vishindo ndani ya jiko na mimi nimo humo humo ndani, izo mbio nilizotoka apo breki ya kwanza nilikwenda kumuamsha Chef mkuu, nkamwambia bana jikoni kuna mauzauza yamenitokea wakati najitaarisha kupika, hapo moyo unakwenda mbio kiama. Halafu chumba changu kilikuwa kinaface moja kwa moja na main entrance ya jiko. Chef mkuu akatoka akasema hebu twende, tukaingia jikoni, tunaanza kuangaza, kumbe bana mle ndani kulikuwa na paka tu alitoka mbio. Dah! roho apo ikatulia afadhali.

Aisee hio hotel hata kama hakuna mauzauza mazingira yake pekee yanatisha, ni sehemu ambayo ipo kimya sana. Na nilikuwa najitahidi kuwa jasiri, mana kuna baadhi ya siku ilinilazimu mida ya saa nane usiku nitoke niende nikamuamshe mgeni kwa ajili ya departure, vyumba vipo mbali sana na staff house, dah apo ilikuwa ni kuomba usiyakute njiani.
 
Nilikua nipo kwenye mood ya kumasturbate yaani nilikua natafuta uzi wa mwisho kabla sijaingia xvideos sasa nimefika hapa na xvideos siendi leteni visa niburudike.
😀😀😀 Mjinga sana wewe
 
MAAJABU YA PAKA
Paka ni mnyama mwenye hisia kali sana na pia paka anauwezo mkubwa wa utambuzi, na paka anapo ona roho yoyote katika nyumba kitu cha kwanza cha kufanya hujalibu kuangalia kama roho hiyo ni nzuli au mbaya.

Na akikuta roho hiyo ni mbaya basi hulia kwa mlio wa mshangao na kuonyesha ya kwamba katika nyumba kuna kiumbe ambacho si cha kawaida. Kwa hiyo kuamakini sana na paka wako na uangalie akiwa anaendelea kuzunguka na kubadili rangi yake ya macho basi jua kua kuna jini mbaya kaingia katika nyumba yako unatakiwa ufanye utaratibu wa kumfukuza.

Wakati paka anapoona roho ndani ya nyumba, jambo la kwanza analofanya ni kumfuata kote ili kufahamu nia ya roho zilizo ingia ndani ya nyumba zina maana gani. Ili kuhakikisha kwamba chombo hiki hakitatishi eneo lao, paka hufanya kila jaribio liwezekanalo kulifukuza jini hilo katika makazi yake ya nishati yaani mahali anapo ishi.

Ikiwa njia ya kupiga makelele haitafanya kazi paka hubeba kipengele katika uwanja wake wa nishati yake yaani katika viumbe wake na huiongoza nje ya nyumba na ndipo utaanza kuona paka anagoma kukaa nyumbani.

katika mila zingine, kulikuwa na njia wakati roho mbaya hupanda au kuruka kwenye paka basi walikua wakimuita paka na kumfinya au kumlingishia kitu ili apige kelele jini huyo aondoke.

watu wenye kuwasiliana na roho hua hawaruhusu paka kuingia katika chumba cha ibaada cha kuitia roho,au mahali walipo fugia huyo jini maana akija na akakuta kuna paka jini huyo hatakaa ataondoka.

Kwa hiyo, tunapaswa kuelewa kwamba wakati paka atakua anajipitisha pitisha na kupiga piga au kukugusa gusa miguu yako, si tu kwamba sio kwamba zamila yake anataka tu chakula kutoka kwako bali anaweza kua anakufikishia ujumbe furani, lakini pia inamaanisha kwamba paka inashirikisha uchawi wake na wewe, nguvu ya astral, na wakati mwingine paka anaweza kukuchukia basi ujue ya kwamba kuna uwezekano wa wewe kua na jini mchafu.

Ili kuamini kua paka ana utambuzi wa hali ya juu hebu jalibu kumpa sumu, ndipo utaamini maana hawezi kula hiyo sumu na kijaliwa kuila basi kufa kwake ni kugumu.

