Njoo tuongee na January Makamba: Asema nyumba ya mama Lwakatare inasubiri maamuzi ya mahakama kubomolewa

  • Thread starter Sauti za Wananchi
  • Start date

Sauti za Wananchi

Sauti za Wananchi

Member
Joined
Sep 2, 2014
Messages
95
Likes
103
Points
40
Sauti za Wananchi

Sauti za Wananchi

Member
Joined Sep 2, 2014
95 103 40
makamba-jan-jpg.622851

Kwa ushirikiano wa karibu na JamiiForums, tunatarajia kuanza kwa kipindi kipya kiitwacho 'Njoo Tuongee' ambacho kitahusisha mjadala na Mawaziri kutoka Serikalini kuhusiana na masuala ya wananchi.

Kwa muda wa wiki 7, Mawaziri mbalimbali watawekwa 'Kitimoto' LIVE kupitia Star TV ili kujibu maswali kutoka kwa wanaowaongoza.

Kipindi cha kwanza kitaanza kurushwa kesho (Ijumaa O3, 2017), SAA 12:30 JIONI na Waziri tutakayeanza naye atakuwa ni Mheshimiwa January Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira.

Lengo kuu la kipindi hiki ni kuwapa nafasi wananchi kujua wanachokifanya Mawaziri na kuwauliza ni wapi wanakwama katika kutatua changamoto mbalimbali.

Sasa kupitia JamiiForums, unaweza kuuliza maswali au kutoa maoni ambayo baadhi yao yatakayopata nafasi, yatakusanywa na kuwasilishwa kunakohusika kisha kuulizwa moja kwa moja kwa mgeni wa siku hiyo.

Je, una swali, maoni, jambo lolote unataka kuliwasilisha kwa Ndg. January Makamba?

Karibu sana..
--------

UPDATES > 3/11/2017..

Kipindi hiki kimetayarishwa na Twaweza kwa kushirikiana na Star TV, Compass Communications na JamiiForums.

Mgeni: January Makamba (Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano)
Watangazaji: Aidan Eyakuze na Maria Sarungi-Tsehai

UNAWEZA KUFUATILIA MJADALA HUU LIVE HAPA CHINI;

======

UPDATES:

Maria Sarungi: Katika kipindi hiki tutakuwa tunajikita katika taarifa zenye takwimu sahihi kabisa.

Swali: Mnafanyaje kazi kwa pamoja?

Majibu: Mwanzoni mazingira ilikuwa chini ya wizara ya maliasili na mazingira. Kwa sasa ipo chini ya ofisi ya Makamu ya rais.

Swali: Ilikuwaje mkatoa kibali cha ujenzi eneo ambalo lina mafuriko pale Jangwani?

Majibu(Makamba): Eneo hili lilipata kibali mahususi na waziri alijiridhisha kwamba eneo lile lisingeweza kuhatarisha maisha ya watu

Swali(Sarungi): Maeneo wanayoishi wananchi kuna uchafu, wizara yako imejipanga vipi kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira mazuri

Majibu(Makamba): Inabidi tupange mkakati mzuri ili tuweze kuhimili maafa katika mazingira yetu kwa kushirikiana na mamlaka zote. TANROADS, manispaa, TANESCO

Swali(Sarungi): Wizara imefikia wapi katika suala mbunge na Mchungaji Rwakatare kujenga katika eneo la mto na kuharibu uoto wa mikoko?

Majibu: Hilo swala lipo mahakamani na mpaka sasa linasubiria maamuzi yamahakama. Pia kwa wale waliokuwa wanabomolewa Mkwajuni bado shauri hilo halijaamuliwa.

Swali(Aidan): Ni hatua gani serikali imechukua kuambatanisha teknolojia kwenye mazingira?

Majibu(Makamba): Moja ya mambo yanayoweza kupunguza uharibifu wa mazingira ni matumizi ya nishati mbadala kwa mfano gesi asili

Swali(Aidan): Tumejiandaa vipi kutumia nishati rafiki?

Majibu(Makamba):Tumeandika sera mpya ya mazingira na katika sera hii tumeweka vichocheo vya teknolojia rafiki kama viwandani na kupikia. Vichocheo hivyo ni kurahisishaji uagizaji na uingizaji wa teknolojia rafiki.

Swali(Aidan): Una mkakati gani wa kuwarudishaia wananchi wa kibiti mazingira mazuri na kuendelea na shughuli zao?

Majibu(Makamba): Mkaa haupunguzi gharama ya nishati. Tunapoelekea tunaweka mkakati wa kuweza kupata nishati mbadala. Kuna mkaa unaotokana na taka au mabaki ya mazao. Nitakachofanya ni kuwajengea uwezo wajasiriamali hawa ili kuongeza uzalishaji

Swali: Ni lini gesi itapungua bei?

Majibu(Makamba): Gesi inayotumika inatoka kwa Mtwara kwa njia ya mabomba ambayo inasambazwa majumbani. Gesi inayotumia mitungi inatoka nje.

Swali(Aidan): Kenya na Uganda wamefanikiwa kuzuia mifuko ya plastiki na hakuna madhara. Nini mpango wa wizara yako.

