Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Kwa ushirikiano wa karibu na JamiiForums, tunatarajia kuanza kwa kipindi kipya kiitwacho 'Njoo Tuongee' ambacho kitahusisha mjadala na Mawaziri kutoka Serikalini kuhusiana na masuala ya wananchi.
Kwa muda wa wiki 7, Mawaziri mbalimbali watawekwa 'Kitimoto' LIVE kupitia Star TV ili kujibu maswali kutoka kwa wanaowaongoza.
Kipindi cha kwanza kitaanza kurushwa kesho (Ijumaa O3, 2017), SAA 12:30 JIONI na Waziri tutakayeanza naye atakuwa ni Mheshimiwa January Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira.
Lengo kuu la kipindi hiki ni kuwapa nafasi wananchi kujua wanachokifanya Mawaziri na kuwauliza ni wapi wanakwama katika kutatua changamoto mbalimbali.
Sasa kupitia JamiiForums, unaweza kuuliza maswali au kutoa maoni ambayo baadhi yao yatakayopata nafasi, yatakusanywa na kuwasilishwa kunakohusika kisha kuulizwa moja kwa moja kwa mgeni wa siku hiyo.
Je, una swali, maoni, jambo lolote unataka kuliwasilisha kwa Ndg. January Makamba?
Karibu sana..
--------
UPDATES > 3/11/2017..
Kipindi hiki kimetayarishwa na Twaweza kwa kushirikiana na Star TV, Compass Communications na JamiiForums.
Mgeni: January Makamba (Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano)
Watangazaji: Aidan Eyakuze na Maria Sarungi-Tsehai
UNAWEZA KUFUATILIA MJADALA HUU LIVE HAPA CHINI;
======
UPDATES:
Maria Sarungi: Katika kipindi hiki tutakuwa tunajikita katika taarifa zenye takwimu sahihi kabisa.
Swali: Mnafanyaje kazi kwa pamoja?
Majibu: Mwanzoni mazingira ilikuwa chini ya wizara ya maliasili na mazingira. Kwa sasa ipo chini ya ofisi ya Makamu ya rais.
Swali: Ilikuwaje mkatoa kibali cha ujenzi eneo ambalo lina mafuriko pale Jangwani?
Majibu(Makamba): Eneo hili lilipata kibali mahususi na waziri alijiridhisha kwamba eneo lile lisingeweza kuhatarisha maisha ya watu
Swali(Sarungi): Maeneo wanayoishi wananchi kuna uchafu, wizara yako imejipanga vipi kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira mazuri
Majibu(Makamba): Inabidi tupange mkakati mzuri ili tuweze kuhimili maafa katika mazingira yetu kwa kushirikiana na mamlaka zote. TANROADS, manispaa, TANESCO
Swali(Sarungi): Wizara imefikia wapi katika suala mbunge na Mchungaji Rwakatare kujenga katika eneo la mto na kuharibu uoto wa mikoko?
Majibu: Hilo swala lipo mahakamani na mpaka sasa linasubiria maamuzi yamahakama. Pia kwa wale waliokuwa wanabomolewa Mkwajuni bado shauri hilo halijaamuliwa.
Swali(Aidan): Ni hatua gani serikali imechukua kuambatanisha teknolojia kwenye mazingira?
Majibu(Makamba): Moja ya mambo yanayoweza kupunguza uharibifu wa mazingira ni matumizi ya nishati mbadala kwa mfano gesi asili
Swali(Aidan): Tumejiandaa vipi kutumia nishati rafiki?
Majibu(Makamba):Tumeandika sera mpya ya mazingira na katika sera hii tumeweka vichocheo vya teknolojia rafiki kama viwandani na kupikia. Vichocheo hivyo ni kurahisishaji uagizaji na uingizaji wa teknolojia rafiki.
Swali(Aidan): Una mkakati gani wa kuwarudishaia wananchi wa kibiti mazingira mazuri na kuendelea na shughuli zao?