Paka sio tu kulinda nyumba kutokana na roho wabaya kuingia ndani ya nyumba, lakini pia analinda nyumba kutokana na nguvu hasi ambayo ilikaa hapo kabla ya paka hata kuja nyumbani. Pia kuna baadhi ya watu walikua wakitaka kuhama nyumba walikua wakimtanguliza paka kwanza kabla hawaja hamia ili iwasaidie kufukiza nguvu hasi za kichawi ambazo huenda zikawa katika nyumba hiyo.

Pia paka akiona mgeni kaja na mgeni huyo ni mchawi basi paka hua hachezi mbali na eneo hilo na huenda akaanza kumparua au kumgusa gusa kwa kutumia mkia wake, hapo anakua anategua uchawi
Kwa kuwa paka ni njia za nishati ya cosmic, zinaweza kuleta nishati nzuri ndani ya nyumba, ambayo itasaidia ustawi na ustawi wa familia nzima.

Warusi walikuwa na ibada ya kuvutia sana: wakati wa kuhamia mahali papya wao kwanza walitanguliza paka ndani ya nyumba. Ikiwa nyumba ilikuwa mzee yaani nyumba ya zamani ambayo ilisha tumika, paka ilikuwa ikivuta nishati zisizo hitajika. Ikiwa nyumba ilikuwa mpya basi pia walikua wakimtanguliza paka ili aingize nishati za kinga na nuru katika nyumba hiyo.

Matumizi makubwa ya nguvu za kichawi za paka hupatikana katika uponyaji na hasa kwa paka mwenye langi nyeupe au alie changanyika madoa meupe na meusi.

Paka mwenye rangi nyeusi tupu hua na nishati za kichawi na mazingaombwe na dawa za giza.

Paka mweusi wachawi humtumia katika dawa za kumpoteza mtu na kumfanya msukule asionekane katika macho ya kawaida.

Paka za uzazi na rangi yoyote zina uwezo wa kutibu na zinaweza kuwatendea mabwana wao bila uwazi, ziko kwenye maeneo yao maumivu. Mojawapo ya mbinu rahisi za matibabu kwa msaada wa paka - rahisi kumpiga, kutolewa watu kutokana na matatizo ya akili na kihisia. Katika paka za uponyaji hutumiwa kuboresha maono pia. Ili kufikia mwisho huu, waganga wengine wanashauriana mchanga paka mweupe.

RANGI ZA PAKA NA KAZI ZAKE.
1. Nyeusi: wivu, nguvu za uchawi, ulinzi, uchawi mwingi! Licha ya tamaa zote, wanyama wa rangi huchukua nishati mbaya huondolewa katika matatizo ya kaya (miji) hutoa hekima na ufahamu.

2. Paka nyekundu (mwekundu): wachawi wa kawaida wa mwezi, wenye nguvu za kiume, nguvu za jua na nguvu ya miujiza hawatakiwi kumuona paka akifanya mapenzi maana wakimuona huwatia mikosi, na malaika au kiumbe anae mmiliki paka huyu wa rangi nyekundu ni kiumbe wa utajili.

3. (paka wa rangi ya kijivu): Paka za rangi hii huleta upendo, furaha, bahati nzuri, pamoja na utulivu wa kihisia na amani ya kimwili na huongeza furaha katika ndoa kama utakua umemfuga paka wa rangi hii.

4. Paka mweupe: paka mweupe wachawi humtumia kuunda uchawi wa mwezi, pia paka mweupe wana nguvu za uponyaji ndo maana katika baadhi ya nchi ukifika kwa mganga au kwa mchungaji utakuta kuna paka mweupe. Paka mweupe huwapa watu hisia za uzuri na kupendeza machoni pa watu, hupunguza matatizo katika familia.

Amerika, inachukuliwa kuwa ni mleta amani katika mji.

