Njonjo Mfaume na Demokrasia yetu


V

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Messages
4,140
Likes
2,559
Points
280
V

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2014
4,140 2,559 280
Njonjo Mfaume ni miongoni mwa wachambuzi mahiri wa siasa na jamii. Nathubutu kusema kuwa ingawa bado kijana, Njonjo ni miongoni mwa wachambuzi huria na makini wachache sana nchini maana huwezi kumkamata na kumuhukumu kuwa anaunga mkono Chama gani cha siasa nchini. Huo ndio usomi.

Ktk Gazeti la Mwananchi leo Julai 9, 2016, Gazeti la, and Njonjo ameandika makala ya siasa isemayo: Kwa mwendo huu, kesho Wapinzani wajipange upya. Kichwa cha habari 'kinatisha' na kama makala hii ingeandikwa na Ruttashobolwa, Barbarosa, Yehodaya, Simiyu yetu au Lizaboni wa hapa JF, ungeweza pasi na shaka kutabiri anazungumza kwa mlengo upi - yaani kuwaponda tu Wapinzani wa CCM na kuusifia utawala wa JPM, lkn la hasha, and Njonjo hamaanishi hilo.

Njonjo (nanukuu yale nayoamini kuwa yuko sahihi), anaandika kuwa : 1. Ktk historia ya Vyamavingi huu ni wakati MGUMU ZAIDI na wa majaribu makubwa kwa demokrasia kwa kuwa Katika kipindi hiki, and watawala siyo tu wanakiuka kanuni za kidemokrasia, and lkn wameenda mbali zaidi hadi kutoa amri zinazoonekana kupingana na sheria.
2. Huu ni muda wa kazi tu kiasi kwamba watawala hawataki hata televisheni zionyeshe matangazo ya Bunge moja kwa moja kwa kuhofia kazi hazitafanyika.
3. Zamani watawala walikataa mikutano ya kisiasa kwa hoja za kuhatarisha amani. Hawakusema mikutano haistahili kufanyika. Sasa tunaambiwa mikutano ya siasa mpaka mwaka 2020.
4. Huko nyuma, hasa Awamu ya nne, and Rais hakuwa mwepesi kutoa msimamo na hivyo kulikuwa na matumaini kuwa anaweza kuombwa kuingilia kati kutafuta suluhu. Kwa sasa uongozi ni sehemu muhimu ya mgogoro na hivyo matumaini ya suluhu ni madogo labda aamue kubadili msimamo.
5. Utawala wa CCM wa sasa unaamini kuwa suala la Wapinzani kususa sio tatizo kabisa na kuwa wanaweza kuendesha nchi wao wenyewe kwa ufanisi mkubwa. Kwa hiyo, CCM Zanzibar inaendelea mambo bila ushiriki wa aina yoyote wa Chama cha Wananchi CUF. Huku Bara ktk kipindi muhimu cha Bajeti, Wapinzani walisusa kushiriki na CCM waliendelea na shughuli za Bunge kama vile hakuna tatizo lolote. Hii inaitwa, 'Mkisusa twala'.
6. Licha ya kutoa amri zinazoonekana kukiuka sheria, lkn watawala wanatumia kanuni kuwabana na kuwadhibiti Wapinzani kila wapatapo upenyo bila kuzingatia malengo makuu na busara.

Nimechagua kubandika hoja hizo chache kwa kuwa Watanzania wote wasio na mitizamo ya kiitikadi na wapenda demokrasia, tutaona mapungufu haya ktk utawala wa sasa, hizo na kwa ajili ya mustakabali na maslahi mapana ya Taifa, ni vema watawala na wanasiasa wetu wakayaangalia haya.

Vv
 
kipara kipya

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Messages
5,392
Likes
5,393
Points
280
kipara kipya

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined May 2, 2016
5,392 5,393 280
kwa kuyachagua haya tu,umeshajionyesha rangi yako halisi!
 
M

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Messages
2,886
Likes
1,341
Points
280
M

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2011
2,886 1,341 280
Obuma

Obuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Messages
2,722
Likes
5,051
Points
280
Obuma

Obuma

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2015
2,722 5,051 280
Mleta mada kama hukuweza kupost makala yote ungeacha tu,piga picha gazeti upload watu wajisomee wenyewe. Habari ikipitia mtu wa kati inakuwaga imeshanajisiwa
 
V

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Messages
4,140
Likes
2,559
Points
280
V

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2014
4,140 2,559 280
Mleta mada kama hukuweza kupost makala yote ungeacha tu,piga picha gazeti upload watu wajisomee wenyewe. Habari ikipitia mtu wa kati inakuwaga imeshanajisiwa
Kichwa chake cha habari kinasema WAPINZANI WAJIPANGE UPYA

Kwa kubandika niliyobandika na ukihusisha na kicha cha habari Wapinzani wajipange upaya nadhani kinajieleza chenyewe.

Vv
 

Forum statistics

Threads 1,235,531
Members 474,641
Posts 29,225,775