Njoo tujifunze kuweka ROM mbalimbali

Kilangi masanja

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
4,184
4,538
Wadau habari za siku, naimani mko njema na siku zinaenda kwa uwezo wake aliye juu.

Kumekuwa na utofauti sana wa kimatumizi ya vifaa vyetu vingi vya mikononi (hasa simu). Imefika kipindi mtu ananunua kifaa flani ambacho pengine kwa namna moja au nyingine hakimvutii kimuonekano ila kwa kutokujua kuwa alikuwa ana uwezo pengine wa kuweka Roms zingine na simu ikawa na muonekano mwingine kabisa.

Binafsi niko kwenye hatua za awali kabisa za kujifunza namna bora ya uwekaji wa roms kwa simu mbalimbali.
Ningependa uzi huu uwe endelevu na tupate mafunzo mbalimbali ya namna na hatua madhubuti ambazo tutazitumia kuwezesha zoezi hili.

Naimani kubwa kuwa humu jukwaani wako wajuzi kibao tu ambao wana ujuzi wa kutosha wa kuweza kukamilisha hili zoezi hivyo karibuni sana.

Mtusaidie
 
Wewe umefikia wapi juu ya hilo? Au umeweza kufanya hiyo kazi kwenye simu zipi?
Nipo hatua ya mwanzo kwa maana nipo nakomaa na tutorial za wahindi youtube kuzidi kuongeza maarifa ,binafsi sijapata simu ambazo niko risky kuitoa kama ya demo. .Kama unalolote ulijualo unaweza kuongezea
 
Naona ROM hujaijua bado na hapo unapotuita tuje kujifunza ni kipi hicho ?
km somo ni lingine basi ukitoka kwa hao wahindi naomba uje ufafanue hioz ROM ni zipi?
1621342474470.png
 
Hyo ni mada ndefu sana boss. Unatikwa ujue kuhusu:

Mambo ya custom recovery na jinsi ya kuzitumia,

Untakiwa kujua jinsi ya kupata custom ROMs

Unatakiwa kujua jinsi ya kunlock bootloader ya simu yako na kma inawezekana. Kwa mfano Xiaomi lazima u request unlock code usubiri week 2 au zaidi

Unatakiwa kujua jinsi ya kubackup na ku recovery operating system ili mambo yasipoenda sawa uwe na uwezo wa kurudisha kama ilivyo mwanzo. Kutumia Sp flashtool for MTK, Mi flash tool, QFIL flash tool, Odin, nk kutokana na model ya simu yako.

Hayo no baadhi tu. Comment moja haiwezi kukupa maelezo yote yanayohitajika.
 
Wakuu hebu naombeni msaada ni rom gani ambayo naweza weka kwenye xiaomi redmi note 3 ambayo haina bugs sana.
Ila iwe android 9 mpaka 10
 
Hyo ni mada ndefu sana boss. Unatikwa ujue kuhusu:

Mambo ya custom recovery na jinsi ya kuzitumia,

Untakiwa kujua jinsi ya kupata custom ROMs

Unatakiwa kujua jinsi ya kunlock bootloader ya simu yako na kma inawezekana. Kwa mfano Xiaomi lazima u request unlock code usubiri week 2 au zaidi

Unatakiwa kujua jinsi ya kubackup na ku recovery operating system ili mambo yasipoenda sawa uwe na uwezo wa kurudisha kama ilivyo mwanzo. Kutumia Sp flashtool for MTK, Mi flash tool, QFIL flash tool, Odin, nk kutokana na model ya simu yako.

Hayo no baadhi tu. Comment moja haiwezi kukupa maelezo yote yanayohitajika.
Hapo kwenye back up nakazia na chaji iwepo ya kutosha kwenye simu, nakumbuka niliweka lineage os kwenye Sony z3 compact, ika brick ikagoma kupeleka hadi chaji MUNGU mkubwa ilikuwa na chaji, nikatumia pc kuiflash kwa kurudisha stock rom, ambayo ilibidi nidownload ko ni inshu ya kua makini sana.
 
Wadau habari za siku, naimani mko njema na siku zinaenda kwa uwezo wake aliye juu.

Kumekuwa na utofauti sana wa kimatumizi ya vifaa vyetu vingi vya mikononi (hasa simu). Imefika kipindi mtu ananunua kifaa flani ambacho pengine kwa namna moja au nyingine hakimvutii kimuonekano ila kwa kutokujua kuwa alikuwa ana uwezo pengine wa kuweka Roms zingine na simu ikawa na muonekano mwingine kabisa.

Binafsi niko kwenye hatua za awali kabisa za kujifunza namna bora ya uwekaji wa roms kwa simu mbalimbali.
Ningependa uzi huu uwe endelevu na tupate mafunzo mbalimbali ya namna na hatua madhubuti ambazo tutazitumia kuwezesha zoezi hili.

Naimani kubwa kuwa humu jukwaani wako wajuzi kibao tu ambao wana ujuzi wa kutosha wa kuweza kukamilisha hili zoezi hivyo karibuni sana.

Mtusaidie
Custom ROMs, ported ROMs and GSI ROMs..sijasomea wala nini ila nipo njema xana
 
Mzee hebu zitofautishe basi, ili tupate kujua tofauti ya hizo 3
Custom ROMs ndio zipo toka mda. Hizi ni kwamba developers wametengeneza kutoka kwenye source code na zinatengenezwa kwa device husika

Ported ROMs ni custom ROMs zilizochukuliwa kutoka hapo juu na kufanyiwa marekebisho ili ziweze kufanya kazi kwenye unsupported phones.

GSI (Generic system images) - hii kitu ilikua introduced na Android 8 kupitia project treble. Inakua image inayo contain system partition tu na inategemea partition zingine zote kutoka kwenye firmware ya simu. Hizi ni popular sana sikuhizi maana hata Google nao wanatoa GSIs. Right now kuna GSI kutoka kwa Google ya Android 12 beta.
GSI ndio step ya kwanza kma mtu unataka kujua mambo ya kuflash custom ROMs. Zipo nyingi sana na hata kwenye Tecno na Infinix zenye Android 8 kwenda juu zina support.
Shida ya hizi ni kwamba kunakua na bugs hasa kwenye simu za MTK kma tecno and infinix ila bado zipo vizuri tu.

sGSI (semi Generic system image) - hii ni kma GSI ila ni ported kufanya kazi na simu nyingi. Kwa mfano GSI wanazotoa Google zinagoma kufanya kazi kwenye baadhi ya simu hvyo sGSI zinarekebisha hayo. Pia kwenye sGSI ndio unakuta GSI za firmware ya simu nyingi. Kwa mfano kuna sGSI za OneUI ya Samsung, MIUI ya Xiaomi, OxygenOS ya Oneplus n.k ambazo unaweza install kwenye simu yoyote hata kma sio ya company husika. Unaweza install OneUI ya Samsung kwenye Xiaomi.

Kuna mambo mengine ya custom kernels, custom vendors n.k. ambayo ni mada nyingine hyo
 
Back
Top Bottom