Majibu(Makamba): Tumefanya ziara Rwanda na Zambia kuona jinsi walivyoweza kufanya na tumerudi tumefanya tathmini na suala hili linajumuisha wizara ya viwanda na nyinginezo. Kwasasa lipo katika mchakato wa kiserikali.

Swali(Aidan): Nini mchakakati wa serikali yako katika kuzuia kelele za mabaa, vigodoro na muziki.

Majibu: Tunachofanya ni kupokea malalamiko na kuyashughulikia. Kama baa imefuata makazi ya watu. Hata juzi kuna baa tumeifungia kule Dodoma.


Swali(Sarungi): Ulijisikiaje maamuzi juu ya NEMC kupinduliwa? Unafikiri una moral authority juu ya bodi ya NEMC?

Majibu(Makamba): Kwa kiongozi wa serikali kufanya maamuzi alafu wakubwa wako wakafanya tofauti ni jambo la kawaida.

Amabacho kilifanyika tulikubaliana wapewe nafasi nyingine kwa muda. Lakini mimi nina moral authority juu yao.

Swali(Aidan): Mmewahi kuwauliza wananchi kama kero za muungano zimetatuliwa?

Majibu(Makamba): Sheria ya haki za binadamu ilikuwa haitumiki Zanzibar. kwa haya mambo ya muungano

Swali(Sarungi): Kuhusu swala la tofauti tozo za kodi kati ya Zanzibar na Bara

Majibu(Makamba): Changamoto ni mifumo tofauti ya ukadiriaji wa kodi. Tulikubaliana iwekwe mifumo inayofanana katika ukadiriaji wa kodi. Na kwa sasa mifumo hiyo ishafungwa Zanzibar ili wananchi wasiendelee kutozwa hiyo tofauti ya kodi.

Swali(Aidan): Kuna mkanganyiko kati ya watanzania waishio bara na Zanzibar. Nini kifanyike kuondoa mkanganyiko huu?

Makamba: Dhana tuliyonayo katika kuunda muungano ni kutoua haiba ya Uzanzibar


Swali(Swali): Katika kushughulikia maswala ya muu, kunapaswa kuwepo ofisi sehemu zote mbili

Makamba: Ofisi zipo pande zote mbili.

Swali(Sarungi): Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja kwanini tuna serikali mbili?
Ni swala la muundo wa serikali na ilikubaliwa kuwe na serikali mbili.

Swali(Aidan): Je umejikita vipi kumbadilisha mwananchi tabia ili asiharibu mazingira?

Majibu(Makamba): Inahitaji falsafa ya kufungamanisha suala hili katika malengo yetu.

Swali(Aidan): Ipi unaipenda zaidi kati ya Mazingira na muungano? Na unaipangaje siku yako