5. paka mwenye rangi tatu= nyekundu,kijivu na nyeupe:

Paka mwenye langi hizi kwa Amelika huhesabika kama paka wa kifalme, na paka akizaa paka wa ainahii hupendwa sana.

Pia paka amepewa uwezo mkubwa wa kuona kitu katika giza na mawindo yake mengi huyafanya kwa urahisi kukiwa na giza.
 
*****Kuna siku moja hapo hotelini, kuna mfanyakazi mmoja alienda choo cha kufanya haja kubwa usiku, kufungua mlango akamkuta paka amejifia katikati ya sink ya choo, na alikuwa paka ameshiba kweli, yaani hakuwa na madonda labda ukasema alipigwa akaja akafia pale. Ebana, wee, staff wote waligoma kwenda kumtoa. Apo hoteli walinzi wetu walikuwa ni JKU, ni jeshi la Zanzibar, akatoka mmoja akaenda kumtoa na kwenda kumzika nje ya hotel. Kila staff akawa ameingiwa na woga, mana wanaona sasa yale mambo ya Zamani ya kukoseshana amani yamerudi tena kwa kasi. Hakuna aliekuwa anaenda chooni ikifika Saa nne usiku.

Sasa mimi kama nlivosema awali, naamini haya mambo yapo, lakini kabla ya ku conclude na assume ni kitu kingine cha kawaida tu.

Siku moja kama kawaida yangu baada ya kumaliza Youtube, navuta taulo naenda zangu choo cha haja kubwa halafu ndio niingie shower. Mara nakaribia chooni, nasikia kama vile mtu anajimwagia maji, lakini hio haikuwa chooni sasa, kuna sehemu karibia na kona ya fensi kuna generator, hapo ndipo nikawa naskia sauti inatokea hapo. Kiroho kikaanza kunidunda, sijui nirudi tu chumbani nikaushie ama vipi. Lakini nkasema hapana, ngoja nipate ushahidi kamili, nikasogea sogea ata kufika lile eneo bana, kuna bidada alikuwa anajimwagia maji kumbe staff wa hotel :D :D :D Alishtuka kuniona, nikarudi nyuma kwenye position ambayo simuoni kumpa stara uku nikamuelewesha aache kuoga chini ya generator atasababisha matatizo. Nikamuuliza, choo kipo, tena kina maji ya moto na baridi, unaoga kwa raha, kilichokufanya uoge maji ya baridi usiku huu pembezoni mwa generator nini? Akanijibu hakuna anaekwenda chooni baada ya saa nne tangu tukio la yule paka! nikamwambia aache upumbavu tu. Mi nikaingia zangu chooni nikiwa nimejikaza kisabuni tu. Mana nlikuwa na wasiwasi ivo ivo. lakini nlimaliza yangu fresh.

Kutoka sasa naskia tena kuna pirika pirika, katika hilo eneo kuna kontena ya mambo ya maintainance, kama kawaida nkasema ngoja nikatafute ushahidi kamili, akatokea fundi kwa nyuma uku akiwa amemaliza kukojoa, Nilimchana kidume kizima na yeye anasita kuingia chooni kufanya haja zake.

*****Hii hapa nilijiroga tu mwenyewe..... Usiku wa manane nilitoka room kwangu nikaenda jikoni kujipikia mana njaa ilinibana sana. Mzee baba nikasikia vishindo ndani ya jiko na mimi nimo humo humo ndani, izo mbio nilizotoka apo breki ya kwanza nilikwenda kumuamsha Chef mkuu, nkamwambia bana jikoni kuna mauzauza yamenitokea wakati najitaarisha kupika, hapo moyo unakwenda mbio kiama. Halafu chumba changu kilikuwa kinaface moja kwa moja na main entrance ya jiko. Chef mkuu akatoka akasema hebu twende, tukaingia jikoni, tunaanza kuangaza, kumbe bana mle ndani kulikuwa na paka tu alitoka mbio. Dah! roho apo ikatulia afadhali.

