Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,797
- 11,959
Watu wane wamenusurika kifo baada ya kutokea mlipuko mkubwa uliyosababishwa na simu ndani ya bajaji yenye nambari za usajili MC 567C JK-TVC katika barabara ya Njombe -Songea .
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mkasa wa betri kulipuka umeleta taharuki kwa abiria na kusababisha dereva kuacha usukani na kupelekea chombo kuacha njia na kupinduka.
Issa amesema punde baada ya ajali hiyo kutokea askari ambao walikuwa wanalinda moja ya bank mjini Njombe wakafika kufanya uokozi na kuwakuta abiria wakiwa wamejeruhiwa na kuamua kuwakimbiza hospitali.
Katika hatua nyingine Kamanda ameshangazwa na kitendo cha mmiliki wa bajaji kumfata mmiliki wa simu na kumtaka amlipe gharama za ukarabati wa bajaji jambo ambalo ni ukosefu wa uungwana.