Majibu(Makamba): Mkaa haupunguzi gharama ya nishati. Tunapoelekea tunaweka mkakati wa kuweza kupata nishati mbadala. Kuna mkaa unaotokana na taka au mabaki ya mazao. Nitakachofanya ni kuwajengea uwezo wajasiriamali hawa ili kuongeza uzalishaji
Swali: Ni lini gesi itapungua bei?
Majibu(Makamba): Gesi inayotumika inatoka kwa Mtwara kwa njia ya mabomba ambayo inasambazwa majumbani. Gesi inayotumia mitungi inatoka nje.
Swali(Aidan): Kenya na Uganda wamefanikiwa kuzuia mifuko ya plastiki na hakuna madhara. Nini mpango wa wizara yako.
Majibu(Makamba): Tumefanya ziara Rwanda na Zambia kuona jinsi walivyoweza kufanya na tumerudi tumefanya tathmini na suala hili linajumuisha wizara ya viwanda na nyinginezo. Kwasasa lipo katika mchakato wa kiserikali.
Swali(Aidan): Nini mchakakati wa serikali yako katika kuzuia kelele za mabaa, vigodoro na muziki.
Majibu: Tunachofanya ni kupokea malalamiko na kuyashughulikia. Kama baa imefuata makazi ya watu. Hata juzi kuna baa tumeifungia kule Dodoma.
Swali(Sarungi): Ulijisikiaje maamuzi juu ya NEMC kupinduliwa? Unafikiri una moral authority juu ya bodi ya NEMC?
Majibu(Makamba): Kwa kiongozi wa serikali kufanya maamuzi alafu wakubwa wako wakafanya tofauti ni jambo la kawaida.
Amabacho kilifanyika tulikubaliana wapewe nafasi nyingine kwa muda. Lakini mimi nina moral authority juu yao.
Swali(Aidan): Mmewahi kuwauliza wananchi kama kero za muungano zimetatuliwa?
Majibu(Makamba): Sheria ya haki za binadamu ilikuwa haitumiki Zanzibar. kwa haya mambo ya muungano
Swali(Sarungi): Kuhusu swala la tofauti tozo za kodi kati ya Zanzibar na Bara
Majibu(Makamba): Changamoto ni mifumo tofauti ya ukadiriaji wa kodi. Tulikubaliana iwekwe mifumo inayofanana katika ukadiriaji wa kodi. Na kwa sasa mifumo hiyo ishafungwa Zanzibar ili wananchi wasiendelee kutozwa hiyo tofauti ya kodi.
Swali(Aidan): Kuna mkanganyiko kati ya watanzania waishio bara na Zanzibar. Nini kifanyike kuondoa mkanganyiko huu?
Makamba: Dhana tuliyonayo katika kuunda muungano ni kutoua haiba ya Uzanzibar
Swali(Swali): Katika kushughulikia maswala ya muu, kunapaswa kuwepo ofisi sehemu zote mbili
Makamba: Ofisi zipo pande zote mbili.
Swali(Sarungi): Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja kwanini tuna serikali mbili?
Ni swala la muundo wa serikali na ilikubaliwa kuwe na serikali mbili.
Swali(Aidan): Je umejikita vipi kumbadilisha mwananchi tabia ili asiharibu mazingira?
Majibu(Makamba): Inahitaji falsafa ya kufungamanisha suala hili katika malengo yetu.
Swali(Aidan): Ipi unaipenda zaidi kati ya Mazingira na muungano? Na unaipangaje siku yako
Majibu(Makamba): Napenda sana mazingira na nimefungamana nayo hata nikistaafu katika wizara hii.
Muungano ni suala pana sana kitaifa na kimataifa na linanipa pia.
Wakati mwingine nakuwa Zanzibar na wakati mwingine nakuwa bara
~~~MWISHO~~~