Aisee hio hotel hata kama hakuna mauzauza mazingira yake pekee yanatisha, ni sehemu ambayo ipo kimya sana. Na nilikuwa najitahidi kuwa jasiri, mana kuna baadhi ya siku ilinilazimu mida ya saa nane usiku nitoke niende nikamuamshe mgeni kwa ajili ya departure, vyumba vipo mbali sana na staff house, dah apo ilikuwa ni kuomba usiyakute njiani.
Je kuna mteja yeyote ambaye aliwahi ku experience hiyo situation hapo hotelini?
 
Je kuna mteja yeyote ambaye aliwahi ku experience hiyo situation hapo hotelini?
Kwenye hotel yetu, ilikuwa ni Staffs tu ndio wanatokewa na mambo. Ila kuna hotel nyengine ipo kusini, hio nimemsikia Tour operator mwenyewe ambaye ni mzungu, wakati tunafanya site inspection kwenye hotel ilioko chini ya kampuni nayofanyia kazi ilikuwa jirani na hio hotel nyengine, alinambia kuwa, wageni wake wengi walikuwa wanampelekea complain kuwa hotel ilikuwa na mauzauza.

Huko nlipokuwepo mwanzo kuna mzungu alikuwa na kihotel chake kidogo, alikuwa anaweka disco usiku afu kelele, wanakijiji wakamfuata na kumwambia aache, akawanyia mbovu. Bibi wa watu haikufika wiki alipatwa na upofu, alilia arudishwe kwao na mwenyeji wake, kufika kwao mwenyeji wake anasema bibi alianza kuona fresh. Hatamani kurudi :D
 
Duh
 
Kuishi visiwani kuna utamu wake
 
Siku moja jioni miaka kama 10 hivi iliyopita nilitinga jijini dar nikitokea mikoani. Nilishuka Ubungo stendi Na kudandia coaster ya kwenda Kariakoo.

Tulifika kariakoo Na nikashukia jirani Na kituo cha Polisi cha msimbazi. Kigiza kilishaanza kuingia.

Ndani ya ile coaster kulikuwa Na msichana amenivutia. Alikuwa amesimama mbali kidogo kutoka nilipokuwa mie hivyo nsingeweza kumsemesha kivyovyote.

Nikawa naombea ashukie mwisho wa basi nnaposhukia mimi halafu nijaribu kama anasemesheka.

Bahati kweli akashukia palepale msimbazi. Makusudi nikaacha atangulie kushuka halafu nifuate nyuma. Akashuka lakin alikuwa ameongozana Na Dada mwingine mkubwa kuliko yeye. Kwahiyo walikuwa wawili.

Mimi nikawa nafuata kwa nyuma huku nikifanya hesabu za kuungana nao. Walikuwa wanaelekea lilipo soko kuu la kariakoo.

Dada mtu hakuwa MTU mzima sana kwahiyo sikuwa Na waswas sana. Umri wao ulikuwa miaka 22 kwa 28 hivi.

Kilichokuwa kinanikwamisha nisiwakabili fasta ni kuwa watu walikuwa wapowapo hapo mtaani Na nilifikiri labda nisubirie sehemu isiyo Na watu wengi ndo nikaanze kujipendekeza. Lakini pia walikuwa wanatembea haraka haraka ajabu.

Nakumbuka Mara 2 au 3 niliwasemesha kutokea nyuma wakageuka kuniangalia halafu wakatizamana Na kuendelea Na safari yao.

Hali ya hewa haikuonekana kama ni mbaya ya kuweza kupigwa kibuti, kwahiyo nikawa nazidi kuwafuata

Mdogo mtu alikuwa anavutia kweli kweli. Na tukawa tulishakaribia sana soko LA kariakoo.

Ghafla bin vuu nikajishtukia nipo jirani na ilipokuwa round about ya mtaa wa Uhuru na msimbazi (makutano ya hiyo mitaa).