Majibu(Makamba): Napenda sana mazingira na nimefungamana nayo hata nikistaafu katika wizara hii.
Muungano ni suala pana sana kitaifa na kimataifa na linanipa pia.
Wakati mwingine nakuwa Zanzibar na wakati mwingine nakuwa bara

~~~MWISHO~~~
 
Replica

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Messages
323
Likes
1,154
Points
180
Replica

Replica

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2017
323 1,154 180
Imepita miaka mingi nyumba ya mama Lwakatare haijabomolewa pamoja na NEMC kutoa notisi ya kuvunja nyumba kwa sababu za kimazingira ambapo inadaiwa ujenzi wake unazuia mto Numbwi na uko jirani na Mikoko, wizara imefikia wapi? Hawaoni kwamba watu waliobomolewa wanajisikia vibaya pamoja kuwa walikuwa na zuio la mahakama kama mama Lwakatare?
 
U

UKAWA2

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2014
Messages
2,106
Likes
1,546
Points
280
U

UKAWA2

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2014
2,106 1,546 280
Wataulizwa maswali kwa wananchi kupiga simu moja kwa moja au watakuwa wanapewa maswali wanalala nayo alafu wanakuja kupiga poyoyo hapo. Kama maswali yataulizwa moja kwa moja na wannchi kwa njia ya simu,hicho kipindi ijumaa ndio itakuwa mwanzo na mwisho wake.
 
beth

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
1,010
Likes
1,459
Points
280
beth

beth

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
1,010 1,459 280
Imepita miaka mingi nyumba ya mama Lwakatare haijabomolewa pamoja na NEMC kutoa notisi ya kuvunja nyumba kwa sababu za kimazingira ambapo inadaiwa ujenzi wake unazuia mto Numbwi na uko jirani na Mikoko, wizara imefikia wapi? Hawaoni kwamba watu waliobomolewa wanajisikia vibaya pamoja kuwa walikuwa na zuio la mahakama kama mama Lwakatare?
Unaota wewe. Hilo jengo halitakaa liguswe maana hata Magufuli kamteua huyo mama kwa moyo safi kuwa Mbunge viti maalumu.. Kuna watu na viwatu!
 
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Messages
493
Likes
864
Points
180
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2017
493 864 180
Mkuu how shuld we trust u. Ungejitambulisha ikiwa wewe ndo January au host husika. Intro yako inaelea bado
 
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Messages
493
Likes
864
Points
180
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2017
493 864 180
Unaota wewe. Hilo jengo halitakaa liguswe maana hata Magufuli kamteua huyo mama kwa moyo safi kuwa Mbunge viti maalumu.. Kuna watu na viwatu!
Aktaka ibomolewe ahamie upinzani kwanza. Hivi yale masaa aliyotoa kangi yataisha lini
 
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
13,530
Likes
11,363
Points
280
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
13,530 11,363 280
Unaota wewe. Hilo jengo halitakaa liguswe maana hata Magufuli kamteua huyo mama kwa moyo safi kuwa Mbunge viti maalumu.. Kuna watu na viwatu!
Correction: Rwakatare hajateuliwa na Rais Magufuli kuwa mbunge bali ametokana na viti maalumu vya UWT!!
 
J

Jua usiyoyajua

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
853
Likes
381
Points
80
J

Jua usiyoyajua

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
853 381 80
Kuna kauli mbalimbali Mheshimiwa Waziri amezitoa katika vipindi mbalimbali vya bunge la bajeti kuhusiana na kupiga marufuku mifuko ya Plastiki, kauli hizo zimeshindwa kutekelezwa hadi sasa pamoja na athali kubwa kwenye mazingira zinazosababishwa na mifuko hii. Je Waziri analipi la kutwambia juu ya hatima ya jambo hili katika nchi yetu?
 
M

MAGALLAH R

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Messages
409
Likes
406
Points
80
M

MAGALLAH R

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2014
409 406 80
Kwa kiwango gani swala la kuzuia uuzwaji wa viroba limesaidia kutunza mazingira?

Na je upi mkakati wa serikali juu ya kuzuia upigaji wa kelele zilizopitiliza kwenye makazi ya watu? Kwani mabaa, vigadoro, kelele za miziki imekuwa kero sana kwenye mitaa
 
beth

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
1,010
Likes
1,459
Points
280
beth

beth

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
1,010 1,459 280
Aktaka ibomolewe ahamie upinzani kwanza. Hivi yale masaa aliyotoa kangi yataisha lini
Achana na hayo.. Mimi swali langu kwa Mheshimiwa Waziri ni kuhusu tatizo la kule Kibiti.

Gazeti la Mwananchi liliwahi kuripoti kuwa chanzo cha vurumai za kule, pamoja na mambo mengine, ni wananchi kuzuiwa kufanya shughuli za mazao ya rasilimali (mainly kukata mkaa) na kunyang'anywa baadhi ya mali zao na watendaji wa kule..

Je,yeye akiwa kama Waziri, ana mkakati gani wa kuwarudishia wananchi wa Kibiti mazingira mazuri ya kufanya shughuli za kuwaingizia kipato ikiwemo ukataji wa mkaa kwa sababu ndio biashara kuu kwa eneo husika?
 
F

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Messages
1,957
Likes
1,486
Points
280
F

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2017
1,957 1,486 280
Namuuliza January Makamba ni lini bei ya gesi inayopatikana humu nchini itashuka ili kila mwananchi atumie kupikia na kuepuka matumizi ya mkaa na kuni ambazo ndiyo chanzo cha uharibifu wa mazingira?
 
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Messages
493
Likes
864
Points
180
makinikia 101

makinikia 101

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2017
493 864 180
Hao ni host wa hicho kipindi. Fuatilia threads zao za nyuma ni watu serious..
Oohh okay sawasawa.
Mhrshimiwa atupe majibu ya nyumba ya Rwakatare, nyumba za kimara na nyumba za mwanza. Kimsingi kuna majibu mengi hapa kuliko maswali
 
OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Messages
24,821
Likes
22,483
Points
280
OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
24,821 22,483 280
Tunamtaka Magufuli mwenyewe na ahadi zake hewa
 
Z

zenarrator

Member
Joined
Mar 22, 2016
Messages
13
Likes
8
Points
5
Age
28
Z

zenarrator

Member
Joined Mar 22, 2016
13 8 5
Kutokana na kupanda kwa bei ya gesi kila wakati wizara yake inachukua hatua gani kupambana na hili swala ukizingatia kwamba matumizi ya gesi ndio yangeweza kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambavyo vinachochea ukataji miti (uharibifu WA mazingira)?
 
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Messages
27,437
Likes
60,767
Points
280
Age
21
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2014
27,437 60,767 280
Miaka ya nyuma kidogo ilikuwa ukitembea unakutana na hali nzuri ya mazingira nikiwa na maama ya uoto wa asili lakini kadri miaka inavyozidi kwenda ukame unazidi.

Licha ya changamoto za mabadiliko ya kimazingira duniani wizara imejipangaje kupunguza hii hali ? Au imekubali kisa tu ni tatizo la dunia nzima? Elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari haitoshi waende hadi mashinani mtaa kwa mtaa nchi zitbaki jangwa.
 

Forum statistics

Threads 1,235,993
Members 474,928
Posts 29,242,644