Kwanza sikujua kama Niko wapi. Ila nilijua nipo mtaa fulani hivi natembea. Nikazidi kutembea. Kuangalia mazingira na nilipozidi kwenda mbele ndo nikajua kumbe nipo jiran na mtaa wa Uhuru Na nimetokea nilikoshukia.

Kilichonishangaza ni kuwa ule haukuwa uelekeo wa safari yangu. Mimi nilikuwa nawafuata wale mabinti wawili waliokuwa wanaelekea soko kuu LA kariakoo wakiwa wametokea na Mimi karibu na msimbazi polisi. Nimefikaje fikaje huku Uhuru?

Any way, fasta nikachukua dala dala Tena nkaenda zangu keko kutafuta pa kulala guest

Japokuwa kipindi hicho nilikuwa nafanya kazi mikoani lakini nilishaishi mtaa wa shaurimoyo kwa miaka 15. Shaurimoyo na kariakoo ni pua na ndomo kwa ukaribu. Kuanzia buguruni mpaka mnazi mmoja maeneo hayo nayajua njema kabisa.

Mitaa ya kariakoo isingeweza kunichanganya. Kuna kitu kilinitokea. Unaenda huku unajishtukia uko kwingine
 
Dah imenikumbusha miaka ya 90s nikiwa Tabora wilaya moja hivi kijijini nikichukua elimu ya msingi shule yetu ilikuwa upande wa magharibi kuna makaburi halafu shule ina miti kibao ya mikaratusi,mikorosho mijohoro mizambarawe na miti fulani hivi inatoa ubani upepo ukipiga inavuma kama gari,

Dah nakumbuka hiyo siku niliamka kwenye kigheto changu pale home kama saa nane hivi mabalamwezi imekubali nje maana ilikuwa wiki ya mwalimu mmoja hivi kusimamia usafi na wechelewaji na ukichelewa unapata bakora za miguuni na lile baridi la kijijini balaa mwanaume mbalamwezi ile nikajua kumekucha nikanawa faster faster hata sikuwastua wazazi ambapo sio kawaida huwa lazima niwaamshe kwenye gheto lao mzee nikanyanyua ufagio mkononi na kidumu cha maji mbio kwenda kabla ya kufika shule kuna kipori fulani lazima ukipite ndio ufike shule mwanaume sikujari japo njiani sikuona mtu yeyote hiyo haikunistua mie nilijona mshindi leo nawahi namba shule,

aisee nimepita chini ya mikorosho na hiyo miti mingine bila kujari nahisi akili haikuwa yangu nakumbuka nafika shule nikakimbilia darasani nafika mlangoni nilichokishuhudia acha niliona moto mkubwa unawaka mule na kuna watu wamekaa kama wako kwenye kikao halafu wote wakaniangalia ila sura sikuziona hapo ndio akili ikarudi kwamba nimezingua niligeuka mbio kurudi home halafu ule upande wa makaburi nilishuhudia watu wakiwa na mguu mmoja wanaruka ruka kwa mstari mbio zangu nilikuwa nahisi kuna kitu nyuma kinanifata kugeuka nyuma niliona mtu mrefu sana kichwa hakionekani ila kavaa vazi refu linag'aa kama mbaramwezi ilivyokuwa inag'aa mwanaume niliongeza speed nilienda nikaingia na mlango mpk ndani yule jini sijui nini nilipokaribia nyumbani nilisikia msonyoo mmoja hatari sana wazazi wakaamka kufungua mlango kuja kunikuta sijitambui wakanichukua nikaenda kulala kwao asubuhi ndio kuwaelezea ni moja ya tukio ambalo huwa sipendi kabisa kulikumbuka maana baada ya hapo mpk leo kuna vitu huwa naviona ambavyo sio vya kawaida na niliwasumbua sana wazazi baada ya hapo . nimejaribu kufupisha ila kuna mambo mengi sana kwa ule usiku na miaka ile niliyashuhudia baada ya ilo tukio.
Kama ni URAMBO,basi shule ya msingi Mwenge
 
Back
Top Bottom